Joshua alilisimamisha Jua

Sputam

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
600
Reaction score
390
Katika maandiko matakatifu tunasoma kwamba Joshua alilisimamisha jua, sawa, utata unakuja ninaposoma ktk vitabu vya sayansi kuwa dunia hulizunguka jua sasa najiuliza sipati majibu kuwa wakati Joshua analisimamisha jua yeye Joshua alikuwa wapi? Kwenye jua au kwenye dunia? Jua liko pale pale halizunguki kwenda kokote labda Joshua aliisimamisha Dunia wala sio jua.
Mwenye uelewa mpana ktk hili anisaidie.
 
Biblia inatumia imani kuwaelekeza watu jambo fulani,lakn science inatumia observation and experimentation,kwa hyo kinachooandkwa kwenye Biblia Mara nyingi hakina uhusiano na kile kilichopo kwenye science!
 
Swali lako halina Msingi... Kwani unadhani ukilisimamisha jua lazima ulishike? Inaweza kua alitamka tu kua jua lisimame (lisi elekee kuzama) mfano:- kama ilikua ni saa 10 jioni na anahisi jua litazama kabla ya kupata ushindi na vita bado inaendelea..
 
watanzania wangekuwa na uwezo huo, wangeshasimamisha moyo wa mtu fulani hivi kudunda mda mrefu sana. hahahahah, sema hawana uwezo huo, bali Mungu tu.
 
Mkuu... Joshua atalisimamishaje jua wakati jua wakati Dunia ndio inalizunguka Jua? Jua liko pale pale kwa mujibu wa sayansi... Badala yake Dunia ndio inalizunguka jua... Labda wewe upindue maandiko uniambie kuwa Joshua aliisimamisha Dunia...

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
NIMEKUJA MBIO NIKIDHANI KUWA NI ANTHONY JOSHUA ....nikawa najiuliza huo ubaunsa wakulishika jua na kulisimamisha AJ ameutoa wapi ...!??
kumbe mnaleta mambo yenu hayo ya dini '' haya endeleeni
 
Ndio maana February in siku 28 mwaka mfupi na 29 mwaka mrefu baada ya Joshua kusimamisha Jua kwa siku moja.Haaaa wanasayansi watanibishia ila huo ndio ukweli
Wanasayansi wapuuzi kweli
 
nimekuelewa....naweza sema sema alisimamisha masaa yasiende kabla ushindi haujapatikana
 
ungeanza kujiuliza kwa nini hadi kipindi hiki cha kisayansi kuna maneno SUNST na SUNRISE.

unatumia uwezo wa awali tu, kuwa alimaanisha kinachomaanishwa na wanasayansi sasa kwa lugha ya awali ambayo inaeleweka haraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…