Jubilee ya miaka 70 ya taifa la Israel na ufunguzi wa ubalozi wa Marekani katika jiji la Yerusalem

Jubilee ya miaka 70 ya taifa la Israel na ufunguzi wa ubalozi wa Marekani katika jiji la Yerusalem

MWAISEMBA CR labda nikuulize umejuaje kama hawa waisraeli waliorudi ndio waisraeli halisi ina maana yale makabila yaliyopotea mmeshayapata mpaka useme wamesharudi israel???

Swali jingine hao waliorudi 90% ni Ashkenazi mbao mpaka leo kuna mjadala kma ni waisraeli halisi au ni wayahudi kwa kubadilisha dini tu maana hakuna ushahidi kama ashkenazi wana damu ya yakobo zaidi ukisoma historia yao utagundua walitoka ukoo wa japhet je ina maana hili hulifahamu

3. Hivi utajuaje kama ni unabii wa Mungu umetimia sasa?? What if ni agenda ya PROJECT BLUE BEAM kutuaminisha unabii umetimia ili watuletee YESU FEKI mawinguni??? Maana sijaona makabila yale 10 yakirudi bado sijaona nabii aliyewarudisha zaidi ya mafreemason wachache kutoka uingereza..... Je tutafahamuje ni Unabii wa Mungu na sio kuna wajanja wachache wanacheza na maandiko ili kutuzuga unabii unatimia ili kuwapa Hawa Israel feki uhalali wa kuitawala PALESTINA

Embu tusaidie na haya maswali
Na kweli mkuu hapa ndo mahali atakopotea Yesu feki ktk project yao mpya ya The blue beam....wayahudi feki hao...
tapatalk_1525714196963.jpeg
 
* MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳SOMO LA 4⃣ : MAANA YA 70 KIBIBLIA KWA ISRAEL NA KANISA✳*

*Na: Shujaa Charles Mwaisemba*

* VIKAO VYA VIONGOZI WA DINI MAREKANI PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI NA BUNGE JUU WAKATI WA BWANA*
*MAANA YA 70 KIBIBLIA JUU YA ISRAEL NA KANISA*
*DONALD TRUMP KUTANGAZA RASMI KUUTAMBUA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*1⃣ UTANGULIZI*

Tuliona kwenye Sehemu iliyopita Kuwa hata Rais Donald Trump kwa mara ya kwanza nae alivyoingia madarakani jinsi kulivyokuwa na uzito mkubwa fulani kutoka kila kona duniani kuwa endapo angetangaza kungeweza kuleta machafuko hivyo kumpelekea nae baada ya mezi 6 kupita alihairisha utekelezaji wa ile sheria ya mwaka 1995 ya marekani kuutambua Yerusalem kama makao makuu ya Israel.Sasa leo tunaendelea kutokea hapo na ikiwa hujaanza na mimi tangu Somo la 1⃣ la mfululizo huu basi wasiliana nani nikupatie

*2⃣ VIKAO VYA VIONGOZI WA DINI MAREKANI PAMOJA NA VIONGOZI WA KISERIKALI NA BUNGE JUU YA WAKATI WA BWANA*

Baada ya Trump kushindwa kutangaza kwa mara ya Kwanza,Walijikusanya Viongozi wengi wa dini wanaoyaelewa maandiko Kuanzia mwezi 10,11 na 12 mwaka 2017 na kufanya vikao mbalimbali vya watu waliokuwa wanatafakari juu ya Neno la Mungu na wakati wa Mungu

Hivyo kuliendelea kuwepo na watu mbalimbali ambao walisukumwa kwa msukumo usiokuwa wa kawaida wa Roho mtakatifu, wakawa wanafanya vikao mbalimbali na kila mmoja kutoka huku na kule akawa anaingiziwa msukumo tofauti kabisa wa KiMungu ndani yake kwamba ni kweli hapa katikati tangu mwaka 1995 jambo hili halijawezekana kwasababu wakati wake ulikuwa bado lakini sasa mwaka 2017 huu ndio Wakati wa Bwana umefika kwasababu ni *MIAKA 70* imetimia baada ya mwaka 1947 kwenye ile kura ya Mwanzo ya Umoja wa Mataifa ambayo ndiyo iliyosababisha Kuwako kwa Taifa la Israel mwaka uliofuata

Hivyo wakawepo wanazuoni,wakawepo watu ambao wanachambua maandiko,Wakawepo wale watu wanaotoka huku na huku wakamkarisha chini Rais wa sasa wa Marekani, *Donald Trump* na viongozi kadhaa wa serikali na Viongozi wa Bunge na kuanza kuchambua kuhusu 70

⚠Hata Kanisa la Mungu tunatakiwa tuifahau 70 katika mpango wa Mungu......

