Joram Kihango vs Willy Gamba

Mkuu naweza kupata wapi hiki kitabu? Hivi ni "Mikononi mwa Nunda au Nunda Mla watu? Nakumbuka pia nilisoma nikiwa darasa la 5

kuna Nunda Mla Watu, (masimulizi ktk maandishi) na Mikononi mwa Nunda(Riwaya ya Joramu Kiango)

kwa bahati mbaya sina copy kwa sasa ila ukienda kwenye serious bookshops utakipata
 
Dah!!! Sikumbuki hata nilikua navipata wapi hivyo vitabu...
 
Mpaka kufikia darasa la tano nilikua nishasoma vitabu vyote vya E. Musiba (Willy Gamba),Ben R. Mtobwa (Joram Kiango), Mashimo ya mfalme Suleiman na Kile kingine cha Allan Quarterman alimo Umsolopagazi na vingine vingi.
Nimeanza mpango wa kuvikusanya na sasa nimefanikiwa kuvipata vya Allan Quarterman na Ben Mtobwa, Alfu lela ulela, vitabu vya watunzi wa Kizanzibari, pamoja na vingine vingi.

Kuna mtu anamkumbuka mpelelezi Ray Sibanda katika "Kamlete akibisha mlipue"mtunzi nimemsahau
 
Jamani naweza kuvipata wapi hivyo vitabu?

Mungu awarehemu waandishi wake imenikumbusha kijijini kwetu.
 
Ndugu zangu ukweli roho inaniuma sana mpaka mchoz unatoka nakumbuka mbali sana hasa kipindi hicho ulikuwa ni ufahali kusoma hadithi za E.msiba.jaman ndugu zangu vp naweza kuviptativa wapi hivyo vitabu ni cheki watsapp au telegram 0755 33 76 82.i miss that books
 

Mkuu Hikma katika 'Kamlete Akibisha Mlipue' adui kubwa alijilipua mwenyewe akiwa amejifungia vile?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Sangomwile naomba nikiri kuwa kumbukumbu zangu zinagoma kunipa ushirikiano wa kutosha.
Lakini nadhani hauko mbali na ukweli, adui mkuu katika hii hadithi aliona heri ajiue kuliko kukubali kurudishwa nyumbani Tanzania kuja kuikabili fedheha kwa usaliti wake.
Mkuu Hikma katika 'Kamlete Akibisha Mlipue' adui kubwa alijilipua mwenyewe akiwa amejifungia vile?
 
Last edited by a moderator:

Duu! Umenikumbusha mbali mno. Ben R.Mtobwa, A.E.Musiba.
 

nakumbuka mwaka 96 nikiwa katoto nikawa naviiba nasoma maana mama hakutaka nisome
 
Dah mmenikumbusha mbali Kweli!!
Nimesoma karibia vitabu vya magwiji wote mliowataja ila Mmemsahau Jackson Eric Kalindimya naye alikuwa moto Katika utunzi.
Baadhi ya kzi zake ni Wimbi la huzuni, Mtafutano etc
 
Namkumbuka pia Azim Bawji katika Usiku wa balaa
 

unanikumbusha Hadithi zz Allan Quotaman, Mtu aliyebisha hodi usiku
 
safi sana maana watu wanasoma vitabu na hawaelewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…