Hivi wanunge huwa wanatutumikiaje? Hawa watu wafutwe watendaji wa serkali wa umma wanatosha. Wachoongea bungeni sio mawazo yetu, hakuna mahali tunakaa nao na kupanga au kuwaambia watusemee nini, wanasema utashi wao tu.
Mkuu that is the best point of the day!!
kuna wabunge wapumbavu wamejaa bungeni wanaongea upumbavu tupu hadi unahama chanel kwa kuboreka halafu unajiuliza hayo wanayoongea hao maziro brein ndio mawazo ya wanaowawakilisha? jibu ni hapana!!
nakumbuka one day nilikuwa Moshi kuna mbunge akaitisha mkutano wa raia waende kumwambia akaseme nini bungeni nikasema huyu ndio mbunge wa ukweli!!alikuwa mwanamke wa viti maalum CCM simkumbuki jina!!
pale mjengoni pamegeuzwa jukwaa la mipasho kuropoka na kubwabwaja tu wabunge wanalitia aibu taifa kwa kuonesha jinsi walivyojaa ujinga wa kuongea upumbavu saa nzima wenzake wakipiga meza tu na kushangilia ujinga unaosemwa usio na tija yoyote kwa wapiga kura, siku moja nilikaa kuangalia bunge Waziri wa Fedha aliwashukuru dunia nzima walio hai marehemu na wafu walio mjengoni na nje, familia yake rafiki zake serikali upinzani wasanii wanamichezo mawaziri, wabunge, Rais kinamama wazee na watoto, waafrika na wazungu aliwashukuru kuku na ndege kwa masaa matatu hadi nikachoka kuangalia nikasema hili bunge gani sasa mbona shukrani haziishi!!ndo maana sisi ni maskini tuna rasilimali kuliko Kenya ila sisi ni makapuku daima!
ukifuatilia wanayosema wabunge bungeni unajiuliza wanayatoa wapi mawazo hayo manake hata hawatuwakilishi chochote wanaongea tu utumbo wao, mfano ni hawa wabunge wapumbavu wenye mada na njama za kuibaka katiba kumuongezea Mkulu muda hawa walikaa na mwananchi gani akawaambia huku mtaani tunataka wakaseme hilo? malofa wakubwa!
hii ni mada kuu kabisa iliyopaswa kujitegemea, yaani wananchi tujue wabunge husema maneno wanayowakilisha kina nani, ni mfumo gani unaotumika kwa wao kupata mawazo ya wananchi wanayotakiwa kuyawasilisha bungeni? ni mfumo gani unatumika kuwadhibiti kusema yale waliyotumwa na wananchi wao tu?
tufanye nini wabunge waseme tunayotaka mtaani na sio upumbavu wao wanaopigiana makofi?
je wananchi tunawezaje nasisi huku mtaani kulidhibiti bunge wakati wowote baada ya uchaguzi ili waache kuongea upumbavu unaoboa kila siku kwa kutumia kodi zetu?