Joseph Kibwetere and Ugandan Cult Mass Murder/Suicide

Joseph Kibwetere and Ugandan Cult Mass Murder/Suicide

Huyu jamaa si ndio alichoma[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91] wenzake
 
Vizur sana...,endelea kutupa kisa cha Kibweretere cuz huwa nasikia aliwachoma moto waumini wake!
 
Kibwetere wa hapa kwetu ni nani kwani... ?
 
IMG_20180807_125124_229.jpg


IMG_20180807_125151_440.jpg


WAFUASI WA KIBWETERE NA MAUAJI YA HALAIKI (Part One)

KULITOKEA mauaji ya kutisha ya halaiki katika mji wa Kanungu nchini Uganda, mauaji haya yanajulikana kama " kibwetere kanungu massacre" au " mauaji ya kibwetere" mwaka 2000 machi 17 itabaki kuwa siku mbaya daima kwa wakazi wa maeneo ya kanungu na maeneo karibu na hayo, Takribani watu 924 ( wapo waliodai ni 530) na zaidi , waliteketea kwa moto na kufa kifo cha kutisha mno.

Wake kwa waume pamoja na watoto waliacha simanzi kubwa kwa familia zao, waganda wenzao na kila aliyepata kusikia tukio hili, yalikuwa mauaji ya kutisha ya kusikitisha na kufikirisha.
Kulikuwa na harakati za kidini zilizoitwa Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God. Harakati hizi zilikuwa ndani ya kundi lililokuwa limejitenga toka Kanisa katoliki ,waanzilishi wa harakati hizi wanatajwa kuwa ni Credonia Mwerinde, na Joseph kibwetere kabla ya watu wengine kuungana nao.

Kabla ya hapo Credonia anayesemwa kuwa mwanamke aliyekuwa akijiuza na kuuza pombe aina ya "Banana" kabla ya kuanza kudai kuwa ana maono ya bikira maria na alipokea kundi la baba yake ,Paul kashaku ,ambaye ndiye hasa aliyejitenga na Kanisa katoliki na kuanzisha kundi lake miaka ya 60.
Baba yake alimtuma kueneza maono yao mnamo mwaka 1989, ndipo alipokutana na Joseph kibwetere wakaamua waungane na kuanzisha harahakati zao, akidai alionyeshwa na mungu amtafute mtu aitwaye kibwetere na kufanya nae kazi ya mungu ,na ndipo lipatikane kundi la movement for the Restoration of the ten commandments of God, ambalo lilikuwa likiamini vikali katika amri 10 za mungu na juu ya mwisho wa dunia .

Umoja wao ulipata nguvu zaidi pale Dominic Kataribabo padre mashuhuri aliyeheshimika ,mwenye kiwango cha elimu ya PhD toka chuo kimoja nchini marekani alipojiunga nao akifuatiwa na Paul Ikazire na baadhi ya mapadre na masista ambao walivutiwa na harakati hizo.
Walipata misaada zaidi na wafuasi wengi , Joseph kibwetere aliuza baadhi ya mali zake kama nyumba, gari na mashine ya kusaga . na mnamo miaka ya 90 mwanzoni tayari Kanisa lilikuwa na mashamba ya mananasi na ndizi huku waumini wakiishi kijamaa katika kambi zilizojengwa kwa pesa na mali ambazo waumini walitakiwa kuziwasilisha kwa viongozi mara tu baada ya kujiunga nao.

Mwerinde alikuwa akidai kupokea ujumbe toka kwa bikira maria kupitia simu iliyokuwa mafichoni kisha kuwaletea waumini ujumbe aliopokea.
Kundi lilikua zaidi ,walijenga nyumba kwaajili ya viongozi wao ,wakajinunulia mashamba na kujenga nyumba ya ibada na shule.
Mnamo mwaka 1992, kundi hili lilitakiwa kuondoka eneo la Rwashamaire kwa amri ya viongozi wa kijiji na ndiyo wakahamia rasmi wilaya ya kanungu ambako baba yake Mwerinde aliwagawia ardhi kubwa ya kutosha.
Mwaka 1994 shule na kundi hili lilifungiwa kwa tuhuma za kutokuwa na mazingira safi kwa usalama wa wanafunzi na waumini kutumia watoto katika shughuli zao na tuhuma mbaya zaidi ya utekaji watoto wadogo na kuwatumikisha.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza ,kundi hili lilifunguliwa na kuruhusiwa kuendelea na shughuli pasipo kuchunguzwa wala kuchukuliwa hatua zozote.
Kama tutakumbuka vyema ,mwishoni mwa miaka ya 90 ,kulikuwa na hekaheka ya ujio wa milenia mpya Y2K ,kwa kibwetere na waumini wake kulikuwa na imani kama hiyo kuwa mwaka 2000 ndiyo mwisho wa dunia .

