Hivi ni kwanini watu wa vyama vya siasa hapa nchini mtu waliyetofautiana naye itikadi wanamuita msaliti?
Watu wengi wa vyama vya siasa ni washabiki wa demokrasia lakini sio waumini wa demokrasia.......kwao demokrasia ni kuwa na mawazo na fikra wanazozipenda wao.......maoni au utashi wako ukienda kinyume na nafsi zao.....ndio unaziona rangi zao halisi.
Harakati za kupambania demokrasia hapa nchini bado Zina safari ndefu sana kwa kuwa hata hao wanaojipambanua kuwa Wana harakati wa demokrasia ndio watu kwa kwanza kuivunja demokrasia.
Sote tunaona matusi yanayoporomoshwa humu na watu wanaojiita watu demokrasia dhidi ya mtu au watu walioamua kuwaza tofauti matamanio ya nafsi zao.
NB; Hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye kukomaa kidemokrasia ni kuimarisha kiwango chako Cha uvumilivu.