Jose Mourinho afutwa kazi Chelsea

Jose Mourinho afutwa kazi Chelsea

Mou ninamkubali sana nitakuwa nae popote atakapo kwenda ila chese nooooo
 
Acha kumfananisha Mourinho na Wenger unajishushia heshima,
Mafanikio ya Mourinho Wenger ataendelea kuyaota ndotoni tu,

Tuchukulie UCL tu, Mourinho amechukua mara 2 akiwa na team za Porto na Chelsea,wenger Kombe la UCL atalisikia tu mpaka anastaafu,kwanza asubiri mziki wa Barcelona

msome wenger vizuri,wenger ni mwanamapinduzi,mjenzi wa mpira,fuatilia alivoubadili mpira wa uingereza,angependa makombe angeenda madrid walikokua wanamtaka usiku na mchana,tena wakat pale arsenal fedha hakuna
 
Nuksi zilianza na dokta Eva caneiro.

Timu ikavurugika kabisaaaaa.

Kwakweli sijafurahi kufukuzwa kwake but mustakabali wa timu ni muhimu zaidi .

Chelsea itabaki kuwa timu
Die hard fans will stick there forever may be we'll welcome him for third coming.

Hasta LA vista jose
 
40 milion pound
halafu Real Madrid wanamtaka...life is unfair

ndio maana wenzetu huwa wanaamua tu kusaidia mifuko ya hisani..asa kama hapo hayo mapesa yote huyo mournho atayafsnyia nini?
 
msome wenger vizuri,wenger ni mwanamapinduzi,mjenzi wa mpira,fuatilia alivoubadili mpira wa uingereza,angependa makombe angeenda madrid walikokua wanamtaka usiku na mchana,tena wakat pale arsenal fedha hakuna

Hivi wewe ni shabiki wa soka kweli au unevamia jukwaa tuu?

Kuna kocha asiyetaka makombe? Mafanikio ya kocha ni makombe,Kocha hukumbukwa kwa makombe na sio mbwembwe zozote,

Unajuaje kama angeenda Madrid angeshinda makombe?

Wewe sio mtu wa Soka rudi tu kwenye jukwaa lako la Mapenzi
 
Nuksi zilianza na dokta Eva caneiro.

Timu ikavurugika kabisaaaaa.

Kwakweli sijafurahi kufukuzwa kwake but mustakabali wa timu ni muhimu zaidi .

Chelsea itabaki kuwa timu
Die hard fans will stick there forever may be we'll welcome him for third coming.

Hasta LA vista jose

MOURINHO atabaki kwenye mioyo yetu sisi mashabiki wa ukweli wa Chelsea,kuna kundi limemuhujumu Mourinho makusudi kabisaaa!!
 
Mourinho huwa hamkejeli Wenger, anamwambiaga ukweli.

Unakumbuka aliwahi kumwambia kwamba kazi ya Wenger haina stress kwa sababu hawazi kufukuzwa hata kama matokeo ni mabaya.

Na Mou alisema ikitokea msimu ukaisha hajachukua kombe anafukuzwa au anaacha kazi, na ndicho kilichomtokea, wameona kwamba hatachukua kombe wakamfukuza. Wenger hata miaka kumi ipite no problem.

wenger hatakuja kufukuzwa na bodi labda mashabiki.maana anatengeneza profit ya ukweli
 
Hivi wewe ni shabiki wa soka kweli au unevamia jukwaa tuu?

Kuna kocha asiyetaka makombe? Mafanikio ya kocha ni makombe,Kocha hukumbukwa kwa makombe na sio mbwembwe zozote,

Unajuaje kama angeenda Madrid angeshinda makombe?

Wewe sio mtu wa Soka rudi tu kwenye jukwaa lako la Mapenzi

tunatofautiana kaka,wewe na mourinho mnaishi ili mule,wengera anakula ili aishi,baada ya arsenal kuhama highbury kwenda emirates,walijua kwa muongo mmoja hawatashindania mataji ..lakini wacheze ligi ya mabingwa,muda ulipofika na kumaliza kulipa deni wakaanza kununua wachezaji kwa bei kubwa,kwa haiba ya wenger,angeenda madrid,psg,bayern..alikotakiwa,angenunua wachezaji wazuri na mataji angepata tu
 
MOURINHO atabaki kwenye mioyo yetu sisi mashabiki wa ukweli wa Chelsea,kuna kundi limemuhujumu Mourinho makusudi kabisaaa!!

mourinho hana 'class'..anapiga domo hovyo kama konda,akifungwa analaumu wachezaj hadharani,ana 'ego' sana
 
Chelsea is there to stay whether in his presence or absence
 
kwangu ni heri chelsea tufungwe hata tushuke daraja kuliko kuondoka kwa Mou... imeniuma sana.... heri abaki...

aliichukua timu ikiwa ya kawaida sana akasaidia kuipandisha hadi pale ilifika... ikapata mashabiki kibao, ambao wengi wao tumekuwa wazalendo zaidi kwa Mourinho kuliko Chelsea halafu leo mnamfukuza??

Aliyenunua timu ndo kaifikisha hapo kwenye mafanikio.
 
Acha kumfananisha Mourinho na Wenger unajishushia heshima,
Mafanikio ya Mourinho Wenger ataendelea kuyaota ndotoni tu,

Tuchukulie UCL tu, Mourinho amechukua mara 2 akiwa na team za Porto na Chelsea,wenger Kombe la UCL atalisikia tu mpaka anastaafu,kwanza asubiri mziki wa Barcelona

Mourinho hajawahi kuchukua UCL na Chelsea bali na INTER na PORTO
 
tunatofautiana kaka,wewe na mourinho mnaishi ili mule,wengera anakula ili aishi,baada ya arsenal kuhama highbury kwenda emirates,walijua kwa muongo mmoja hawatashindania mataji ..lakini wacheze ligi ya mabingwa,muda ulipofika na kumaliza kulipa deni wakaanza kununua wachezaji kwa bei kubwa,kwa haiba ya wenger,angeenda madrid,psg,bayern..alikotakiwa,angenunua wachezaji wazuri na mataji angepata tu

Well said...!
 
attachment.php

Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.

Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Chelsea kwa kipindi cha pili, kilichoanza Juni 2013.

Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.

mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.

Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi.

Chanzo: BBC Swahili

TFF wamchangamkie aje fundisha timu yetu ya Taifa
 
Back
Top Bottom