PreGE2025 Joseph Mussa Mahindoni achaguliwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA Dodoma

PreGE2025 Joseph Mussa Mahindoni achaguliwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA Dodoma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wajumbe wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Cchadema (BAVICHA) Mkoa wa Dodoma, leo tarehe 7 Aprili 2025, wamemchagua Joseph Mussa Mahindoni kuwa Mwenyekiti mpya wa baraza hilo katika uchaguzi uliofanyika katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kati.

Soma Pia: Shangwe la CHADEMA Arusha wakifurahia ushindi wa Deogratius Mahinyila kama Mwenyekiti MPYA wa BAVICHA Taifa

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika Ofisi za Chadema Kanda ya Kati zilizopo Jijini Dodoma wajumbe 19 walioshiriki wamempigia kura za ndiyo, hatua iliyompa ushindi wa asilimia mia moja Mahindoni.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Nafasi hiyo awali ilikuwa ikishikiliwa na Wakili Deogratius Mahinyila, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Taifa.
 
Wapiga kura 19 wanamchagua Kiongozi wa Mkoa? Ahahahahaha!!

Yaani nimecheka kidogo nimwage Konyagi yangu! Ahahahahaha!!!
 
Back
Top Bottom