Elections 2010 Jopo la CCM (taifa) kutua Arusha muda wowote kuanzia kesho

Elections 2010 Jopo la CCM (taifa) kutua Arusha muda wowote kuanzia kesho

Hapo ni watu wamekichoka CCM au viongozi walioko madarakani?

Maana kaa ukijua pia ndani ya CCM kuna viongozi safi sana ambao nao wanaitaji mabadiliko sana esp Nyamagana na Arusha pia, Ila kumekuwa na

Mkuu hapo kwenye red
1-huwezi kuwa ndani ya basi linalopinduka ukajifanya eti kuliokoa lisipinduke, lazima litapinduka na kama ni mauti, itakukuta
2-huwezi kutumbukia au kuwa kwenye shimo (choo) la mavi usipakae mavi.

Hao viongozi unaodai ni wasafi ni wanafiki na ndio wabaya, nchi hii inahitaji roho ya kishujaa ili ibadilike. Hao nao ni mafisadi tu, kuna vimirija vyao huko. Hawafai waondoke katika utawala pia au wahame ccm. Period!!!
 
Wana JF,

Vipi Huko Mbeya Mr.II anaendeleaje na kampeni za huko na wana CCM? nasikia joto ni kali mbaya pia huko?
 
Huyo Makamba ndio kwanza anaenda kuharibu mambo!
 
Hao viongozi unaodai ni wasafi ni wanafiki na ndio wabaya, nchi hii inahitaji roho ya kishujaa ili ibadilike. Hao nao ni mafisadi tu, kuna vimirija vyao huko. Hawafai waondoke katika utawala pia au wahame ccm. Period!!!

Ivi unajua ki ukwelii watakao wapigia kura watu wa upinzani na wakashinda ni wanachama wa CCM? na huko huko ndani ya CCM kunaviongozi shujaaa ambao wanapingwa kila kukicha kama wakina Mwakyembe, si dhani ni maslahi tu kuna wengine wanania nzuri kabisa na chama wanataka wakinusulu kuwatoa hao mafisadi na mabadiliko yanaenda taaaratibu tuu na itawafikia hao mafisadi wakubwa ndani ya CCM na watatoka bila ubishi zao 40 zinahesabika tuu bira shaka.

Me nadhani ni mbinu gani zitumike kwa wanaCCM safi kuhakikisha kuwanyofoa hao mafisadi PAPA

Sio siri sisiem wana hali mbaya,hizo fedha zote wanazotumia si ingekua vizuri kama wangewasaidia wananchi na kujenga vitu vya jamii kwa ujumla,leo hii wangekua safi lakini ona ama kweli ujuha wetu tuuondoe kwa kumpa kura Dr.SLAAAAAAAAA na wabunge wake kila sehemu ya nchi hii jamani tuondoeni UJUHA sisiem imechemsha.
 
CCm wanatafuta shuka wakati kumeisha kucha CCM basi,basi basi basiiiii na ukimwangalia mtu aliyetumwa huko Kichekesho Makamba!!!!!!!!!!!!! ananini kipia mbali na kauli zinazoendelea kuiangusha CCMMUNGU IBARIKI TANZANIA
Wana JF,

Kwa taaaarifa ya kutoka kwa mtu wangu wa karibu huko Dar ameniambia Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba Kutua Arusha muda wowote kuanzia kesho akiongozana na Jopo la wana CCM Taifa wengine.

Na hii ni dhahili kuwa huko Arusha ndiko kuna upinzani wa hali ya juuu sana na nguvu nyingi ya CCM imemwagwa huko kwa kuwa hakuna matumaini yeyote ya CCM kushinda kilahisi.

Kwani tunavyosikia kila kukicha vijana wengi ni kunyoosheana vidole viwili kuashiria wataipikia kura CHADEMA na hiii yote ni kuwepo na mapungufu ndani ya CCM wilaya ya Arusha esp viongozi wa CCM kutofautiana kwa hali kubwa.
Pili ni Kampeni ya Batilda ina ndugu wengi kuliko wanachama wa CCM.
Tatu Serikali ya CCM haijafanya cha maana cha kuwavutia vijana wengi kukipigia kura CCM na wanataka mabadiliko na hii ni kuwapo kwa uongozi mbovu katika mkoa huo kichama/Kiserikali.

Kutatua hilo ni kuunganisha vijana wa mji huo kuanzia UVCCM na vijana wengine kwani sasa twasikia kuwa kuna uhasama kati ya vijana wanao support CCM ambao ni wachache sana na wanatumia ubabe kwa wale vijana wanao support CHADEMA.