Watu waliuza mali zao ,watu walikaa mkao wa kunyakuliwa kwenda mbinguni ,viongozi wao wakizidi kuwajaza imani kuwa mwaka 2000 ulikuwa mwisho wa dunia ,kuna walioacha kazi ,kuna waliosalimisha hati zao za nyumba na mashamba ,pesa za mauzo ya mifugo ,mishahara ya mwisho kama sadaka.
Watu walisisitizwa kutubu dhambi zao na kuwa tayari kuiona mbingu ,kulikuwa na sherehe ndefu kuelekea mwisho wa dunia na mwisho wa mwaka.
Januari 1,2000 ilipita bila tukio lolote la mwisho wa dunia.

Baadhi ya waumini walicharuka, sadaka Kanisani ilishuka ghafla ,wapo walioanza harakati za kudai fedha zao na mali zao walizokabidhi ,walichachamaa vibaya mno wakiwakaba kibwetere na Mwerinde .
Inasemekana uasi huo na hekaheka hizi ndizo zilizopelekea mauaji ya machi 17.
Baada ya kubanwa sana ,ghafla ilitangazwa kuwa wamepokea maono kuwa machi 17,2000 ndiyo mwisho wa dunia, kundi lilianza sherehe ya kukata na shoka waliyoiita karamu ya mwisho.

Walichinja ng'ombe dume watatu na kuagiza kreti 70 za vinywaji laini, watu waliserebuka hatari siku hiyo ,pasipo kujua nyuma ya pazia ,Siku ya tukio ,viongozi wa kundi hili walifika Kanisani kuabudu na kusifu . masaa kadhaa baada ya ibada kuanza ,ghafla majirani waliokuwa karibu na eneo la kuabudu walisikia mlipuko mkubwa sana ulioambatana na Milipuko midogo midogo isiyo na idadi . vilio vya uchungu na maumivu makali vilisikika wakati moto ukizidi kushika kasi huku madirisha na milango vikiwa vimefungwa kwa kugongewa misumari.

Watu waliteketea Vibaya sana ,Inasemekana viongozi wote wa kundi hili ,Joseph kibwetere, Joseph kasapurari ,john kamagara , Dominic Kataribabo na Credonia mwerinde walikufa katika tukio hili.
Miili ya watu ilikuwa imeungua Vibaya sana watoto wanaokadiriwa kufikia 78, walikufa katika tukio hili, miili na Mafuvu mengine yaligeuka kuwa majivu kabisa ,ikagundulika ,siku chache Zilizopita kabla ya tukio ,Dominic kataribabo alionekana mahali akinunua Lita 50 za sulphuric Acid ambazo zinasemekana kuwa ndizo zilizotumika katika mauaji.

Mashuhuda wanasema walisikia harufu Kali ya petroli hivyo yawezekana walidanganywa warundikane ndani ili wanyakuliwe mbinguni pamoja na kinyume chake wakafunguliwa hewa yenye sumu na kuzungushiwa petrol na moto kuwashwa .
Wapo wanaodai Pengine waliaminishwa kufa kwa moto kwa kujimiminia mafuta hayo na kuwasha moto kama safari ya kwenda mbinguni huku hewa yenye sumu ikiwa imeshafunguliwa ,maana madirisha na milango yote ilifungwa barabara kwa ndani kiasi kwamba hakuna aliyeweza kutoka wala kupona.

Kuna sherehe nyingine ilitangazwa kuwa ingefanyika tarehe 18 machi 2000, sherehe hii ilitangazwa ili kupoteza watu mawazo kwa kuwa kuna watu walianza kuhisi kitu kibaya kingeweza kutokea.

Inaendelea..............
 
Asante kwa uzi mzuri uliokumbsha kumbukumbu zangu. Nakumbuka milenia nilivyoipokea nikiwa na mpenzi wangu ambaye ni mke wangu sasa. Alitoroka kwao kuja kwangu ili milenia itukute sote. Tulikunywa soda baridi na Chakula kizuri geto. Ni kweli miezi ya MBELE BBC na dochvere iliripoti sana hii habari tukifuatilia kwenye TV chache za kwenye mabaa.
Tukio limesaidia serikali kuzifatilia kwa karibu madhehebu wa dini na kuyadhibiti.
 
Sasa unapoishia hapa...unafikiri ni lini tena ntaingia humu?
 
Hizi imani zna mambo, ndiyo maana bliblia inasema mciziamini kira roho, coz ziko roho zidanganyazo. roho za mashetani
 
Sasa unapoishia hapa...unafikiri ni lini tena ntaingia humu?
Hawa nao bwana wanatutesa!!kwa kisha kuonjesha utamu kidogo tu utasubili weeee!!!UTAMU UNAKUJA UNAKATA!!Kuna ile nyingine ya jamaa mwingine part 3 imegoma kabisa kuletwa wiki tatu sasa!!!
 
Back
Top Bottom