Ulikuwa unajisikiaje unapomuona mwenzako ameshika KUFA NA KUPONA, NJAMA, KIKOSI CHA KISASI, KIKOMO ama SALAMU TOKA KUZIMU, TUTARUDI NA ROHO ZETU?, LAZIMA UFE JORAM, MIKONONI MWA NUNDA, NAJISIKIA KUUA TENA!!!HEBU KUMBUKA ULIPOKUWA UNASUBURI ZAMU YAKO NA WEWE UAZIME!!!
Nimeshangazwa kujua kwamba karibia kila mwandishi bora wa nyakati hizi amefariki. Nataka tuwakumbuke na kuwaombea. Lakini ni lazima nimpongeze mwandishi bora wa nyakati hizi HUSSEIN TUWA. kwa kweli ni mkali sana hebu kwa wale wapenzi wa riwaya tutafute riwaya zake MKIMBIZI, UTATA WA 9/12 NA MDUNGUAJU