Joseph Mbilinyi 'Sugu', ni zaidi ya mfano bora wa kuigwa

Ndg.MWASALEMBA.

Senior Member
Joined
Dec 18, 2013
Posts
141
Reaction score
280
Salama!

Awali ya yote na declare interest kuwa hakika uyu Jamaa mimi binafsi namuona ni mfano bora. Ni bora hasa kwa kaya nyingi sana za kiTanzania,ambazo ni watafutaji wao sio waliokuta mali au mazingira bora tayari.

Maisha yake yanafaa kuigwa na kijana mtafutaji yeyote wa kiTanzania mwenye kuhisi unyonge, kutengwa, kutoweza kufanya jambo na yeyote anaetoka katika familia isiyo na ukwasi wa mali!

Nakusihi, pamoja na mapungufu yake jamaa ni real mfano, na wewe unaweza. ..hapa nazungumzia na nawahasa wale tusio na wajomba wa kutushika mkono ili tupete kwenye fursa au dili flani. ..you can make it on your own.


Lolote linawezekana, kuwa binadam ni sababu tosha wewe kufikia malengo yako, unaweza...
Hata kama ni mvivu wa kusoma vitabu vya kiada, basi nenda kwa hiki cha ziada cha SUGU; Maisha na Muziki, naamini hautatoka kapa...maisha ni haya haya, wewe ndio muamuzi wa maisha yako.

Angalia hii attached video ya Sugu, ulikuwa mwaka 1996, leo ni 2015 yaani miaka 19 baadae, naamini kabisa huyu jamaa hakuandika mkakati wa maisha yake kwamba atapita hapa na pale, lakini naamini sana yeye aliinuka na kufanya Kile alichoamini ni sahihi. ..LIFE IS A LOOONG WAY TO GO, NEVER GIVE UP.

Jifunze kitu toka kwenye hiyo video attached.

Regards,

Mtafutaji..
 

Attachments

Sio vizuri kujadili watu binafsi lakini huyu jaamaa ni vizuri akajadiliwa kwa maana ni icon ya mabadiliko ya kijamii na kifikra kwa nchi isiyo na mwelekeo kama yetu.
Hebu angalia mchango weke katika bunge na alivyoweza kuleta picha tofauti na halisi ya uendeshwaji wa bunge letu. Watu wenye upeo kama wa ki.bon.de wataishia kumdharau lakini hii ni alama ya mafanikio na mabadiliko Tanzania.
 
sugu ni kijana mtafutaji sana.

toka enzi na enzi halafu sio muoga wa maisha.

1993 yuko boarder anaelekea south africa kusaka maisha..

hata usa ameenda mwenyewe kutafuta maisha.. anatoka familia duni.. lakini kachakalika na kufanya mavurugu kama amezaliwa ushuani vile..
 
Mimi pia najifunza kutoka kwako kuwa siyo lazima kuimba tu lakini kuuza mafanikio ya wenzako ni mwendo pia hivyo bwana Mwasalemba kupitia namna ulivyotokelezea kwa hoja naweza pia fanikiwa!!! bila kujali lala nje na kuacha mlango wazi.
 
miaka 19 since ameimba mambo ni yaleyale kweli tupu.Huyu jamaa may be ni ka nabii fulani ila hana promo awe rais,au anatosha kuwa rais wa hapa kwetu mby
 
...maisha,maana yake ni ioio maisha(vile uishivyo),izi tafsiri nyingine kuu kuu za kimadaftari zaidi,grrrr sometime,tuinuke ndugu zangu...we better die empty,otherwise we ask for forgiveness BUT only if you were on trying,lakini kama haukuwa katika harakati za kutafuta na umefariki,mimi nakuona wewe ndio ulikuwa shida,sio maisha!

FANYA LOLOTE LILILO SAHIHI,hatua za mbele zitajipa along the way,binafsi nina daftari ya kunukuu niliokwisha yafanya,SIO nitakayo yafanya...yananipa njia,ujazo na nashiba mambo meengi kichwani ultimately next step inajishepu,kisomi ningeiita to do list.
 
