PostGE2025 Jovin Kaaya: Nilivyotajiwa uhaini mahakamani nilimkumbuka Tundu Lissu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kijana Jovin Kaaya, mzaliwa wa Mkoa wa Arusha, amesimulia kwa kina sakata la kukamatwa kwake jijini Dar es Salaam Oktoba 31, 2025 na kushtakiwa kwa kosa la uhaini, hadi kuachiwa huru baada ya kesi hiyo kufutwa rasmi na Mahakama Desemba 24, 2025.

Akizungumza na Jambo TV jana Desemba 29, 2025 akiwa nyumbani kwao eneo la King’ori, Wilayani Arumeru, Mkoani Arusha, Jovin amesema tukio hilo lilimpa mshtuko mkubwa kutokana na uzito wa tuhuma zilizokuwa zinamkabili.

Jovin amesema siku ya kwanza alipofikishwa mahakamani na kutajwa kosa la uhaini, alipatwa na hofu kubwa, hali iliyochochewa zaidi na kumbukumbu ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu

Amesema wakati huo hakuwa na Wakili wa kumtetea, jambo lililomfanya ajisikie yuko hatarini na kukosa mwelekeo wa nini kingefuata.

Jovin alipata umaarufu mkubwa mitandaoni baada ya kuonekana mara kadhaa akimbeba mwenzake Baraka Chacha, aliyekuwa anashitakiwa naye kwa kosa hilo la uhaini, kutokana na Baraka kuwa na miguu yote Miwili iliyovunjika.

Kitendo hicho cha upendo, mshikamano na utu wakati wa kuingia na kutoka Mahakamani kiligusa hisia za Wananchi wengi, na kumfanya Jovin kutambulika kama kijana mwenye huruma na moyo wa kujali wengine, licha ya changamoto nzito na shinikizo kubwa alilokuwa anakabiliana nalo katika kipindi hicho kigumu.
 
Lissu ataendelea kukumbukwa vizazi na vizazi kwa miaka ijayo 1000
 
Back
Top Bottom