Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
José Mourinho ameondoka katika nafasi yake ya ukocha wa klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki, baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Jumano, Agosti 27, 2025 Fenerbahçe walifungwa jumla ya 1-0 na Benfica katika mchuano wa mchujo wa Ligi ya Mabingwa, na hivyo kushindwa kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Mourinho alijiunga na Fenerbahçe mnamo Juni 2024, akitokea Roma ya Italia. Katika kipindi cha miezi 14 alichokuwa na klabu hiyo, aliiongoza kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Uturuki (Super Lig), lakini alishindwa kutwaa taji lolote.
Aliondolewa mapema katika michuano ya Kombe la Uturuki na Ligi ya Europa, na alikumbwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na faini ya £35,000 baada ya kumshika kwa nguvu kocha wa Galatasaray, Okan Buruk, katika mchuano wa derby ya Istanbul mwezi Aprili 2025.