Joseph Kibwetere and Ugandan Cult Mass Murder/Suicide

Umenikumbusha mbali sana mkuu wangu ila inasemekana Kibwetere alitoroka na katika hili ilisemekana alikuwa amefanya ushirika na baadhi ya maofisa ya serikali ndio waliomtorosha
 
Daah huyu jamaa Kibwetere aliacha gumuzo kubwa sana aisee hizi dini ukizitumia vibaya ni siraha moja kubwa sana ya maangamizi
 
Hakuna kitu cha hatari kama imani, endapo umakini hautakuwepo.
 
Kaa m
Hakuna binadamu anaeweza kunishawishi niuze Mali yangu au nimpe pesa kwa kunishawishi au kutumia udhaifu wa imani yangu hata Mara moja
Kaa mbali na imani mkuu usiichezee kabisa kitu imani,, kuna mengi na mazito sana yanayoendelea kwenye madhehebu huwezi kuyasikia,, ni watu na imani zao,, na wafuasi wametia pamba masikioni,, amini tu katika ulichojaaliwa kuamini kupitia hicho utaishi salama,,
 
Bora wao walikufa kabisa lakini naamini leo hii kuna wafuasi wa watu fulani fulani walishakufa siku nyingi wamebakiza kuzikwa tu,, yaani imani imewafanya wamekua kama mazombi,,
 
Haitakuja kuwezekana labda kwa iman za giza,
 
Ni miaka 17 sasa tangu yalipotokea mauaji ya kutisha ya halaiki katika mji wa Kanungu, nchini Uganda. Mauaji haya yanajulikana kama ‘Kibwetere Kanungu Massacre’ au ‘Mauaji ya Kibwetere’

Mwaka 2000, Machi 17 itabaki kuwa siku mbaya daima kwa wakazi wa maeneo ya Kanungu na maeneo karibu na hayo. Takribani watu 924 (wapo wanaodai ni 530) na zaidi waliteketea kwa moto na kufa kifo cha kutisha mno.

Wake kwa waume pamoja na watoto waliacha simanzi kubwa kwa familia zao, waganda wenzao na kila aliyepata kulisikia tukio hili. Yalikuwa mauaji ya kutisha… ya kusikitisha na kufikirisha!

VILIANZIA WAPI HADI KULETA MAUAJI?

Kulikuwa na harakati za kidini zilizoitwa Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God. Harakati hizi zilikuwa ndani ya Kundi lililokuwa limejitenga toka Kanisa Katoliki. Waanzilishi wa harakati hizi wanatajwa kuwa ni Credonia Mwerinde na Joseph Kibwetere kabla ya watu wengine kuungana nao.

Kabla ya hapo Credonia anayesemwa kuwa mwanamke aliyekuwa akijiuza na kuuza pombe aina ya Banana kabla ya kuanza kudai kuwa na maono ya Bikira Maria, alipokea Kundi la baba yake, Paulo Kashaku, ambaye ndiye haswa aliyejitenga na kanisa katoliki na kuanziaha Kundi lake miaka ya 60.

Baba yake alimtuma kueneza maono yao mnamo mwaka 1989, ndipo alipokutana na Joseph Kibwetere, Mwalimu wa Shule ya Msingi kitaaluma na mtu wa imani.

Walipokutana Credonia alimshawishi Kibwetere waungane na kuanzisha harakati zao akidai alionyeshwa na Mungu amtafute mtu aitwaye Kibwetere na kufanya naye kazi ya Mungu, na ndipo likapatikana Kundi la Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God ambalo lilikuwa likiamini vikali katika Amri 10 za Mungu na juu ya mwisho wa dunia.

Umoja wao ulipata nguvu zaidi pale Dominic Kataribabo, Padre mashuhuri aliyeheshimika, mwenye kiwango cha elimu ya PhD toka chuo kimoja nchini Marekani alipojiunga nao akifuatiwa na Paul Ikazire na baadhi ya mapadre na masista ambao walivutiwa na harakati hizo.

Na ili kupata misaada zaidi na wafuasi wengi. Joseph Kibwetere aliuza baadhi ya mali zake kama nyumba, gari na mashine ya kusaga. Na mnamo miaka ya 90 mwanzoni tayari kanisa lilikuwa mashamba ya mananasi na ndizi huku waumini wakiishi kijamaa katika kambi zilizojengwa kwa pesa na mali ambazo waumini walitakiwa kuziwasilisha kwa viongozi mara tu baada ya kujiunga nao.

Mwerinde alikuwa akidai kupokea ujumbe toka kwa Bikira Maria kupitia simu iliyokuwa mafichoni kisha kuwaletea waumini ujumbe alioupokea. Kundi lilikuwa zaidi. Walijenga nyumba kwa ajili ya viongozi, wakajinunulia mashamba na kujenga nyumba ya ibada na shule.

Mnamo 1992 kundi hili lilitakiwa kuondoka eneo la Rwashamaire kwa amri wa viongozi wa kijiji. Na ndiyo wakahamia rasmi wilaya ya Kanungu ambako baba yake Mwerinde aliwagawia ardhi kubwa ya kutosha!

1994, Paul Ikazire aliachana nao na kuondoka na waumini karibia 70 lakini kufikia 1997 Kundi lilikuwa na waumini wengi mno.
1998, Shule na kundi hili lilifungiwa kwa tuhuma za kutokuwa na mazingira safi kwa usalama wa wanafunzi na waumini, kutumia watoto katika shughuli zao na tuhuma mbaya zaidi ya utekaji watoto wadogo na kuwatumikisha.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza, kundi lilifunguliwa na kuruhusiwa kuendelea na shughuli pasipo kuchunguzwa wala kuchukuliwa hatua zozote.