*3⃣ MAANA YA 70 KIBIBLIA JUU YA ISRAEL NA KANISA*

Sasa Sabini(70) katika Israel ina kitu kikubwa sana katika mpango wa Mungu..Na Vile Vile *Sabini(70)* Inazungumzia juu ya *NYAKATI ZA MWISHO ZA KUMALIZIA*

Ndio maana ni vyema Kulifahamu hili nyakati zote,Maana Mungu amekuwa akisema na Kanisa lake kwanza kabla ya kutokea kwa wengine

Hivyo lile kusanyiko lililowaita Viongozi wa kiserikali na Viongozi wa Bunge la Marekani pamoja na Rais wakitafakari wakati wa Bwana ndio ikaja Kwamba Mwaka 2017 ni Mwaka wa 70 baada ya ile Kura ya Mwaka 1947 na ikaja habari ya Mwaka wa 70 kuhusiana na Israel(Jubilee ya miaka 70),kuhusiana na Wakati wa Bwana

*♨{ YEREMIA 25 :11-12}*
_"Na nchi hii yote pia *itakuwa ukiwa*, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli *miaka sabini(70)*.Na itakuwa miaka hiyo *sabini(70) itakapotimia*, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele."_

*♨{YEREMIA 29:10-11}*
_"Maana BWANA asema hivi, Babeli *utakapotimiziwa miaka sabini*, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa *kuwarudisha mahali hapa*.Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini *siku zenu za mwisho*."_

Mwaka wa 70 katika mpango wa Mungu na hususani kwa Israel na hususani kwa Kanisa lake ambalo tunasimama kama Israel ina maana kubwa sana ikizungumziwa na kuhusishwa na siku za Mwisho kama tulivyoona na siku za Mwisho
*Maana ya 70 inatupa tafsiri tatu za kibilia*

*1) Ni mwaka wa Kutimiza Neno lake la kuwajiria Watu wake au Kurudi kwake kuwaokoa na kuwasaidia Watu wake*.Utaona Sehemu Nyingi ambapo biblia inataja 70 juu ahadi ya Mungu kutimizwa kwa watu wake.Na Kwa kanisa Ahadi kuu tunayoisubilia ambayo Mungu alituahidi watakatifu ni kuja kwa Yesu kulinyakua Kanisa lake.Hivyo Neno hilo nalo litatimizwa Kama alivyosema

*2) Ni Mwaka wa Kurudisha Walio wake*.
Kipindi hichi kutakuwepo na wimbi la watu wengie Kumrudia Mungu kwa toba,Waliokuwa wamerudi Nyuma wataanza tena kusikia Sauti fulani ya Roho mtakatifu ikiwakumbusha juu ya Toba(Usiipuuze sauti hiyo).Ni mwaka Ambao Hata wengi ambao hawajaokoka wataokolewa kwa wingi wake .Hata wale wateule Shetani aliotaka kuwapoteza zaidi watarudi tena kwenye njia na wataisikia sauti ya Bwana wao

*3) Ni mwaka wa Mawazo mema ya Mungu kwa Watu wake Na kanisa lake YEREMIA 29:10-11*.

Utaona Mwaka huu wa 70 unazungumziwa pamoja na Siku za Mwisho

*♨{DANIELI 9:1-2}*
_" .................katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, *kwa kuvisoma vitabu,* nalifahamu *hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii*, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, *miaka sabini.*

Utaona Daniel hapa,hìi yote mpaka mwisho anazungumzia juu ya siku za Mwisho,Mfano *(DANIELI 12:9)*

Kwahiyo Sabini,Sabini ,sabini,Sabini kwa habari ya Israel inazungumzia vilevile juu ya Nyakati za Mwisho juu ya Kanisa wa majir

4⃣ RAIS WA MAREKANI,DONALD TRUMP KUTANGAZA RASMI KUUTAMBUA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL

Ndipo Katika kikao kile baada ya Trump Kukaa nao,Roho alishuka kwa namna ya ajabu sana ikajulikana ilikuwa Mwaka 1947 kura ile ya Umoja wa mataifa ilipigwa na Mwaka 2017,Miaka sabini(70) ilitimia wakati umefika wa kutangaza Kulitambua mji wa Yerusalem kama makao makuu

Na ni tangazo linalotolewa mwaka wa 70 lakini kumbuka linatolewa katika mwaka 70 katika nchi ile ile ambayo Umoja wa mataifa una Makao makuu (Marekani)
Lakini zaidi sana Tangazo la Kuutambua Yerusalemu kuwa Makao makuu ya Israel liliyolewa vilevile Muda mfupi kabla ya Jubilee ya Miaka 70 ya Israel ya Israel ambayo imefanyika 14/5/2018 mwaka huu.