Pumbafu zake tu, shauri yao hao wana Mbeya waliochagua mvuta bangi. Na hivyo ndivyo walivyo
 
Pumbafu zake tu, shauri yao hao wana Mbeya waliochagua mvuta bangi. Na hivyo ndivyo walivyo
sina neno lakukufananisha nalo,lakini ningekuwa mimi ni wewe nisinge,KATU nisinge andika ulichoandika! ubunge any time akiamua anaweza akauacha,lakini katu huwezi wala yeye mwenyewe hawezi tena kufuta historia,ameshaandika kwa...endelea ivyoivyo utakuja wahadithia wajukuu zako,naamini kuna siku utajilaumu.
 

Nyerere ni binafsi kiasi gani? usijichanfanye. we jadili kwa kusingizia kujiepusha kujadili watu
 
sugu moto chini...!!!

Huyu jamaa ana akili.Full stop

Ni mfano wa kuigwa...tukiwa kama vijana tuna chakujifunza toka kwake...
Natamani io video isiwe kama attachment iwe open kuiplay tu,naamini itatoa funzo kwa haraka zaidi,na pia kwa watumiaji wa simu zenye changamoto itamrahisishia pia kuiangalia.
 
sugu bwana namba nyingine kwanza sio muoga ht kidogo
 
Yani ukitaka ukose amani na raha mchokoze huyu jamaa.Ana mdogo wake ana akili HATARI!!!! kasoma sayansi na wazungu huwa wanadata kwa utendaji wake.
 
Kimsingi jamaa yupo vizuri, lakini mimi binafsi naamini sana katika exposure ya mambo,hii ni silaha ya mafanikio.Kama Mungu kakujalia kalama nyingine hewalaaa, lakini kalama kubwa zaidi ni hamu yakujifunza mambo mengi zaidi na kuyadaka yenye tija hii ni muhimu zaidi.

Hivyo tukiwa kama vijana naona tuwe fasta sana katika kutafuta taarifa na kuzitumia zile zenye tija, inaweza kuwa ni ndani nchini kwetu au toka kwa majirani zetu na hata toka ng'ambo. Taarifa ya jambo ndio wigo wa mafanikio....usibweteke.

i. e kuna usemi mmoja wa kizungu naupendaga sana! Kwa manufaa ya wengi naomba niuweke kwa kishwahili.

Una AMKA alfajiri na mapema, unashukuru Muumba umeamka salama, unajiandaa vema yani kama mswaki unapiga, kama kuoga unaoga, kisha baada ya muda upo barabarani unawahi eneo lako la ajira, yani sehemu uliyoajiriwa au kwa lugha nyingine sehemu ambayo unamsaidia mtu ( mmiliki wa io ofisi ) kutimiza ndoto na malengo yake, wewe ukiwa na furaha kabisa na amani moyoni unaita io ni fulsa. INASIKITISHA SANA!

NB :TENA NA TENA NAOMBA ANGALIA IO VIDEO YA SUGU,NI MWAKA 1996 io, leo hii tunabeza hatua aliyoifikia tunaona kama ni bahati mbaya, take time kufikiri vema, maisha ndio yapo hivyo. ..sio bahati mbaya,wala ajafika alipofikia kwa msaada wa kutumia ubini au kutumia mkono wa mjomba, mbio zimemsaidia na alikuwa na bado ni mwepesi kupokea vijiti vya wachovu katika mbio.

Hii ni zamu yako sasa, anzia apo si lazima wote tuwe wabunge, sio lazima wote tuimbe, sio lazima wote tulime. ..na mengine meeengi, ila ni lazima sote tuongeze exposure ya mambo kupitia umoumo njia ITAJITENGENEZA. ...
 
Sugu namkubali sana aisee,,jamaa mtafutaji balaa.
 

sawa sawia Mkuu
 
Last edited by a moderator:
Sugu ni moja kati ya vijana wa kipekee kabisa kuwai kutokea hapa bongo. Ni mtu ambaye kwake hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana.

Ukikaa kumsikiliza huyu mshikaji lazima udouble hustle zako, kuna watu wanamchukulia mibange ila mshikaji yupo smart ile mbaya ni vile hataki kupoteza identity yake ya street.

Tokea kuwa mlinzi wa getini mpaka kuwa icon wa muziki mpaka kuingia bungeni akiibadilisha mtazamo wa watu kuhusu nani anastahili kuingia bungeni. Kuna Phd holders wanatamani wafike hapo ila zitaishia kuwa ndoto na bado jamaa atazidi kuwashangaza watu 2020.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…