Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite wa mahakama ya Hakimu Mkazi - Mbeya, amegoma kujitoa katika shauri linalo mkabili mbunge wa Mbeya mjini , na Katibu wa Kanda ya Nyanda za juu kusini, Emanuel Masonga. Kesi hiyo inayo simamiwa na mawakili wasomi Hekima Mwasipu na Boniface Mwabukusi imeleta mvutano mkali wa kisheria, jambo ambalo linatoa shaka kama Hakimu hana agenda binafsi na kesi hiyo.
Sugu alitoa sababu kuu Tatu za kumkataa Hakimu :-
1. Kuwanyima dhamana bila sababu za msingi.
2. Hakimu kuamua kupokea ushahidi wa kifaa kilicho rekodi sauti ya Sugu km kielelezo wakati aliye rekodi kifaa hicho siye aliye kiwakilisha mahakamani hapo. Jopo la mawakili walidai kifaa hicho hakija kidhi matakwa ya kisheria na muwasilisha ana maslai na kesi hiyo kwa kuwa ni Askari polisi anaye fanya kazi katika Ofisi ya upelelezi mkoa wa Mbeya (RCO) . Na ingefaa aliye rekodi ndiye awasilishe kifaa hicho na aleze alirekodi kwa maudhui gani.
3. Hakimu kukiri kesi, imekupa shida, Sugu alisema "Mi ni Mkristo sitaki upate shida naomba nikukatae ili aje hakimu mwingine aendeshe kesi kwa uhuru bila kupata shida na mazingira ya shinikizo lolote lile.
Pamoja na sababu zote hizo Hakimu amekataa kujitoa. Ila mawakili wa upande wa utetezi (Sugu) wakatumia busara ya kisheria wakaamua kujitoa.
Katika mazingira hayo kama wewe huelewi masuala ya sheria unaweza Shangaa na kupata shida na maamuzi hayo ya "learned Advocates "
Kama Hakimu akiendelea na kesi na Kuamua kumtia hatia Sugu na Katibu huyo. Mawakili watakataa rufaa mahakama kuu na watashinda kwa grounds/sababu kuu Tatu-:
1. Makosa yao kisheria yalikuwa yadhaminika, "bailable" ila Hakimu kwa utashi wake akagoma kuwampa watuhumiwa dhamana.
2. Kwa kuwa watuhumiwa walikuwa na mawakili ila kutokana na mwendeno wa kesi walio utilia shaka, wakaamua kujitoa. Na mahakama ikaamua kuendelea kusikiliza kesi husika, hukumu hiyo itakuwa batili kwa sababu mahakama imewamnyima haki ya uwakilishi watuhumiwa " trial magistrate denied appellant right to legal representation.
3. Kwa kuwa upande wa utetezi umeomba Hakimu ajitoe katika kesi kwa kutokuwa na imani nae" on the grounds of bias" na Hakimu kwa utashi wake akaamua kukataa, basi maamuzi au hukumu itakayo tolewa itakuwa batili pia. Kisheria mtuhumiwa ana haki ya kumkataa Hakimu. Sasa iweje huyu ang'ang'anie,?
Kuna kifungu kimoja cha sheria kinasema " where bias has been alleged, then unless there be very good reason, it's prudent for a judge or magistrate concerned to step down and not to insist on hearing the matter"
Kw tasfri isiyo rasmi," Ikiwa kuna tuhuma za ependeleo, , basi isipokuwa kuna sababu muhimu ni busara kwa hakimu anayehusika kuachana the hiyo kesi na si kusisitiza kutaka kuendelea nayo"
[HASHTAG]#Msigope[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Tutashinda[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForAll[/HASHTAG]..
Ndimi, Noel Shao
[HASHTAG]#mjenziWaTanzaniaMpya[/HASHTAG]