Kama utakumbuka vyema mwishoni mwa miaka ya 90 kulikuwa na hekaheka ya ujio wa milenia mpya. Kwa Kibwetere na waumini wake kulikuwa na imani kuwa Mwaka 2000 ndiyo mwisho wa dunia.

Watu waliuza mali zao, watu walikaa mkao wa kunyakuliwa kwenda mbinguni. Viongozi wao wakizidi kuwajaza imani kuwa mwaka 2000 ulikuwa mwisho wa dunia. Kuna walioacha kazi, kuna waliosalimisha hati za nyumba na mashamba, pesa za mauzo ya mifugo, mishahara ya mwisho kama sadaka.

Watu wasisitizwa kutubu dhambi zao na kuwa tayari kuiona mbingu. Kulikuwa na sherehe ndefu kuelekea mwisho wa mwaka na mwisho wa dunia.

1 Januari, 2000 ilipita pasipo tukio lolote!

Baadhi ya waumini walicharuka, sadaka ilishuka ghafla, wapo walioanza harakati za kudai fedha zao na mali zao walizokabidhi. Walichachamaa vibaya mno wakiwakaba Kibwetere na Mwerinde.
Inasemekana uasi huu na hekaheka hizi ndizo zilizopelekea mauaji ya Machi 17.

Kabla ya hapo waumini walikatazwa kuhoji chochote, kusahihisha chochote walichoona kina mapungufu, na kucharuka kwao kulimaanisha kuanza kujitambua na mengi yangefichuka.

MAUAJI YA HALAIKI….

Baada ya kubanwa sana, ghafla ilitangazwa kuwa wamepokea maono kuwa Machi 17, 2000 ndiyo mwisho wa dunia.
Kundi liliandaa sherehe ya kukata na shoka waliyoiita karamu ya mwisho.

Walichinja ng’ombe dume watatu na kuagiza kreti 70 za vinywaji laini. Watu waliserebuka pasipo kujua ya nyuma ya pazia.

Siku ya tukio, viongozi wa hili kundi walifika kanisani kuabudu na kusifu. Masaa kadhaa baada ya ibada kuanza, ghafla majirani waliokuwa karibu na eneo la kuabudu walisikia mlipuko mkubwa sana ulioambatana na milipuko midogo midogo isiyo na idadi. Vilio vya uchungu na maumivu makali vilisikika wakati moto ukizidi kushika kasi huku madirisha na milango vikiwa vimefungwa kwa kugongewa misumari.

Watu waliteketea vibaya mno, inasemekana viongozi wote wa kundi hili. Joseph Kibwetere, Joseph Kasapurari, John Kamagara, Dominic Kataribabo, na Credonia Mwerinde walikufa katika tukio hili.

Miili ya watu ilikuwa imeungua vibaya sana, watoto wanaokadiriwa kufikia 78 walikufa katika tukiom hili, Maskini pengine pasipo hata kujua imani ni nini, pasipo kuwa na uamuzi wa kukataa kuwa sehemu ya imani hii. Miili na mafuvu mengine yaligeuka kuwa majivu kabisa.

BAADA YA MAUAJI….

Ikagundulika, Siku chache zilizopita kabla ya tukio Dominic Kataribabo alionekana mahali akinunua lita 50 za Sulphuric Acid ambazo zinasemekana kuwa ndizo zilizotumika katika mauaji.

Mashuhuda wanasema walisikia harufu kali ya petroli hivyo yawezekana walidanganywa warundikane ndani ili wanyakuliwe pamoja na kinyume chake wakafunguliwa hewa yenye sumu na kuzungushiwa petrol na moto kuwashwa.

Wapo wanaodai pengine waliaminishwa kufa kwa moto kwa kujimiminia mafuta hayo na kuwasha moto kama safari ya kwenda mbinguni huku hewa yenye sumu ikiwa imeshafunguliwa. Maana madirisha na milango yote ilifungwa barabara kwa ndani kiasi kwamba hakuna aliyeweza kutoka wala kupona.

Kuna sherehe nyingine ilitangazwa kuwa ingefanyika tar. 18 Machi 2000. Sherehe hii ilitangazwa ili kupoteza watu mawazo kwa kuwa kuna watu walianza kuhisi kitu kibaya kingeweza kutokea.
 
Daaaaaah inasikitisha sana lakini ni kweli na kibwetere mwenyewe kweli alikubali kujichoma moto!! Apana sidhani kama hii ni kweli haiwezekani itakuwa hawa viongozi waliwafungia wafuasi wao kisha wao wakala kona
 
Ndugu wanajukwaa habari, kama kichwa cha habari kinavyojieleza naomba mwenye kujuwa habari za kibwetele maana nimekuwa nikisikia habari zake kwamba aliwachoma moto wa umini wake kanisani baada ya kuwadanganya juu ya uwepo wa mwisho wa Dunia je baada ya tukio hilo alikamatwa au alikimbilia wapi na sasa ivi yuko wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu hapa Kibwetere. Aliwakusanya wafuasi wake miaka ya 2000 baada ya kuwatabiria mwisho wa dunia. Akawaweka kanisani kisha akawachoma moto wakiwa ndani. Yeye akasepa na mali zao zote walizokusanya
Mauaji haya aliyofanya kibwetere,yanatisha.
 
Mauaji ya kutisha.
 
Mauaji ya kutisha na ya kuhuzunisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…