Joti Na Mkewe "HoneyMoon" Wakiwa Singita Grumeti Game Reserve Sabora Camp Serengeti

Mkuu acha kabisa Bora Wewe ulienda camp ambazo zipo karibu na uduma za kibank au malipo.... Hiyo niliyoenda unaacha barabara kubwa unaingia ndani 5km unakutana na geti kuna jamaa wa mabakabaka... Jamaaa alichukua doc akazisoma zaidi YA 15min kama vile anamashaka na Sisi tulikuwa na privt car... Ila wazungu walikuwa wakifika hata dakika 5 ni nyingi wanaachiliwa waingie... Yaaan Sisi ngozi nyeusi tumelaaaniwa atudhaminiani kabisa... Hata wahudumu wa kule ndani YA lodge wanadhamini ngozi nyeupe Sana.... Ila tuache utani kwenda porini ni gharama kuliko kwenda south Africa kupumzika.....
 
Acha kabisa mkuu!
 
Nasikitikaga sanaaa utakuta mtu masikini ametoa mchango kufanikisha harusi ya Joti, katoa kwenye kamtaji kake ka nyanya, karoti na vitunguu kama wale wanaopanga pale stand Mbezi jioni. Alafu yeye yupo kula honeymoon,, kweli masikini rafiki yake tajiri tuu
 
sijui kwanini,karibia kila kitu anacho fanya joti nahisi kama ni comedy...lol.

pongezi nyingi sana kwake na kwa mke wake kwa kuamua kwenda kulia fungate yao mbugani badala ya kwenda kwenye mahoteli maarufu jijini dar es salaam au Zanzibar.
 
Daah mi nashukuru nilibahatika kishule shule kwenda Ngorongoro, Serengeti na Manyara...

Na ule utoto sikujua kama kuna usumbufu huu mnaousema!
 
Daah mi nashukuru nilibahatika kishule shule kwenda Ngorongoro, Serengeti na Manyara...

Na ule utoto sikujua kama kuna usumbufu huu mnaousema!
Mkuu zile za kishule au zile za Offer ya Ncca kwa basi lao hazina thrilling yoyote!! Ndiyo maana hata wao huwa hawahangaiki nazo,kwanza mnakimbizwa kama mwenge wa uhuru!!hakuna kushuka popote hata getini! Shida ni hizi za kifamilia! Muwe wawili/watatu na kigari chenu binafsi Ndiyo mtanyooka!
 
Hapo kwenye master card na visa card ni kasheshe lkn ni kwa mbuga za TANAPA tu zingine unalipa hata cash kama mikumi n.k. Wakati umefika hata mitandao ya simu itumike kama wanaogopa kuibiwa cash huko porini. Kumbe tunakataa wenyewe fedha halafu tunalalamikia wananchi hawaendi mbugani.
 
Aisee nimeingiwa na uwoga mkubwa sana, nilitaka kwenda huko na malaya wangu kumbe ndio kunasumbua hivo halaf promo nyingi kuweni wazalendo mkatembee mbuga
Labda utafute gari la wanafunzi wanaokwenda uende nao,inaweza kukupunguzia usumbufu kidogo!
 
Reactions: SDG
Yaaan na kweli tu...full kukimbizwa kimbizwa daah

At least Manyara niliinjoi kidogo
 
Nchi yangu Tanzanian pahala pekee unapoweza kuwaona wanayama wakiwa kwenye mazingira yao asili kama ulivyokuwa mpango wa Mwenyezi Mungu alipoiumba dunia
 
Wasimamiz na guider wa mbugani wafundishwe kuondoa ule ushamba wa kuonesha dhalau kwa wazawa kisha wataona jinsi mbuga zitakavyofurika wabongo,
Kama hawatak waondolewe wawekwe wapya, kingwangala nakuaminia mkuu kama unapita hapa kuna dr. Mwaka mwingine kwenye mbuga zetu
 
Kuna nini huko swala na tembo# mi nilienda ka mikumi tu hapakuwa na usumbufu
 
Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…