Wanataka nini CCM? Najua wananchi hupiga kura kumpata mtu atakayewawakilisha vyema ndani ya nyumba ya waheshimiwa kule Dodoma, sasa sijaona mapungufu ya Dr. Slaa ambayo yaweza kuwafanya wananchi wake wakese imani naye. Hakika yeye bado ni Heavyweight Politician katika Tanzania. Hata kama angepelekwa nje ya jimbo lake, bado angetikisa tu na kuibuka mshindi. Hivyo, CCM kwa sababu ni chama cha Siasa waachwe wafanya wanachofanya maana mtu kama mimi naamini hiyo ni mojawapo ya demokrasia. Lakini wasitumia njia chafu yeyote katika ujaguzi ujao. Mungu ambariki Dr. Slaa kwa niaba ya watanzania wote na wanakaratu.
Ameni!!