Josephat Gwajima akana utajiri wake

Josephat Gwajima akana utajiri wake

Gwajima hajui kama imeigusa ngome ya Vatican, yenye mafia wakutosha dunia nzima, hapo wamemsamee tu, wangeweza kumpoteza kimyakimya. JK mwenyewe anajua hilo wala asimsingizie Rais wetu. Aombe msamaa kwa Muadhama Kadinali Polycap Pengo yaishe, aendelee kuchuna misukule yake aliyo ipumbaza na kujikuta inamuona kama mungu.
 
wewe ni Mkristo wa kubumba toka lini serikali itake kanisa kuonyesha waumini wake,mapato yake nk hili ni shabulio kwa UKRISTO ili tu kuudhofisha au kuuweka MFUKONI.
Mkuu mimi kama mkristo nachukia sana wizi, uongo na ulagghai, kama wa self made "askofu" Gwajima.
Sasa ninyi mnaoamini kuwa mko 70,000 ilhali mnajiona kwa macho kuwa hamzidi 5000, basi ni lazima mmepandikizwa mapepo.
 
Kwani Gwajima akibaki na waumini wake na nyiye mkibaki na dini yenu kuna ubaya gani....???
 
Asema, JK atoe tamko juu ya polisi wanaomwandama. Adai kama hajatoa tamko basi yeye ndio aliowatuma.

Aeleza siri ya utajiri wake, waumini wamchangia mamilioni papo hapo.

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuvikemea vyombo vya dola vinavyomfuatafuata vikihoji mambo binafsi na kwamba akishindwa kufanya hivyo itakuwa wazi kwamba yeye ndiye anawatuma.

Akihubiri mamia ya waumini wa kanisa hilo jana, Gwajima alisema amekuwa akifuatwafuatwa na vyombo vya Serikali utadhani yeye si raia wakati ni Mtanzania halisi.

“Rais Kikwete tafadhali namuomba awakemee watu hawa... asipowakemea, basi kanisa langu litajua kwamba yeye ndiye anayewatuma,” alisema Gwajima huku akishangiliwa na waumini waliokuwa wakimsikiliza.

Huku wakinyeshewa na mvua, waumini hao walikuwa wakimsikiliza Askofu Gwajima, siku tatu baada ya kiongozi huyo kuhojiwa kwa mara ya pili na polisi na kutakiwa awasilishe mambo 10 yanayohusiana na usajili wa kanisa, uongozi na mali zake.

Uraia wake

“Mimi ni Mtanzania halisi acheni nifanye kazi ya Mungu, kama mnadhani mimi si Mtanzania, basi mmepotoka kwani kwa hilo mtashindwa,” alisema.

Alisema makundi ya jamii yamekuwa yakitoa kauli mbalimbali lakini hayabughudhiwi anavyofanyiwa.

“Madaktari, wanasiasa, wafanyabiashara wamekuwa wakitoa misimamo yao lakini hawabughudhiwi iweje Gwajima tu? Nitaendelea kuwapa vidonge vyenu kila mtakapopotoka, nafanya kazi ya bwana,” alisema.

Kuhusu utajiri wake

Gwajima alisema amekuwa akishangazwa na vyombo vya Serikali vinavyohoji utajiri alionao bila kujua anaongoza idadi gani ya waumini. Alisema anaongoza kanisa lenye waumini zaidi ya 70,000 ambao ni kama watoto wake na kwamba yeye ni baba yao wa kiroho.

“Waumini hawa mimi ni baba yao wa kiroho, nikiwaomba kila mmoja anipe Sh1,000 tu nitakuwa na Sh70 milioni, halafu mnahoji utajiri ninaupata wapi?” alisema na kisha kuwauliza waumini hao... “Hivi baba yenu nikiwaomba kila mmoja anipe Sh1,000 mtanipa au mtaninyima?”

Alijibiwa, “Tutakupaaaa!” Baada ya majibu hayo waumini hao walianza kupeleka fedha katika jukwaa kuu huku wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu.

Waumini hao, wengi wao wakiwa wameshikilia noti za Sh10,000 na Sh5,000 walianza kusonga mbele na kutumbukiza kwenye maboksi.

Mchango huo ulichukua dakika 25 kuanzia saa 6.30 hadi saa 6.55 mchana na ulisimama pale Askofu Gwajima kuwaambia... “Basi basi naomba muache kuleta fedha, zinatosha, kaeni msikilize mahubiri, tukiendelea kupokea fedha hapa tutakesha. Watu wa idara ya fedha kusanyeni maboksi yenye fedha na pelekeni kunakohusika, hizi ni fedha za kanisa ambazo zitatumika katika mambo mbalimbali ikiwamo kununua mafuta ya kuendesha jenereta la kuzalisha umeme.”

Gwajima alisema kutokana na idadi ya waumini wake kama kila mmoja atampa Sh10,000 basi atakuwa na Sh700 milioni.

