Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tetesi za Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kugombea uenyekiti wa chama hicho zikiendelea kusambaa, maoni mseto yameibuka miongoni mwa wanachama.
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Makambako, Begron Kyando, amesema ni wakati wa Freeman Mbowe kuachia nafasi hiyo baada ya kuongoza kwa muda mrefu, huku Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Iringa Vijijini, Rachel Lema, akisisitiza chama kinahitaji mabadiliko na kiongozi mkakamavu kwa sasa.
Lema ameongeza kuwa Mbowe anaweza kubaki mshauri wa chama, akitoa mfano wa Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo. Alimtaja Lissu kama anayefaa kuendana na mazingira ya sasa ya kisiasa nchini.