Joseph Mbilinyi 'Sugu', ni zaidi ya mfano bora wa kuigwa


Nadhani hii ni safiii sana boss kazi. ..kubwa nadhani jamaa ana focus sana katika Kile anacho hitaji kupata,hii dhana vijana wengi tujifunze pia, tusiwe watu wakuishia njiani katika mpango flani unaokuwa unahitaji kufikia...Unaweza! Kimsingi binafsi naona safari yake ni ndefu na ana nafasi kubwa zaidi yakutushangaza nakutuacha midomo wazi. ..

Hii naweza pia kufananisha na jambo hili. ..hasa apa Tanzania, tasnia ya 'MAGAZETI' bado inakumbana saaana na changamoto katika swala la mauzo ya machapisho yao ya kila siku. Mauzo ni chini sana Kiasi uendeshaji wa media houses nyingi zinategemea matangazo na vyanzo vingine zaidi kuliko pesa ya mauzo ya gazeti lenyewe, sasa nataka sema nini?

Magazeti tunayagawa katika makundi matatu:

1.magazeti ya kuhabarisha habari wanazo ziita habari serious i. e mwananchi,rai, n.k
2.magazeti ya kuhabarisha habari wanazo ziita habari za michezo i. e dimba, mwanasport n.k
3 . magazeti ya kuhabarisha habari wanazo ziita habari za udaku i. e ijumaa,uwazi n.k

Haya magazeti ambayo yanaonekana hayajaenda shule na hayapo serious yani udaku na michezo ndio yanafanya vizuuuuri zaidi kimauzo kiasi kwamba magazeti meengi sana ya ayo ya serious news hayafiki ata nusu ya mauzo yao.

So kuna watu wanaweza kujiona wao ni maprofesa, madegree holders n.k siwezi walinganisha na SUGU, kimsingi maisha ni wewe. ..bado nazidi kupata sababu yakuona huyu jamaa kuna mshangao zaidi anaweza kuufanya, na wewe pia kama ukiamua simama kisha fanya kilicho sahihi unaweza. ..
 

points tupuu
 

Nimeipenda hii video, safi sana ni kumbukumbu nzuri sana.
 
Katika group letu moja la whatsapp kuna mdau kapost hii makitu:kama inaukweli hivi...sema nayo;

Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana
elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka
makubwa ni wale wa "darasa la saba B", ama ambao hawakuingia kabisa darasani.

Wasomi wengi wana maisha ya kawaida[yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi na magari ya kutembelea baaasi tena kwa mikopo!]. Na tena wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini[kistaarabu tunaita wana
maisha ya kuungaunga].

Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana. Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga. Mosi; [wameelezwa na kuaminishwa kwamba] yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli.

Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na
kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa
sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huamua kufa kimasikini wakitegemea
mishahara pekee[kwa sababu ndio ina uhakika].

Pili; madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Utaniuliza nimejuaje? Jibu lipo! Angalia namna mitihani inavyofanyika; ni sheria kwamba kila mwanafunzi afanye mtihani
peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha
mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida(hasa ya
kusaka fedha), unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja,
wafanyakazi n.k.

Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani! Simaanishi kusoma hakuna maana[hata mimi nimesoma nina digrii na vyeti vya kozi za kumwaga] isipokuwa ninakwambia hivi: Kama ukipata nafasi ya
kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku
mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia hayo
makaratasi wanayokuzawadia yaitwayo vyeti.

Ukitaka kutajirika usiulete "u-smart" wa darasani huku mtaani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…