StaloS was a great leader who saved the world from falling in the hands of Hitler
He successful made Russia the most Powerful nation both militarily and economically
Hayo unaamini? Alikuwa dikteta aliyeua milioni ya wananchi wake. Urusi haukuwa na nguvu kushinda nchi nyingine. Ilikuwa na nguvu kubwa ya kijeshi kwa sababu aliwekeza kila kitu kwenye tasnia ya kijeshi, ilhali wananchi walikuwa maskini.
Mwanzo wa Vita Kuu ya Pili, jeshi lake lilipotea askari milioni kadhaa kwa sababu Stalin aliwahi kuua sehemu kubwa ya majenerali kabla ya vita. Wajerumani waliweza kufika kirahisi hadi kilomita chache mbele ya Moscow. Kama wasingekuwa wabaguzi wabaya walioona eti Mrusi ni nusu-binadamu tu, wengi sana wangewaunga mkono; pia mwenzake Stalin yaani yule Hitler alivuruga mipango ya kijeshi.
Kuwa na dikteta ambaye havumilii upinzani wowote na mawazo tofauti ni hakika ya kuanguka. Stalin alianguka sana kwenye mwanzo wa vita, hadi alikubali kusikia wengine. Hitler alianguka zaidi, kwa sababu hadi mwisho hakuwa tayari kusikiliza wengine.
Uchumi wa Stalin ulibaki nyuma ya nchi nyingine zilizoendelea. Magari yao yalikuwa kichekesho, baada ya mwisho wa ukomunisti viwanda viliporomoka haraka kwa sababu wananchi hawakutaka kununua tena bidhaa za Urusi, walipendelea kulipa bei za juu kwa bidhaa kutoka nje.
Miaka michache baada ya kifo cha Stalin, mfumo wake ulifikisha watu kwenye anga-nje, lakini kwa vifo kadhaa vilivyofichwa. Walishindwa kupeleka watu Mwezini, maana tekinolojia yao haikutosha.