JK naye ni mtumishi wa Mungu
Ukisoma maneno ya Bwana Yesu kwenye Yohana 19:11,utagundua viongozi wa kiserikali ni watumishi wa Mungu pia soma Warumi 13:1 kwa maana mamlaka yao imetoka kwa Mungu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JK naye ni mtumishi wa Mungu
Ukisoma maneno ya Bwana Yesu kwenye Yohana 19:11,utagundua viongozi wa kiserikali ni watumishi wa Mungu pia soma Warumi 13:1 kwa maana mamlaka yao imetoka kwa Mungu
JK siyo mtumishi wa Mungu hilo nalipinga kabisa
JK siyo mtumishi wa Mungu hilo nalipinga kabisa
ASKOFU Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, amesema yeye si tajiri kama inavyodhaniwa, bali alichonacho ikiwa ni pamoja na nyumba, magari na helikopta ni baraka tu za Mungu, lakini kama ni utajiri, anatarajia siku moja utamshukia.![]()
Aliyasema hayo jana wakati akihubiri kanisani kwake Kawe, Dar es Salaam, ambako alisema anawashangaa watu wanaomfuatilia maisha yake huku wakisema yeye ni tajiri mkubwa.
Wanaodai mimi ni tajiri wana wivu tu na wananionea, mimi si tajiri, bali ni masikini kama walivyo masikini wengine. Natarajia kutajirika hapo baadaye waumini wangu wakiwa matajiri, siwezi kutajirika kama waumini wangu bado ni masikini, nitatajirika pamoja nao, alisema Gwajima.
Kuhusu mgogoro unaoendelea baina yake na Jeshi la Polisi, Askofu Gwajima alisema yeye anauona kama ni vita vya kiroho na hivyo ataendelea kumwomba Mungu ili amsaidie kupambana na kilichopo mbele yake na anaamini kuwa atashinda vita hiyo kwa uweza wa Mungu anayemtegemea.
Mungu wangu na awasamehe wote wanaonituhumu kuwa mimi ni tajiri na kuamua kudhoofisha huduma, nasema huduma yangu haitakufa kamwe na wala hatutayumba katika mipango yetu ya kuhubiri injili. Tutapigana kwa uweza wa Mungu na tutashinda kama alivyosema kuwa tutapigana pamoja naye na tutashinda, alisema Gwajima.
Akizungumzia afya yake, Askofu Gwajima alisema kwa sasa anaendelea vizuri na anaweza kusimama na kutembea, kuhubiri kama ilivyokuwa hapo awali na hatarajii kurejea tena kwenye kiti cha baiskeli ya magurudumu matatu bali atasimama imara daima.
Kuhusu kupeleka nyaraka kadhaa anazotakiwa aziwasilishe polisi siku ya mahojiano Aprili 16, mwaka huu, Askofu Gwajima alisema suala hilo bado wanasheria wake wanalishughulikia na wataendelea kufuata taratibu zote zinazotakiwa na jeshi hilo.
Gwajima anatakiwa kuwasilisha nyaraka muhimu za hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa, hati ya umiliki wa helikopta, hati ya nyumba anazomiliki, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake pamoja na hesabu za fedha za kanisani kwake zinazohusu mapato na matumizi.
Nyaraka zingine ni majina ya Bodi ya Udhamini wa kanisa, mpiga picha za video kanisani kwake siku ya ibada na shughuli zingine za kanisani hapo pamoja na waraka wa Maaskofu uliosomwa makanisani ambao Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alioupinga na kusababisha yeye kumkashifu kiongozi mwenzake huyo wa dini.
Akionekana kuwa makini sana na lugha anayotumia wakati wa kuhubiri, Gwajima aliwaomba waumini wake waendelee kufuatilia kila sehemu na kuchunguza mambo yote mabaya yanayosemwa juu yake na kanisa lake na kuyaripoti kwake au kwa uongozi wa kanisa ili wayafanyie kazi mara moja kabla hayajaleta madhara.
