Nimemwangalia YouTube nimeiona baadhi ya matatizo kwenye filamu ya Agent Bravo, hawapo serious kuanzia yeye na waandaaji wa hiyo filamu. Laiti wakiwa serious watafika mbali zaidi ya hapo.
Kwanza star wa hiyo filamu, huyo jamaa nilichokiona ni mtaalamu wa mapigano pia action choreographer ni mzuri mno hilo nilipongeze hilo jambo..... Ila uigizaji ni tatizo nililoliona, wengi hawajapatendea haki kiasi cha kujenga uhalisia. Yaani inaonekana kabisa wanaigiza, hata body language kwa waigizaji hilo ni tatizo mno.
Haya yametokana na kuchukuliwa watu wenye ujuzi mdogo, au kutojiandaa kwa muda mrefu ili wawe tayari.... Nchi za wenzetu watu wanapewa script miezi kabla ya kushoot, muda wote huo wanafanya kazi ya kukariri script na baadhi ya matendo kama vile mwanafunzi anajiandaa kujibu mtihaniwa taifa.. Kupata kilicho bora umakini ni muhimu.
Nikija kwenye jopo la watu wasiyoigiza, kusema kweli mshika kamera kazingua hiyo movie. Hiki ndiyo kinaangusha filamu nyingi mno, yaani hata wachukua video za wasanii wa muziki wanamshinda. Huyo anapaswa atambue hii ni filamu, umakini ni mkubwa mno. Wahariri nao hawakuwa serious kabisa, haswa upande wa video editing. Rangi siyo poa hiyo,
Kiujumla idea ni nzuri, movie ni nzuri ila watu waliyohusika kuigiza au kuandaa baadhi wamezingua