Aliporudi Chelsea baadae akapoteza dressing room na ile dressing room ilikuwa chini ya John Terry.
John Terry akapeleka kesi kwa Abramovich na Mourinho akafukuzwa na malipo yote juu.
Sssa yupo Man Utd anaishapoteza dressing room ambayo imegawanyika. Kuna wachezaji ambao wanasikiliza maelekezo yake na kuna wale wasokubali kufuata maelekezo na kocha ambae anawazodoazodoa.
Bado Mourinho ana nafasi ya kuwa Pep Guadiola ambae ana uwezo wa kumfundisha na kuwatawala (man management) mchezaji jinsi ya kucheza mpira na akafuata na mifano ni mtu kama na Fabian Dephi ambae ametokea kuwa mchezaji wa kawaida na kuwa mchezaji mahiri.
Maourinho anapaswa kutumia utawala wake kwa wachezaji kama jinsi mzee Alex Ferguson alivyoweza kuwadhibiti wachezaji matajiri kama Bavid Beckam na Cristiano Ronaldo.
David beckam aliwahi kukung'utwa na kiatu cha mpira alichirushiwa na mzee Ferguson alipomletea za kuleta na mambo yakaishia dressing room, ingawa baadae taarifa zilitoka nje.
Sasa Mourinho ana mchezaji kama Paul Pogba, Romelu Lukaku ambao ni wana fainali na nusu fainali za kombe la dunia halafu leo hii wanacheza kwasakwasa badala ya mpira!