Pia watizame Athari ya kisiasa baada ya uchaguzi katika jimbo hili maaaana litaacha chuki na ugonvi wa hapa na pale.
 
Huyo Makamba ndio kwanza anaenda kuharibu mambo!

Hapa naweza nikakuelewa pia maana najua hana diplomacia ya kisasa ya kusuruhisha mambo ndani ya CCM kabisaa bali ni blaaa blaaaa nyingi na command za kibabe kama alizozifanya kule Tarime kipindi cha uchaguzi mdogo na aangalie safari hii watamrecord kama atarudia kuwa tukana wana chadema kwa ishara ya vidore, na gharama za kulikomboa hilo Jimbo nadhani zitazidi zile za kule Tarime kipindi hiki namgoje Pius Msekwa atasema nini kwa hili la Arusha maana sija msikia kabisa kwenye hilo sakata la Jimbo la Arusha

CCM hawajajifunza tu walienda Kilimanjaro - Moshi Mjini na kundi lao la ze komedy watu wakajaa kuangala ze komedy waliposhuka jukwaani alipopanda JK watua wakatawanyika wote wakabakia wale wenye kungojea usafiri na posho, wakajisifu wamekusanya watu wengi wakati kiu ya wakazi wa moshi ilikuwa kuona ze komedi live sio kusikiliza sera za ccm
 
Je ni nini Tatizo hapa esp Kwa Arusha na Nyamagana? Ni Kuwa chama CCM ndicho chenye matatizo? Au ni Viongozi wanao Kiongoza chama ndioa Chanzo cha matatizo? Na kupelekea vijana wengi kusupport Opposition? Na Je ni Hatua gani hawa CCM (viongozi) wajirudi vipi kukubali mabadiliko na wapewe nafasi na hawa vijana ili wawapigie Kura kwa kipindi hiki kilicho baki? Maana Tusije sawa wakapewa upinzani Jimbo ndio niwatanzania wenzao je nao wakishindwa timiza hayo ya vijana wa kizazi kipya iweje?

Kwa kuwa CCM siyo chombo kama gari au baiskeli bali ni mkusanyiko wa watu wanaoongozwa na itikadi moja. Hivyo tatizo lipo ndani ya watu wenyewe walioko ndani ya chama, ambao wengi wao wanamasikio na wanasikia lakini hawatafakari, wana macho yanaona lakini haelewi kile wanachokiona; na wamejigeuza kuwa wasanii; ndiyo sababu hasa inayowafanya watu kupendelea vyama vingine shindani. Kumbuka ni asilimia ndogo tu ya watanzania wenye umri wa kupiga kura ambao ni wanachama wa vyama vya siasa; na ndani ya hao wanasiasa wapo wanaolitanguliza kwanza taifa; na siyo chama kama wasanii wa hicho chama chenye rangi za njano na kijani kinavyotamani mambo yawe. Yaani hata ukiambiwa uchague mavi kati ya chakula uwe tayari kula mavi ili mradi tu yametoka ndani ya chama chako. Hii ni dalili tosha ya walevyi wa madaraka wanaoamini kuwa wanaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati wote. Generation Y imeliona hilo na haijalipokea; Makamba anajua, JK anazotaarifa na Salma pia ujumbe wa hii generation Y anao.

Watakaochaguliwa hawaji kujenga nchi wao wenyewe, watashirikiana na waliowachaguwa ili kusukuma gurudumu la maisha yao; hivyo usitegemee kukatishwa tamaa kwa hicho kizazi; bali tegemea mambo makubwa zaidi. Tanzania tajiri inawezekana.
 
tisishangilie in advance.
twendeni mstari wa mbele kuhakikisha tunashinda this tyme.
CCM wapo chali na sasa wanatumia last breath kujihakikishia maisha
 
Kwa kuwa CCM siyo chombo kama gari au baiskeli bali ni mkusanyiko wa watu wanaoongozwa na itikadi moja. Hivyo tatizo lipo ndani ya watu wenyewe walioko ndani ya chama, ambao wengi wao wanamasikio na wanasikia lakini hawatafakari, wana macho yanaona lakini haelewi kile wanachokiona; na wamejigeuza kuwa wasanii; ndiyo sababu hasa inayowafanya watu kupendelea vyama vingine shindani. Kumbuka ni asilimia ndogo tu ya watanzania wenye umri wa kupiga kura ambao ni wanachama wa vyama vya siasa; na ndani ya hao wanasiasa wapo wanaolitanguliza kwanza taifa; na siyo chama kama wasanii wa hicho chama chenye rangi za njano na kijani kinavyotamani mambo yawe. Yaani hata ukiambiwa uchague mavi kati ya chakula uwe tayari kula mavi ili mradi tu yametoka ndani ya chama chako. Hii ni dalili tosha ya walevyi wa madaraka wanaoamini kuwa wanaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati wote. Generation Y imeliona hilo na haijalipokea; Makamba anajua, JK anazotaarifa na Salma pia ujumbe wa hii generation Y anao.

