Joti amebeza mchakato wa katiba mpya kwamba hauna tija; nimejiuliza msanii wa Tanzania anawezaje kuwatukana mashabiki zake Bila aibu? Kwamba Joti anajionaa anafaa kuwa DC? Anaona uchawa unalipa? Na kwamba hapo alipofiko ndo mwisho?
Mhe. Rais anataka watu wanaosema ukweli siyo wanafiki; wasanii jifunzeni kumaintain brand yenu. Leo angekuwa na makampuni wanaomdhamini wangevunja mkataba. Hakuna kampuni serious itafanya KAZI serious na thinking ndogo kama hizi.
Jifunze kukaa kimya
View attachment 2504701
Resilience !
Kila mtu anao Uhuru wa kutoa maoni yake,kulingana na anachokiamini,bila kuvunja au kukiuka kanuni na sheria za nchi hii.
Na kwa mujibu wa katiba ya nchi inavyotamka.
Kwa hiyo hupaswi kufanya "Personal Attacks "
Kisa tu!
#Joti ametoa maoni tofauti na unavyoamini na kutaka iwe!
Hupaswi kuwalazimisha watu wote kuamini kile unachokiamini na kukifikiri kichwani mwako wewe!
Kwa sababu sio kila mtu anapitia yale unayopitia wewe!
Kwa mfano....
Wakati wewe ukiendelea kuumia na benchi la siasa,na hivyo kudhani katiba mpya yaweza kuleta upenyo mpya wa kukutoa benchi ulipo.
Yeye Joti.....
Anaendelea kupambana na kukitumia kipaji chake,na kunufaika na mikataba ya makampuni tofauti,ambayo yanamtumia kwenye Brand zao kibiashara.
Tena makampuni hayo,yakiwa yanafanya biashara,na kupata faida nchini,chini ya "katiba" hiyo hiyo ambayo kwako wewe,unaamini imechangia kukuweka hapo ulipo.
Sasa mtu kama huyo,huwezi mlazimisha akuunge mkono kwenye siasa!
Wakati yeye mambo yake yanasonga mbele,tena kwa faida zaidi.
Nyiny...i
Resilience na Joti mko nchi moja ndiyo,lakini mko Pande mbili tofauti za sarafu.
Binafsi Ninajua kabisa,kuna umuhimu wa katiba mpya nchini.ili kuwepo na wigo sawa wa upatikanaji wa tija katika nyanja mbalimbali.
Lakini wanasiasa msiwalazimishe wale ambao,wanayo maoni tofauti na nyinyi kwa wakati husika.
Mleta mada unafanya mambo kwa chuki,huenda unasukumwa na msongo wa yanayokukumba kwa wakati huu.
Hivyo nakushauri kuacha mihemko,huku kwenye Social Platforms,hakuna kundi moja au mtu yeyote mwenye hakimiliki ya mawazo na Imani za wenzie.
Tuwe na utamaduni wa kuwaheshimu na wengine pale wanapokuwa na mlengo tofauti na yale tunayoyawaza na kuamini.