Nawaombeni sana mfuatilie kila chanzo cha habari na kuchunguza mambo yote yanayosemwa juu yangu au kuhusu kanisa na kuyaleta mara moja hapa kanisani ili tuyafanyie kazi kabla hayajaleta madhara makubwa, alisema Gwajima.
Aliongeza kuwa, tuendelee kuwa na umoja katika kipindi hiki ambapo shetani anataka kupigana nasi ili tuweze kushinda. Tukifarakana hatutaweza bali tukiwa kitu kimoja tutasonga mbele na kuwa huru.
Utajiri wake
Wakati akikana kuwa tajiri, mwanzoni mwa mwaka jana alifanya mahojiano na gazeti hili na kukiri Mungu anambariki, ndiyo maana mambo yake yanamnyookea.
Aliyasema hayo alipokuwa anazungumzia mpango wake wa kununua helikopta kwa ajili ya huduma za injili ndani na nje ya nchi.
Alikiri kutokana na utajiri anaosema unatokana na baraka za Mungu, anamiliki jumba la ghorofa nne eneo la Mbezi Beach katika Manispaa ya Kinondoni.
Pia amewanunulia wachungaji wake 40 magari ya kutembelea kwa bei tofauti, yakiwemo ya chini ya Sh milioni 10 na mengine ya zaidi ya Sh milioni 20.
Ni kweli nimewanunulia magari, unajua moja ya misingi yangu ya maisha ni kwamba, mimi siwezi kuishi maisha mazuri, wakati wachungaji wangu wanadhalilika, nimewanunulia magari karibia 40. Lakini nina wachungaji wa ngazi mbalimbali, hawa ni wale wa juu, wengine wachungaji wadogo wapo zaidi ya 670, hawa ni watenda kazi muhimu na wanatofautiana kwa ngazi zao, ndio maana kazi ya Mungu inasonga mbele hata nisipokuwepo, alisema Gwajima.
CHANZO: Habari Leo
Akili zipi? Utajili wa huduma ya Gwajima una uhusiano gani na katiba pendekezwa? jibu swali usiingie kichwa kichwa.
Jibu sahihi ndio hiloJK naye ni mtumishi wa Mungu
Emma. Viongozi wako wanaojitwisha UASKOFU km Gwajima na wengineo wa UPAKO, MITUME nk ambao hachaguliwi ila kujikweza Viongozi wa Kiserikali huwa hawahudhurii kuwekewa mikono kwao au kupandishwa UASKOFUUkisoma maneno ya Bwana Yesu kwenye Yohana 19:11,utagundua viongozi wa kiserikali ni watumishi wa Mungu pia soma Warumi 13:1 kwa maana mamlaka yao imetoka kwa Mungu


gwajima amwambia rais kikwete asimfuatilie fuatilie ama sivyo........
Kama yeye ni msafi kwa nini asiwe huru kupresent nyaraka hizo arafu nachukizwa na mabwege wachache wanaojifanya wanamtetea huyu mpuuzi na uhuni wake wa kuwaibia sadaka maskini wa Tz.Eti ufufuo damn it kama unafufua basi atufufurie JK Nyerere aone li nchi linapoelekea basi wanafufuka watu unknown tu.
majeshi ya bwana. Songa mbele. tulio eohoni tunajua walioko mwilini watahangaika sana. yeremia 1:19 watashindana nawe lakini hawatashinda.MIMI SIO KAMA WALE.Mkuu emma mtumishi wa mungu kwako..mm kanitukania kiongoz wang mkuu wa kanisa mkuu..ulifurahii..mtu mwenye akil timamu awez kuongea vile
Kama yeye ni msafi kwa nini asiwe huru kupresent nyaraka hizo arafu nachukizwa na mabwege wachache wanaojifanya wanamtetea huyu mpuuzi na uhuni wake wa kuwaibia sadaka maskini wa Tz.Eti ufufuo damn it kama unafufua basi atufufurie JK Nyerere aone li nchi linapoelekea basi wanafufuka watu unknown tu.