Watakaochaguliwa hawaji kujenga nchi wao wenyewe, watashirikiana na waliowachaguwa ili kusukuma gurudumu la maisha yao; hivyo usitegemee kukatishwa tamaa kwa hicho kizazi; bali tegemea mambo makubwa zaidi. Tanzania tajiri inawezekana.

Hoja Safi,

Vijana wa hayo majimbo wapo tayari kwa hayo mabadiliko watapiga kura ya mabadiliko kweli??? ndilo linalo nisibu saaaana kuona Y Generation ina taaabika na uwezo huo tunao sasa sijui kama hiii iko akilini mwa vijana wenzetu ?????

Kama hawa wazeee tu wanayanyasana na wazeee wao wa EAC ya zamani mpaka leo hawajaripwa haki yao nanimepata habari muda mchache kama 20min ago waeziba baadhi ya barabara za DAR iwe sie vijana kama hatujauungana basi inakula kwetu kama hao wazee waa EAC

Jana Ridhwani Kikwete na Malisa hawa ni vijana wa CCM Taifa walikuwa arusha.. ila nadhani wamejionea wenyewe CCM chali hapa.....

kuhusu kuiba hawawezi zamu hii kwani hata watendaji wengi wa Halmashauri ya manispaa nao wemechoshwa na hali ya uchumi....

Wache Makamba aje na Mkapa then tutawaumbua mbaya....
 
ccm hawajajifunza tu walienda kilimanjaro - moshi mjini na kundi lao la ze komedy watu wakajaa kuangala ze komedy waliposhuka jukwaani alipopanda jk watua wakatawanyika wote wakabakia wale wenye kungojea usafiri na posho, wakajisifu wamekusanya watu wengi wakati kiu ya wakazi wa moshi ilikuwa kuona ze komedi live sio kusikiliza sera za ccm

watu wa moshi hawadanganyiki tena wakisikia ccm wanapiga ukunga mbaya kabisa
 
Bora hata wangempeleka Kinana!!!!!!!!!!!!!!!! Makamba!!! Wamechemka mbaya!!!!
 
"PakaJimmy;
Nimeamini hivyo kwa kuwa asilimia 70 ya wafanyabiashara hawa ni wachaga, na wana uelewa wa juu sana na siasa za Arusha..Ukikaa nao wanaongea kwa uchungu sana jinsi walivyochoka na chama hiki kikongwe, na wanasema safari hii hawafanyi kosa. Wanasema Lema wa CHADEMA ammekuja kuwakomboa!"

Fafanua!
 
Hakuna chochote ambacho Makamba anaweza kunusuru huko Arusha. Kama wameshindwa kunusuru Bukombe na wilaya zingine nchini, nini kinamwaminisha kuwa ataweza kubadilisha kwenye hilo jiji la Arusha.

Yeye aendelee kuvuta Night Allowance yake, asubiri neema ya mwenyekiti wake kama atambakiza kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa chama chake.
 
Bora hata wangempeleka Kinana!!!!!!!!!!!!!!!! Makamba!!! Wamechemka mbaya!!!!

Nasikia hata kinana alikwenda mwanzoni mwa kampeni akachemka mbaya huko Arusha nadhani watu wameisha choka na blaaa blaaa sana watu wana taka Action na sio maneno ya ahadi zisizo kuwa na kichwa wala miguu.

Mwl.Nyerere 1995 Kilimanjaro Hotel aliwambia kuwa viongozi wa CCM wanapaswa kujifunza jinsi ya kujua kukiongoza chama esp katka nyakati hizi za vyama vingi, yaani wajue jinsi ya kuongoza nchi katika mfumo wa vyama vingi sasa wao wakabweteka kabisaaa.

Na jana Mwinyi akarudia tena kusema Tusipo fuata yale aliyoyaseama baba wa Taifa Mwl. Nyerere basi mjue tunapotea kabisaaaa, Pia hapo zamani nadhani mwanzoni mwa mwaka huu Mwinyi nae alikubali kuwa Azimio La Arusha lilikuwa halina tatizo.

Nadhani lilikuwa linahitaji mabadiliko machache yanayoendana na wakati tuuuu,

Back
Top Bottom