Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah! mwenye vitabu hivi;
TUTARUDI NA ROHO ZETU
na LAZIME UFE JORAMU,
anipm tufanye biashara au nielekeze vinapopatikana.
Diana Kiboko ndiyo star wa novel hii kama sikosei
Utata wa 9/12 uwakute kina Jadu Mfaume! !Kwa sasa majeshi nimehamishia kwa Hussein Tuwa, Mdunguaji na Mkimbizi ni noma sana
Nadhani bado nakumbuka kidogo............
Kufa na Kupona-Wizi wa Karatasi za Siri
Njama-Harakati za Ukombozi Kusini mwa Afrika
Kikosi Cha Kisasi-Mtanange ulikuwa pale DRC Kongo
Kikomo-Wizi wa Almas Mwadui
Hujuma-
I stand to be corrected......Hivi Mkuu wapi ntapati vitabu hivi?
Dar-Es-Salaam usiku kitabu hiki kilitungwa na nani
Halafu kulikuwa na kile kitabu kinamhusu panga la shaba, sikumbuki vizuri but panga la shaba alikuwa mganga dada mmoja akaenda kutibiwa akaishia kuwa mke wa panga la shaba na urembo wake. mtunzi wake ni nani jamani
Kama Kumbukumbu yangu ni sahihi Simu ya Kifo ni kitabu cha zamani zaidi na kiliandikwa na Hassan Hussein Katalambula kama sikosei na si Hammie Rajab.
Kilitungwa na BEN R.MTOBWA kitabu chake cha mwisho ni MALAIKA WA SHETANI.
vitabu vyake bado vipo madukani, mfano nyuma ya pazia..roho ya paka,zawadi yaushindi,mpishi mwenye kibiongo..mwalimu mwenye mikono ya bandia...mwalimu mwenye miwani myeusi n.k
Nimefurahi kwa hili sana, ajabu nilibahatika kusoma kimoja tu cha Joram Kiango roho ya paka, na sijabahatika tena kupata vitabu vyake, mwenye uelewa wapi nitavipata kwa hapa Dar anielekeze
Mkuu naweza kupata wapi hiki kitabu? Hivi ni "Mikononi mwa Nunda au Nunda Mla watu? Nakumbuka pia nilisoma nikiwa darasa la 5joram mikononi mwa nunda
kiukweli vitabu hivyo nilivisoma nikiwa STD 5-7 na nikiwa O-level. haviwekeki chini. nikikumbuka vitabu hivyo, natamani kurudisha muda nyuma
watunzi waliotangulia mbele za haki wapumzike kwa amani!
Ulikuwa unajisikiaje unapomuona mwenzako ameshika KUFA NA KUPONA, NJAMA, KIKOSI CHA KISASI, KIKOMO ama SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU?, LAZIMA UFE JORAM, MIKONONI MWA NUNDA, NAJISIKIA KUUA TENA!!!HEBU KUMBUKA ULIPOKUWA UNASUBURI ZAMU YAKO NA WEWE UAZIME!!!
Nimeshangazwa kujua kwamba karibia kila mwandishi bora wa nyakati hizi amefariki. Nataka tuwakumbuke na kuwaombea. Lakini ni lazima nimpongeze mwandishi bora wa nyakati hizi HUSSEIN TUWA. kwa kweli ni mkali sana hebu kwa wale wapenzi wa riwaya tutafute riwaya zake MKIMBIZI, UTATA WA 9/12 NA MDUNGUAJU