Jaribu kukutana na mfuasi wake uone jinsi wana imani Kali, wanamtetea baba yao si mchezo, wanaweza kurusha ngumi, yani hizo Mali anazomiliki Gwajey wanasema anasingiziwa na pia wanang'ang'ania kusema muacheni mtumishi wa Mungu.
Kuna kanisa LA mnigeria mmoja lipo karibu na clouds fm mikocheni, huyo kaspecialize kuwaombea waumini wake (wengi wakiwa mademu tena wakali) wapate wachumba, na wale wasiopata watoto, na wanamuamini kinoma,
Watanzania wengi hua wanaabudu binadamu wenzao bila kujua, binafsi hua naamini kuna nguvu za Giza na sio kweli ni nguvu za Mungu wa kweli.
Hapa hapahitaji akili mambo yako wazi. Gwajima awe huru kusema amepata wapi utajili. Mfano Kanisa Katoliki wao wanasoma mapato ya sadaka yao na kila aina ya mchango na matumizi na ndo maana wako huru hakuna la kuuliza hata wanakoziweka wanasema. Hata kama itatokea muujiza gani, jini gani, free mason gani, hakuna chanzo cha kumnunulia hammer gwajima pale Tanganyika Packers, hakuna. Hakuna chanzo cha kununua helicopter pale. Angalia kwa Lusekelo na hadhi ya watu alio nao. Angalia mchungaji Lwakatare na hadhi ya watu alio nao. Sijaona utajili walio nao na wameanza kabla yake. Wale wa Tanganyika Packers ni vishikizo kuna jambo hapa la kujiuliza inawezekana tuna kigugumizi. Nafikiri tuanze kuwa wazi mambo yatafichuka. Mbona Escrow yametimia......
====Waeshimuni watawala wenu, waeshimuni baba na mama mpate miaka mingi na heri duniani====
Baada ya kutoa maelezo, sasa sema hoja yako ni nini?
Unajua hata vichaa huwa hawakubali kama wao ni vichaa na wewe hakika ni Kichaa!
Unamfahamu Papa, kiongozi wa juu wa kanisa katoliki duniani? Unaweza kunikadiria ulinzi wake ni kiasi gani? Kwanini kunakua na ulinzi wakati yeye kiongozi wa dini tena aliyechaguliwa na kuwasha moshi mweupe kwenda angani? Kwanini asimwamini Mungu amlinde tu?
Unaufahamu utajiri wa kanisa katoliki hapa Tanzania? Unaufahamu utajiri wa makada wa CCM hapa nchini? Unaufahamu utajiri wa Ridhiwan au Pinda? Mbona huo utajiri wao haukuumi sana kama utajiri au mali za Askofu Gwajima?
NIKUTOE UJINGA SASA:
Viongozi wa kiroho ni wazazi wetu wa Kiroho na ni jukumu la watoto kuhakikisha baba anakua salama na anaishi vizuri. Baba yako akifanyiwa jambo baya ukifurahia basi wewe utakua si mtoto halali wa baba huyo.
Kuna mambo machache ya kutofautisha hapa; MALI ZA KANISA kama TAASISI na MALI ZA ASKOFU kama mwananchi wa kawaida.. Tunaposhindwa kuambiwa ukweli na Jeshi la Polisi na watu wote wenye nia mbaya na Gwajima ndiposa tunashindwa kujua nini tunazungumza.
Gwajima sio tajiri labda tunamuombea awe tajiri!
-Gwajima ni tajiri kwa Chenge?
-Gwajima ni tajiri kwa Mohammed(Mo)?
-Gwajina ni tajiri kwa Ridhiwan?
-Gwajima ni tajiri kwa Sumaye?
Msituondoe kwenye hoja zetu za msingi za kudai haki katika nchi hii.