Jonas Mkude inabidi apewe heshima yake

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Hellow JF

Kipindi kile waliposema jamaa ana matatizo ya akili hadi wakamsafirisha kwenye matibabu alitangazwa kwenye media sana.

Lakini kiukweli huyu jamaa Jonas Mkude tokea arudishwe kwenye kikosi amekuwa bora sana anaupiga mwingi pale kati lakini hawampi ile sifa anayostahili kwenye media shida ni nini hasa?

Kwa mtazamo wangu nilitegemea SSC wampe haki yake hadharani sio tu kwenye mabaya ndiyo wanatangaza kwa maana hiyo wanasubiri hadi afanye madudu ndiyo wayaseme mzani inabidi ubalance kote kote au hawaoni anayofanya pale kati ya dimba tokea arudi kikosini?


 
Wanasubiri achelewe kambini au alewe waanze kuchonga.
 
Mkude ni mchezaji wa kulipwa anavyoishi sasa na kutimiza majukumu yake ndivyo inavyopasa kuwa.

Hayuko pale kula mshahara huku akishindwa kutimiza wajibu wake na kuonesha utovu wa nidhamu.

Haifanyii timu hisani bali anapambania mshahara wake na wala hiyo sio akiba ili akiboronga aangaliwe tu.

Kwa ishu ya kumsifia nadhani wewe tayari umeshaonesha njia.
 
Mkude ni mchezaji wa kulipwa anavyoishi sasa na kutimiza majukumu yake ndivyo inavyopasa kuwa. Hayuko pale kula mshahara huku akishindwa kutimiza wajibu wake na kuonesha utovu wa nidhamu...
nimeonesha njia lakini kiofficial zaidi ndiyo inapendeza hata mchezaji mwenyewe anaona kumbe hata club ipo pamoja nami kwenye shida na raha
 
angekuwa anafanya kazi bure angesifiwa sana.... lakini kama analipwa mshahara atasifiwa na mkewe na mademu anaowahonga.... UMEELEWA??
 
angekuwa anafanya kazi bure angesifiwa sana.... lakini kama analipwa mshahara atasifiwa na mkewe na mademu anaowahonga.... UMEELEWA??
we jamaa wewe kipindi kile tulivyokuwa tunamsifia Chama vipi alikuwa analipwa mshahara au alikuwa anacheza bure??
 
Kwani anafanya hisani au?
Ni pro anafanya yanayotakiwa kufanywa.
Kwa kuwa huwa unachelewa kazini unalaumiwa na kutishiwa kufukuzwa.
Siku ukiwahi unatakiwa kusifiwa?
Afu mkude kapewa mchezaji bora december, unataka sifa gani?
hata kazini mtu akifanyakazi vizur huwa anapongezwa kumpongeza mtu anapofanya vizur ni mojawapo ya motisha mzee

Yah kwa muungwana atakupongeza kwa kubadilika na kuwahi kazini ila kwa ambaye sio muungwana atapiga kimya ataona kuwa n jukumu lako
 
Ulitaka afanyiwe nini? Kwa hiyo ulitaka asichukuliwe hatua alipoharibu? Sasa hivi kajitambua angalau lakini siyo jukumu la taasisi ya Simba kuanza kumuomba radhi.

Simba na washabiki wa Simba SC wanatambua mchango wake kwenye club.
 
hata kazini mtu akifanyakazi vizur huwa anapongezwa kumpongeza mtu anapofanya vizur ni mojawapo ya motisha mzee

Yah kwa muungwana atakupongeza kwa kubadilika na kuwahi kazini ila kwa ambaye sio muungwana atapiga kimya ataona kuwa n jukumu lako
Ndio maana kapewa tuzo mchezaji bora wa mwezi, au mkuu ulikuwa unapewe nini?
Nyumba au gari.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Sasa bro apewe haki kama ipi...!!!!!? Kusifiwa mitandao or!!!? sijaelewa haki gani unaizungumzia
kipindi kile ana matatizo kila mtanzania alilijua hilo na sasa hivi kwa vile anafanya vizur ilipaswa kila mtanzania ajue pia hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…