Ndg.MWASALEMBA.
Senior Member
- Dec 18, 2013
- 141
- 280
- Thread starter
- #21
Sugu ni moja kati ya vijana wa kipekee kabisa kuwai kutokea hapa bongo. Ni mtu ambaye kwake hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana.
Ukikaa kumsikiliza huyu mshikaji lazima udouble hustle zako, kuna watu wanamchukulia mibange ila mshikaji yupo smart ile mbaya ni vile hataki kupoteza identity yake ya street.
Tokea kuwa mlinzi wa getini mpaka kuwa icon wa muziki mpaka kuingia bungeni akiibadilisha mtazamo wa watu kuhusu nani anastahili kuingia bungeni. Kuna Phd holders wanatamani wafike hapo ila zitaishia kuwa ndoto na bado jamaa atazidi kuwashangaza watu 2020.
Nadhani hii ni safiii sana boss kazi. ..kubwa nadhani jamaa ana focus sana katika Kile anacho hitaji kupata,hii dhana vijana wengi tujifunze pia, tusiwe watu wakuishia njiani katika mpango flani unaokuwa unahitaji kufikia...Unaweza! Kimsingi binafsi naona safari yake ni ndefu na ana nafasi kubwa zaidi yakutushangaza nakutuacha midomo wazi. ..
Hii naweza pia kufananisha na jambo hili. ..hasa apa Tanzania, tasnia ya 'MAGAZETI' bado inakumbana saaana na changamoto katika swala la mauzo ya machapisho yao ya kila siku. Mauzo ni chini sana Kiasi uendeshaji wa media houses nyingi zinategemea matangazo na vyanzo vingine zaidi kuliko pesa ya mauzo ya gazeti lenyewe, sasa nataka sema nini?
Magazeti tunayagawa katika makundi matatu:
1.magazeti ya kuhabarisha habari wanazo ziita habari serious i. e mwananchi,rai, n.k
2.magazeti ya kuhabarisha habari wanazo ziita habari za michezo i. e dimba, mwanasport n.k
3 . magazeti ya kuhabarisha habari wanazo ziita habari za udaku i. e ijumaa,uwazi n.k
Haya magazeti ambayo yanaonekana hayajaenda shule na hayapo serious yani udaku na michezo ndio yanafanya vizuuuuri zaidi kimauzo kiasi kwamba magazeti meengi sana ya ayo ya serious news hayafiki ata nusu ya mauzo yao.
So kuna watu wanaweza kujiona wao ni maprofesa, madegree holders n.k siwezi walinganisha na SUGU, kimsingi maisha ni wewe. ..bado nazidi kupata sababu yakuona huyu jamaa kuna mshangao zaidi anaweza kuufanya, na wewe pia kama ukiamua simama kisha fanya kilicho sahihi unaweza. ..