Kuna kitu kimoja Wakenya tunafaa tuelewe, vita vya ukabila huwa havina mshindi, tutanyukana hiyo tarehe 26 na kumwaga damu lakini mwisho wa siku hakuna atakayeibuka mshindi. Haijalishi utaua Wakikuyu, Wajaluo wangapi lakini baada ya hapo utakuja kugundua hakuna aliyeshinda.
Hitler aliwachinja Wayahudi mamilioni, lakini leo hii yupo kaburini na hakuibuka na ushind wowote. Wengi huwa mnasema vita huleta hesima eti tuchinjane ili tuheshimiane, huo ni uwongo, pale Rwanda asikudanganye mtu, wale watu hawana amani ya ukweli maana sioni jinsi nitaishi na mtu aliyechinja watoto wangu eti tunachekeana kila siku, itakua usanii na ipo siku nitapata fursa lazima nimtenganishe na kichwa chake.
Hivyo tuhubiri amani, pande zote mbili tunanoa mapanga na kueneza chuki kwenye mitandao lakini ipo siku tutaitamani hii amani ya leo. Tumechonganishwa na hawa viongozi kama makondoo na kukubali kauli zao, wakati wao watahama hili liinchi na kuacha tukipokezana mapanga. Mimi yangu macho......