Joto likipanda utasikia ni uchafuzi wa mazingira, baridi likizidi wanafunga midomo hawana majibu

Joto likipanda utasikia ni uchafuzi wa mazingira, baridi likizidi wanafunga midomo hawana majibu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Kuna wakati Mimi napingana na sayansi ya mazingira. Mara nyingi hata kwenye mikutano ya kimataifa wanajadili global warming ambayo inasababishwa na shughuli za kibinadamu kama viwanda, kilimo, uvuvi n.k.

Lakini kuna misimu mingine ya baridi kwa maeneo mbalimbali duniani inapita kawaida yake na kufanya baridi kuwa kali zaidi mpaka kusababisha vifo kwenye baadhi ya maeneo.

Sasa unajiuliza miezi michache tu au miaka michache tu nyuma kuna watu walikuwa wanatoa speech kuhusu global warming katika dunia au maeneo fulani unajiuliza ndani ya muda mfupi huu mwanadamu ameshaacha kuharibu nature nasasa baridi limeongezeka?

Mfano: Baridi la Dar es Salaam msimu huu wa baridi limekuwa kali kuliko miaka mingi iliyopita. Je, kuna mwanasayansi anaweza kuthibitisha kuwa Dar shughuli zinazoharibu mazingira zimekoma?
 
Hali ya hewa inajumuisha vitu vingi ikiwemo baridi,ukungu,joto,upepo n.k(rejea vtabu vya drsiv&v&kidato)
Hivyo vyote vinatakiwa vitokee katika uwiano sawa kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
Ikitokea kimojawapo kikazidi kingine ktk eneo hilo hilo ndo huitwa MABADILIKO YA HALI YA HEWA.

Zaidi waje wataalamu waeleze.
cc Mwalimu Hema & MWALIM WA KIJIJINI & mwali wa giningi
 
Unatia huruma kwa jinsi ulivyo mjinga, ila ujinga si tusi.

Sikia nikueleweshe, ‘Global warming’ haisababishi hali ya hewa kuwa ya joto tu, bali inaweza kusababisha hali ya hewa kuwa ya joto kali kuliko kawaida na kwa kipindi kirefu kuliko kawaida, pia inaweza kusabisha hali ya hewa kuwa ya baridi kuliko kawaida na kwa kipindi kirefu kuliko kawaida, kwa kifupi ‘Global warming’ huleta ‘Climate change’.
 
Unapoelekezwa basi ni jambo jema kurudi kutoa mrejesho.Hii itawashawishi watu kuwa wanajitoa zaidi kushauri/kuelekeza.
cc Sandali Ali
 
Mkuu uharibifu wa mazingira bado ni mkubwa kuliko vipindi vya baridi unavyoshuhudia.

Mfumo wa anga umeharibika ndiyo maana unashangaa mvua za April au November to December huzioni, hii hali ya ubaridi inabadirika ni kutokana na uharibifu huu ninaosema.

Fikilia njaa inayokuja kwa sababu ya ukosefu wa mvua za wkt kwa msimu uliopita, kwa Dar watu walizoea mafuriko kwa mwezi wa kumi na mbili ila hayakuwepo ya kutikisa.


20220428_080647.jpg

Global warming it's real and is there asee tutunze mazingira.
 
Back
Top Bottom