“Wakinipa Sh100,000 kila mmoja ina maana nitakuwa na Sh7 bilioni, nawashangaa wanaohoji kuwa huu ni utajiri, watu hawalali usingizi wanajiuliza Gwajima anapata wapi utajiri huu, nawaambia mimi siyo tajiri hizi ni fedha za kanisa,” alisema.

Idadi ya waumini

Askofu huyo alisema mbali na utajiri, watu wanahoji anapata wapi waumini wengi namna hiyo.

“Shida si kumkashifu Askofu Pengo, bali sasa wanahoji waumini wengi wanafuata nini hapa,” alisema na kuongeza,” nao wakija kunisikiliza watafahamu nini mnachokifuata kwani nao watabaki hapahapa hawatatoka.”

Alisema baada ya kuandamwa na vyombo vya Serikali, maaskofu walitaka kutoa tamko lakini aliwakataza kwa sababu aliona anafanyiwa hivyo kwa sababu binafsi. Alisema katika kipindi ambacho amekuwa akiandamwa na polisi, waumini wameongezeka kanisani kwake.

“Walokole wakiwa katika tabu, ndiyo kwanza wanashikamana, ukitaka kuwasambaratisha wape neema utafanikiwa. Wakipata nyumba nzuri, gari zuri, kazi nzuri na safari katika nchi mbalimbali wanaacha kuja kanisani lakini wakiwa katika matatizo wanashikamana, hamuwezi kuwasambaratisha,” alisema.

Ilivyokuwa awali

Gwajima amehojiwa mara mbili na polisi kutokana na matamshi yake ya kashfa dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, lakini mara ya pili mwelekeo wa mahojiano ulibadilika ukalenga zaidi kanisa na mali zake.

Mara ya kwanza kuhojiwa ilikuwa Machi 27, siku ambayo alizimia na kupelekwa katika Hospitali ya TMJ alikolazwa kwa siku nne huku taarifa zikieleza-

Baada ya kutoka Polisi, Gwajima amekuwa akitembea kwa kutumia kiti cha magurudumu mawili hadi Aprili 6, Siku ya Pasaka baada ya kuombewa na wachungaji kutoka Japan.

Alhamisi iliyopita, alihojiwa kwa mara ya pili na kutakiwa kurudi tena Polisi Aprili 16 akiwa na mambo 10 yakiwamo hati ya usajili wa kanisa, namba ya usajili, majina ya Baraza la Wadhamini, idadi ya makanisa (matawi) anayohudumia, nyaraka za helikopta ya kanisa, muundo wa uongozi wa kanisa, waraka wa maaskofu uliosomwa makanisa yote, nyaraka za nyumba na mali za kanisa na nyaraka kuonyesha taarifa za hesabu kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Hiari.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi leo.

Yeremia 23:1 "watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea,wachungaji wao wamewapotosa"

SO,SISHANGAI WATU WAKE KUENDELEA KUMSHANGILIA NA KUMCHANGIA,ashawateka,ashawachanganya,wanahitaji msaada.
 
Ahaaaaaa Naona kumekucha kwa Gwajima. Lakini pia Gwajima ni mchuuzi wa maji ya chumvi kulee mabondeni, asije akasahau. Na ana Green House ameajili Vijana kutoka Kenya hawana vibali vya kufanya kazi hapa. Sasa kama ana utajili wa kutosha mbona anachuuza maji????SADAKA HAITOSHI?
 
wewe ni Mkristo wa kubumba toka lini serikali itake kanisa kuonyesha waumini wake,mapato yake nk hili ni shabulio kwa UKRISTO ili tu kuudhofisha au kuuweka MFUKONI.
Makanisa yote yenye heshima nchini na duniani hayana kitu cha kuficha.

Ya Kaisari mpe Kaisari.

Huwezi kuwekwa mfukoni kwa kuwa MKWELI.
Onyesha origin ya mapato yako ili uwe huru.
 
sawa hata unamjua huwezi kumwita mtumishi wa Mungu ni mvuta bangi.
Nani kakwambia JG ni Mtumishi wa MUNGU
kachaguliwa na nani?
kasimikwa na nani?
kajifunzia Chuo gani? au ndio UTUME, UPAKO?
anazaa na wanawake wa watu OVYOOOOO
unamjua Emma Mbasha, umeyasoma malalamiko yake, mtu anauza sembe ni mtumishi wako si mtumishi wangu au wa Baniani au wapagani? km ni kwako sawa endelea usiwalazimishe wenzako
attachment.php


Hawa waliopo chini ndio Watumishi wa MUNGU
na imenenwa TIINI MAMLAKA
maaskofu_kikwete.jpg

 
Hivi Kova mlikuwa wapi muda wote huo? Gwajima huduma yake ni ya muda mrefu sasa zaidi ya miaka 10.Kosa kubwa ni kuipiga KATIBA PENDEKEZWA.Fikiri Gwajima kwa maneno yake hayo angeungana na Mhashamu PENGO kwa kuwashauri wa Tz waipigie katiba hiyo NDIYO.Yasigempata hayo.Mbona kuna Manabii na Wachungaji wengi wanaendelea kula bata tena wanaukwasi mkubwa kuliko hao.Kama HAMMER na Helikopta mbona hata wanasiasa wengine wanazo.Ukweli nchi hii bado hatujawa huru.
 
