Katika pitapita zangu nimekutana na hii situation ikijadiliwa kuwa wakati wa mawio hadi kufikia mida ya saa 2 na pia mida ya kuanzia saa 12 kasoro mpaka jua linapochwaa, hilo jua tunaloliona si jua halisi. Ni taswira tu
Kuna ukweli wowote kwenye hili?
Kuna ukweli wowote kwenye hili?
- Tunachokijua
- Jua ni nyota kubwa na muhimu kwa maisha ya viumbe hai waishio duniani kutokana na kutoa nishati inayotoa mwanga na joto kwa dunia. Kadhalika ni chanzo cha uwepo wa usiku na mchana, misimu na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Tovuti ya National Geograpgic inaeleza kuwa Jua limeundwa na matabaka ambayo kwa ujumla wake ni gesi ya hydrogen na helium ambapo gesi hizi huwa na kazi tofautitofauti katika kila tabaka. Matabaka ya jua hupimwa kwa asilimia ya jumla ya kipenyo cha jua.
Kumekuwepo na hoja kwamba jua la wakati wa mawio na machweo si jua halisi ukilinganisha na jua linaloonekana wakati wa mchana, au baada ya mawio asubuhi na kabla ya machweo jioni.
Ni upi uhalisia wa hoja hii?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa jua linaloangaza wakati wa mawio na machweo halina utofauti na wakati wa baada ya mawio na kabla ya muda wa machweo. Wakati wa asubuhi na jioni jua huwa mbali na uso wa dunia na hivyo kusababisha miale ya jua kusafiri umbali mrefu kuelekea anga letu na hivyo kusababisha hali ya rangi ya njano, chungwa au nyekundu lakini haiondoi uhalisia wa jua.
Mzunguko wa jua kila siku kupitia anga ni kawaida kama ilivyo kwa nyota, huchomoza kutoka upande wa mashariki na machweo yake kuwa magharibi, na hukamilisha mzunguko kwa masaa 24 huku ukichukua siku 25 mpaka 35 kukamilisha mzunguko wake kwenye njia yake kama dunia.
Tovuti ya Environmental Protection Agency (EPA) ya nchini Marekani inaeleza kuwa Jua linatoa nishati yake kuelekea duniani kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitia mwanga unaoonekana, mionzi ambayo haionekani bali kwa kuhisi kama joto, na miale ya mionzi ya Utra Violet ambayo haionekani kwa macho wala kwa kuhisi.
Kuna sababu kadhaa ambazo zinachangia miale ya jua kuwa na nguvu zaidi na kusababisha joto kubwa kutokana na miale hiyo kusafiri umbali mfupi kuelekea uso wa dunia jambo ambalo huweza kusababisha utofauti kwa kulitazama kati ya jioni asubuhi na mchana, mfano wakati wa mchana jua huwa karibu na uso wa dunia ukilinganisha na asubuhi na jioni, wakati wa kilele cha jua la utosi, vipindi vya mwaka kipindi ambacho jua huwa na nguvu kubwa kupitia mionzi inayoelekea duniani.
Katika kuangazia uhalisia wa rangi ya jua kwa kuzingatia vipindi vya siku, Wakati wa mawio na machweo kuenea kwa bluu na zambarau kunaweza kuonekana kiasi kwamba jua linaweza kuonekana kuwa na rangi ya njano, machungwa, au hata rangi ya shaba. Lakini uhalisia ni kwamba jua lenyewe ni jeupe. Jua ni jeupe linapotazamwa kutoka angani na pia ni jeupe linapotazamwa kutoka uso wa dunia (isipokuwa muda mfupi wakati wa alfajiri na machweo).
Asubuhi na jioni jua huonekana kuwa na rangi nyekundu, kwa sababu miale ya mwanga wa jua husafiri umbali mrefu zaidi angani ambapo husababisha kusambaa kwa rangi ya njano pia lakini jua halina tofauti.