View attachment 623974 View attachment 623974
Jumlisha na ubaguzi wa rangi mkuu! Ningehadithiwa ningebisha! Card yangu (master) niliyoitumia siku hiyohiyo pale karatu kufika getini naambiwa haifai!! Watu watatu pamoja na gari yetu tulitakiwa kulipa shilingi 77,800/, wale askari wa getini wakaniambia kwa kuwa kadi yangu haifai niwape wao shilingi 120,000 ili wanisaidie kulipa,nikawaambia hicho ni kiasi kikubwa mno,wakaniambia kama hutaki basi ondoa gari lako hapa sasa hivi!! Nikawauliza niliweke wapi wakati bado sijalipia? Nikawaambia wasubiri kuna mtu nimewasiliana naye anakuja kulipa,wakaondoka,baada ya dakika tatu tu wakarudi! Wakanishurutisha niondoe gari langu pale mara moja kwa kuwa nimekataa msaada wao hivyo sina nia ya kulipa! Wakati tunazozana pale mtu niliyewasiliana naye akaja,akaenda kulipa,akaambiwa network mbaya hivyo tuingie tukalipie makao makuu ya Ngorongoro!wakati huyu mwenye kadi yake alipaswa kurudia tu pale getini,yaani nilijuta kwenda huko