Serikali haiwezi kuingilia hata watu mia tano wakifa kwa sababu yenyewe ilishamkubali huyu babu tangu alipoanza kutoa huduma yake, kwa wao kukubali kushindwa sasa hivi ni aibu kubwa. Hata wananchi wenyewe wanaoenda huko kupewa hiyo dawa hawawezi kuacha kwenda hata wakiambiwa watu 1000 wamekufa, maana wao wanang'ang'ana na imani yao tu bila hata kifikiria.
Huna imani hiyo na huumwi ndo maana wasema hivyo. Acha watu wapone, kufa kupo tu
This is the thing, we are not critically thinking, sisi tunaona tu basi kwa sababu huyu mtu anatumia jina la Mungu basi ni mkweli na ndio maana watu hawajiulizi iweje Mungu huyuhuyu akubali watu wafe kisa wanasubiria kikombe. Kama Mungu anataka kumponya mtu hatakubali watu wasafiri kilometers zote hizo kupata dawa wakati anaweza kuwaponya popote walipo. Tunawaamini viongozi wa dini kama wao ndio Miungu wadogo na kila wanachotuambia lazima tukifate, kama vile wao ndio bora zaidi yetu mbele za Mungu.
hapo kwenye RED Ni matokeo ya dhambi mkuu, na kila mwanadamu atakufa hata kama atakuwa mtakatifu kiasi gani kwa hiyo watu kufia Loliondo ni kitu cha kawaida kwa sababu babu hazui kifo yeye anatoa tiba.
Nakubaliana na wewe kwenye suala moja, kwamba hata wagonjwa wote wakipona bado vifo vitakuwepo. Ila ngoja nikuulize swali moja Mzee Punch, mfano wewe unaumwa sana kwa muda mrefu sasa, na uko hoi hospitalini then unasikia kuna babu ametumwa na Mungu kutibu watu ambao wanaumwa magonjwa kama yako. Unataka kuniambia hautatoka hospitali na kwenda kuponywa na huyo babu wakati madaktari wameshakuambia kuwa una cancer na cancer haina dawa? Just think before you answer me please, utaendelea kubaki hospital huku unasikia watu wengine wamepona na possibility ya wewe kupona ni kubwa maana si binadamu anayekuponya ni Mungu mwenyewe?
...MWANZONI NILITAKA KUMFANANISHA BABU NA SHUJAA WA VITA YA MAJIMAJI! Kwamba risasi zinapigwa zinabadilika kuwa maji.... Labda watasema babu anasingiziwa.."walinukuliwa baadhi ya watu wakisema "babu alisema maiti zitupwe hazitaoza katika eneo lile" wengine wakanukuliwa wakisema "anaekwenda na hirizi au kumjaribu babu hatoki salama kijijini Samunge!"Sasa hii connection ya Kibwetere inaingiaje hapa? Watu kufa kwa ajali na magonjwa ni jambo la kawaida. Unategemea nini iwapo unamtoa mgonjwa mahututi hospitali na kumuweka kwenye foleni kwa wiki nzima bila tiba wala uangalizi wa daktari? Babu mwenyewe amekemea tabia hiyo. Hapa huna hoja ila unadhihirisha tu usivyo na imani na tiba ya Babu.
Mkuu hao ndio great thinkers!! tunaowategemea WABOMOE HOJA NZITO NA KUJENGA HOJA IMARA!Mimi ndio maana nawalaumu sana wana JF wengine maana si wastaarabu. Kmf. anayemtukana miss judith, mjinga, mara amechanganyikiwa! Hivi kweli, tukimpima thinking and reasoning capacity atamzidi Miss judith? Miss judith ametoa coments! Wewe jibu kwa hoja na sio matusi bwanaaa!! Try to be a great thinker. Great thinker hawezi kuongea ovyo kama huyu hata kama anampinga miss judith.
Nafikiria kupumzika JF licha ya hii forum kuitwa the home of Great Thinkers, lakini ukweli hao Great thinkers wa kweli humu hawazidi 50. maana kuna watu humu wako makundi matatu, 1. La kuishambulia Chadema 2. kulishambulia kanisa katoliki 3. kumshambulia babu baada ya makanisa yao kuwa na uhaba wa sadaka za waumini.
Haingii akilini kwa mtu makini eti mtu mmoja kwa wiki nzima anafunguwa thread za kumuandama babu! this can only happen in Tanzania.
haiingii akilini, magari yamepanga foleni kilometa 40 yakienda kwa mganga wa kienyeji loliondo. This has happened only in tanzania
Haiingii akilini, magari yamepanga foleni kilometa 40 yakienda kwa mganga wa kienyeji Loliondo. This has happened only in Tanzania
Uko sahihi kabisa mkuu, wala hatutofautiani kimtazamo. Ndio maana nimependekeza tujadili namna ya kuweka utaratibu wa kuwatibu waliozidiwa ili wasifie kwenye foleni.