- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona barua ya Mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizitaka. Hii ni baaada ya balozi hizo kuanza kuingilia masuala ya ndani ya nchi kufuatia sakata la kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA siku chache zilizopita.
Nimependa sana ujasiri huu, ni lazima hawa mabalozi waache kuingilia mambo yetu.
Nimependa sana ujasiri huu, ni lazima hawa mabalozi waache kuingilia mambo yetu.
- Tunachokijua
- Agosti 13, 2024, baadhi ya akaunti kwenye Mitandao ya kijamii zilianza kuchapisha barua inayodaiwa kuwa ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizikumbusha Balozi nchini kufuatilia kanuni za Kidiplomasia na kuheshimu masuala ya Ndani ya nchi. Barua hiyo imehifadhiwa hapa, hapa na hapa.
Pamoja na mambo mengine, barua hii inadokeza mambo matatu, Kutoingilia siasa za ndani ya nchi, kutokuegemea chama chochote cha siasa pamoja na kuheshimu sheria na kanuni za nchi mwenyeji na kuepuka kuingilia masuala yake ya ndani kama inavyobainishwa kwenye Kifungu cha 41 cha Mkataba wa Vienna.
"Kifungu cha 3 cha Mkataba wa Vienna kinasema majukumu ya msingi ya misheni ya kidiplomasia, ikiwa ni pamoja na kuwakilisha taifa linalotuma, kulinda maslahi na raia wake, kufanya mazungumzo na nchi mwenyeji, kubaini hali katika nchi mwenyeji, na kukuza mahusiano ya kirafiki. Ingawa majukumu haya ni muhimu, ni muhimu pia kwa misheni za kidiplomasia kuepuka aina yoyote ya kuingilia katika masuala ya kisiasa ya ndani ya Tanzania. Taasisi ya Mwalimu Nyerere inasisitiza kuwa upande wa kisiasa ni muhimu sana kwa kudumisha imani na heshima zinazounga mkono mahusiano ya kidiplomasia", imebainisha barua hiyo.
Ukweli upoje?
JamiiCheck ilipowasiliana na Mzee Butiku kwa njia ya simu, alipokea na kusikika akimkabidhi mtu kuzungumza, ambapo alijitambulisha kuwa Msaidizi wa Mzee Butiku, alipoulizwa kuhusu barua hiyo amesema:
“Mzee anamalizia kikao, kuhusu huyo barua sio ya Mzee Butiku, tumeiona ikisambazwa, mtasaidia sana kufikisha ujumbe huu kwenye jamiii, akimaliza kikao atakurudia yeye mwenyewe."
Dakika chache baadaye Mzee Butiku akapatikana kwenye simu akasema “Siijui hiyo barua, sijaiona na siwezi kuzungumzia kitu ambacho sikijui wala sijakiona.”
Barua hii imeibuka wakati sakata la Kukamatwa kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA likiendelea ambapo baadhi ya balozi nchini, ikiwemo Ubalozi wa Marekani wakitoa wito kwa Serikali, Vyama vyote vya siasa, Asasi za kiraia na Wananchi kudumisha na kuheshimu haki za kukusanyika, na kushirikiana ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakuwa huru, wa haki, wa amani, jumuishi, na wenye uwazi unaoakisi matarajio na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.