Jua kesho tarehe 21 Machi litaingia Ikweta, Masika kuanza

Jua kesho tarehe 21 Machi litaingia Ikweta, Masika kuanza

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema!

Joto la leo likanifanya niikumbuke Jiographia ya Kidato cha Kwanza.

Leo na kesho Tarehe 20 na 21 March Jua litakuwa Ikweta baada ya kuingia katika kizio cha Kusini (Southern Hemisphere) Tropical of Capricorn tangu mwaka jana Septemba lilipokuwa pia Ikweta.

Hivyo ni kusema jua limetokea Kusini na hivi leo na kesho litakuwa Ikweta likiigawanya Dunia katika mapande mawili yaliyolingana.

Kumaanisha usiku na mchana kutakuwa sawa na hii wanajiografia wanaiita EQUINOX yaani usiku na mchana kulingana.

Kumaanisha kuanzia tarehe 22 masika umeanza, mvua katika baadhi ya maeneo zitaanza kunyesha hasa kwenye wiki ya mwandamo wa mwezi katika siku 10 mpaka 15 zijazo.

Jua huwa Ikweta mara mbili kwa mwaka 20, 21 March ambayo hutambulika Vernal Equinox ambapo Msimu wa Masika huanza, na usiku na mchana hulingana.

pPa 22, 23Septemba ambayo hutambulika kama Autumnal Equinox ambapo msimu wa Vuli huanza, pia urefu wa usiku na mchana hulinganana.

Jua kwa sehemu kubwa ndio huongoza hali ya hewa na tabia ya nchi.

Masuala kama ya jotoridi, kiwango cha unyevunyevu angani, upepo, mawingo, mvua huratibiwa kwa kiasi kikubwa na jua.

Miale ya jua huchangia pakubwa.

Hata hivyo upo uhusiano wa mwezi kuandama na mabadiliko ya halo ya hewa Kwa baadhi ya maeneo.

Endapo jua litakuwa Ikweta basi mambo yafuatayo yanatarajiwa,
1. Ongezeko la joto Kali
2. Mlingano wa usiku na mchana
3. Mvua kuanza kunyesha hasa siku chache kabla ya mwezi kuandama n.k.

Athari za kiafya zinazoweza kujitokeza:

1. Watu kuumwa kifua na mafua kutokana na wengi kulala usiku wakiwa wamepunguza vyakujifunika, ilhali nyakati za usiku wa manane hali ya hewa hubadilika na kuwa ya baridi.

Hivyo mapafu huingia unyevuunyevu kutokana na baridi.

Tutarajie mvua Maeneo ya Dar es Salaam kwani na maeneo mengi ya Pwani kuanzia wiki hii kutokana na kutakuwa na ongezeko kubwa la unyevu unyevu angani kutokana na joto na uwepo wa bahari hivyo mvua itanyesha.

Naomba niishie hapa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom