DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kijana Jovin Kaaya, Mzaliwa wa King’ori, Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, amesimulia safari yake ya kukamatwa, kushitakiwa kwa kosa la uhaini, pamoja na hali na maisha aliyopitia akiwa chini ya uangalizi wa Vyombo vya Dola kuanzia Kituo cha Polisi hadi alipofikishwa Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.
Jovin, ambaye hivi karibuni alipata umaarufu mkubwa mitandaoni, aligusa hisia za Wananchi wengi baada ya kuonekana katika picha na video akimbeba mgongoni mara kadhaa mwenzake Baraka Chacha, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka ya kosa hilo hilo la uhaini.
Baraka alikuwa katika hali ya kutoweza kutembea baada ya miguu yake yote Miwili kuvunjika.
Akizungumza jana, Desemba 29, 2025, akiwa nyumbani kwao Arusha, Jovin amesema alishuhudia tofauti kubwa ya mazingira na huduma kati ya kipindi alipokuwa chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na alipofikishwa katika Gereza la Segerea.
Amesema walipokelewa kwa utu na kuoneshwa ushirikiano mkubwa na askari magereza, ambapo yeye na wenzake walipatiwa huduma mbalimbali ikiwemo matibabu.
“Tulipokelewa vizuri, tukapatiwa matibabu, na maisha yalikuwa tofauti kidogo ukilinganisha na kule Kituo cha Polisi,” amesema Jovin.
Pia Soma: Jovin Kaaya: Nilivyotajiwa uhaini mahakamani nilimkumbuka Tundu Lissu