JPM hatajwi kabisa inavyostahili kwenye hili jambo la bwawa la umeme

JPM hatajwi kabisa inavyostahili kwenye hili jambo la bwawa la umeme

nkoge

Member
Joined
Jun 7, 2018
Posts
53
Reaction score
90
Salaam!

Ni kweli,hii ni ndoto ya Mwalimu Nyerere iliyobadilishwa kuwa uhalisia na Rais wa awamu ya tano ndugu JPM ambaye alimwachia kiti chake Daktari Samia Suluhu Hassan

Ajabu katika Kila kinacjofanyika hakuna mtu anataka kulitaja jina la mtekelezaji wa ndoto.Wasemaji wote wanaanzia Kwa Mwalimu Nyerere na kuruka mpaka Kwa Samia Suluhu Hassan.

Hii inatakafarisha sana.
 
Pamoja na kutomgaja lakibi idadi kubwa ya watanfanyika tunajua yeye ndiye amefanikisha hili bwawa.huyu wa sasa hamna kitu cha maana amefanya zaidi ya kuteka watu.
 
Salaam!
Ni kweli,hii ni ndoto ya Mwalimu Nyerere iliyobadilishwa kuwa uhalisia na Rais wa awamu ya tano ndugu JPM ambaye alimwachia kiti chake Daktari SSH.
Ajabu katika Kila kinacjofanyika hakuna mtu anataka kulitaja jina la mtekelezaji wa ndoto.Wasemaji wote wanaanzia Kwa Mwalimu Nyerere na kuruka mpaka Kwa SSH.
Hii inatakafarisha sana.
Umesema jambo la msingi sana. Tuwe wakweli tu, bila kuingiza ushabiki wa kisiasa. Ni kweli kabisa kwamba hili lilikuwa ni wazo la muda mrefu la Mwalimu Nyerere, lakini JPM ndiye aliyelifanyia kazi kwa msukumo mkubwa na kulitoa kwenye hatua ya ndoto na kulipeleka kwenye utekelezaji.

Sasa leo ukimsikia mtu akizungumza kuhusu bwawa hili anamtaja Nyerere, anamtaja SSH, lakini JPM anapita kimya kimya kana kwamba hakuwahi kuwepo kwenye historia ya mradi huu. Hii si sawa.

Kumtaja JPM kwenye hili si kwamba tunamsujudia au tunasifia kila kitu alichofanya. Ni kutambua mchango wake pale unapostahili kutambuliwa. Historia haiwezi kufutwa kwa sababu tu mtu fulani alikuwa na madaraka kipindi fulani.

Nyerere alikuwa na maono, JPM akayasukuma kwa vitendo, na SSH akaendeleza kazi. Kila mmoja apewe nafasi yake kwenye historia.
 
Washasema la mama yao, usijeshangaa ikapelekwa hoja na babalevo kule chumbani dodoma kwamba walibadilishe jina liwe na malkia rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa kwa kura nyingi kuliko mwingine yoyote tangu kuumbwa kwa dunia na aliyewapa ubonge bure! Level ya kina kagame na kim jon un
 
Ili idhihirike kuwa walimuua lazima hayo yafanyike màana walimuua kwa kuona alikuwa mbaya kwa taifa sasa mtu aliyekuudhi mpaka ukamuua huwezi kumsifia maana utaonekana ulimuonea.

Hii historia ya mchongo wanayoiandika ipo siku atakuja mzalendo ambaye ataweka mambo sawa na Magu atapata haki yake stahiki katika kufanya miradi mikubwa ambayo hapo mwanzo zilikuwa ni ndoto lakini yeye akazitafasiri kuwa uhalisia. Haya madhalimu hayana muda mwingi sana wa kutamalaki bado kitambo kidogo tu mengine yatajifia na mengine yatakosa ushawishi na kuondolewa madarakani.
 
Salaam!
Ni kweli,hii ni ndoto ya Mwalimu Nyerere iliyobadilishwa kuwa uhalisia na Rais wa awamu ya tano ndugu JPM ambaye alimwachia kiti chake Daktari SSH.
Ajabu katika Kila kinacjofanyika hakuna mtu anataka kulitaja jina la mtekelezaji wa ndoto.Wasemaji wote wanaanzia Kwa Mwalimu Nyerere na kuruka mpaka Kwa SSH.
Hii inatakafarisha sana.
Unachosema ni kweli mimi mwenyewe nimesikiza hotuba yote mwanzo mwisho hakuna sehumu waliyomtaja Magufuli wanaanza kwa Mwalimu wanaruka kwa Samia
 
Back
Top Bottom