Inakuwaje mambo ya polisi yanakuja kuhubiriwa kanisani hivi huwa ni sehemu ya ibada, kwa nini injili isihubiriwe kama injili bila kuleta mambo ya polisi.

utaratibu wa ibaada huwa ukoje huko?

Huo ni utaratibu wa Gwajima tu!!! sio makanisa yote
 
Lumumba mpo biz kuanzisha thread za Gwajima kupotezea mnavotoa sadaka watu kwenye ajali!
Na leo tena mmefanya! Baada ya kustukiwa kwenye albino sasa mmehamia barabarani!
Kwani damu haijatosha tu?

Ndio haijatosha!! tutafika hadi hapa jukwaani kuwatakatisha watu kama ninyi.
 
Rais wetu kikwete maliza hilo sakata katika waumini wa Gwajima wapo makada wa ccm mule na wapiga kura wako wengi tuu wape furaha wanaoitegemea kwa sasa macho yote kwako mh.

Hawataki washabiki wa gwajima wabaki hukohuko!!!!
 
Nani kakwambia JG ni Mtumishi wa MUNGU
kachaguliwa na nani?
kasimikwa na nani?
kajifunzia Chuo gani? au ndio UTUME, UPAKO?
anazaa na wanawake wa watu OVYOOOOO
unamjua Emma Mbasha, umeyasoma malalamiko yake, mtu anauza sembe ni mtumishi wako si mtumishi wangu au wa Baniani au wapagani? km ni kwako sawa endelea usiwalazimishe wenzako
attachment.php


Hawa waliopo chini ndio Watumishi wa MUNGU
na imenenwa TIINI MAMLAKA
maaskofu_kikwete.jpg


I reserve my comments!
 
Hivi Kova mlikuwa wapi muda wote huo? Gwajima huduma yake ni ya muda mrefu sasa zaidi ya miaka 10.Kosa kubwa ni kuipiga KATIBA PENDEKEZWA.Fikiri Gwajima kwa maneno yake hayo angeungana na Mhashamu PENGO kwa kuwashauri wa Tz waipigie katiba hiyo NDIYO.Yasigempata hayo.Mbona kuna Manabii na Wachungaji wengi wanaendelea kula bata tena wanaukwasi mkubwa kuliko hao.Kama HAMMER na Helikopta mbona hata wanasiasa wengine wanazo.Ukweli nchi hii bado hatujawa huru.

Shirikisha AKILI wakati unajadili na watu wazima, GT. Pengo hakuwaambia waumini wakaipigie kura ya NDIYO. Pengo kawaambia wakaisome katiba waielewe na Kila mmoja kwa uelewa wake na utashi wake akaipigie kura. suala la kura ni la muumini mmoja mmoja jinsi atakavyo.
Gwajima alichemka.
 
Shirikisha AKILI wakati unajadili na watu wazima, GT. Pengo hakuwaambia waumini wakaipigie kura ya NDIYO. Pengo kawaambia wakaisome katiba waielewe na Kila mmoja kwa uelewa wake na utashi wake akaipigie kura. suala la kura ni la muumini mmoja mmoja jinsi atakavyo.
Gwajima alichemka.
Akili zipi? Utajili wa huduma ya Gwajima una uhusiano gani na katiba pendekezwa? jibu swali usiingie kichwa kichwa.
 
Akili zipi? Utajili wa huduma ya Gwajima una uhusiano gani na katiba pendekezwa? jibu swali usiingie kichwa kichwa.

Hoja hapo ni utajiri na siyo katiba, wamemchunguza utajiri haulingani na mapato yanayoonekana ndiyo maana wanataka documents. suala la katiba kila mtu anazungumza hata sheikh mkuu wa DSM aliisha zungumza mara nyingi.
 
Nani kakwambia JG ni Mtumishi wa MUNGU
kachaguliwa na nani?
kasimikwa na nani?
kajifunzia Chuo gani? au ndio UTUME, UPAKO?
anazaa na wanawake wa watu OVYOOOOO
unamjua Emma Mbasha, umeyasoma malalamiko yake, mtu anauza sembe ni mtumishi wako si mtumishi wangu au wa Baniani au wapagani? km ni kwako sawa endelea usiwalazimishe wenzako
attachment.php


Hawa waliopo chini ndio Watumishi wa MUNGU
na imenenwa TIINI MAMLAKA
maaskofu_kikwete.jpg


JK naye ni mtumishi wa Mungu
 
Back
Top Bottom