Sabato ya Miaka 70,mwaka huu 2018 tarehe 14/5/2018 taifa hili la Israel linakuwa limetimiza Miaka 70 ya kuwapo kwake tangu lilipotangazwa kuwepo 14/5/1948(Sabato ya Miaka 70) ambayo inaashiria kitu kingine Kikubwa na ni Mwanzo wa kuyaona Mengi ya KiMungu na kinabii juu ya dalili za kuja kwake Kristo yakitimia kwa haraka sana

Kabla ya wakati ule mwaka wa 70 katika nchi ile Tangazo linatolewa *TUNAITAMBUA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL* (Imekuwa ni Sheria yao israel kwamba ni Makao makuu tangu mwaka 1950)

Lakini Hapa anasimama Huyu *Rais wa Marekani (Donald Trump)* Kulitangaza hili kwa mara ya Kwanza kwamba anaitambua Yerusalemu Kama makao Makuu ya israel mwaka 2017, na Kuamua Kuhamisha Rasmi ubalozi wake Kutoka Telhaviv(Makao makuu ya awali ya israel) na Kupeleka Rasmi Yerusalemu Siku ile ile ambayo ndiyo Kulikuwa na Jubilee ya Miaka 70 ya Israel

✍Usikose kufuatilia sehemu ya 5⃣ ya Mfululizo huu ambapo utajifunza mambo mengi yajayo tunayotarajia kuyaona yakitokea kabla Kanisa halinyakuliwa.Ila Mpaka hapa Jiulize wewe umejifunza Nini?

Mungu anakupenda sana ndugu yangu ndio maana amekupa hamasa Kuyafuatilia na kulisoma Somo hili,anataka likupe kujiweka tayari na Unyakuo ambao upo karibi sana kutujilia!Je utaendelea na maisha haya ya dhambi uliyo nayo❓ Inawezekana ni kweli umekoka lakini unayaona maisha yako kama huyaelewi elewi hivi,unajikuta unaanguka anguka kwenye dhambi,Unajikuta hauna uwezo wa kushinda dhambi❓Inawezekana ni kweli ulishawai kuokoka ila umerudi nyuma,Je utaendelea na maisha hayo?

Nisikilize Ndugu yangu neema bado ipo,Usijihukumu kwa dhambi unazotenda au ulizotenda,Mungu anaangalia umaliziaji sio Uanzaji.ikiwa unahitaji uwezo wa Kushinda dhambi au unahitaji maombi ili upate Nguvu za Kumalizia basi wasiliana nami nitakuombea utapokea nguvu hiyo mpya

*♨Kwa mawasiliano zaidi au Ushauri*

*Na: Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
*MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳SOMO LA 5⃣ : VIASHIRIA VYA KUBOMOLEWA VYA MSIKITI WA AL-AQSA(DOME OF THE ROCK)✳*

* Na :Shujaa Charles Mwaisemba*

*KUBOMOLEWA KWA MSIKITI WA AL-AQSA(DOME OF THE ROCK)*

*ONYO KWA KWA WAKRISTO KUSHABIKIA KUPINGA ISRAEL*

* NGUVU ZA MAPINGAMIZI KUONGEZEKA KUTOKANA NA MUDA MCHACHE WA SHETANI ALIOBAKIZA KUFANYA KAZI DUNIANI*

* NINI WAJIBU WETU WA KUFANYA BAADA YA YOTE❓*

*1⃣ UTANGULIZI*

✍ Tukumbuke kuwa Mara baada ya Rais Donald Trump Kutangaza Kuutambua Mji wa Yerusalemu kama Makao Makuu ya Israel,Lakini hata Israel walikuwa na Sababu ya Kuhamisha makao yao Makuu Kutoka Telhaviv Kwenda Yerusalemu kwasabbu mambo mengi ya Muhimu Yapo Yerusalem Kama
i) Bunge la Israel lipo Yerusalem
ii)Makao ya Viongozi wa juu wa nchi yapo Yerusalemu
iii)Ofisi nyingi aa kiserikali zipo Yerusalem

Kwahiyo imekuwa ni makao yao makuu tangu mwaka 1950 kisheria yao,Lakini kusimama kutangaza ndio ilikuwa ni shughuli kubwa na ngumu ambayo ndiyo imetekelezwa na Taifa la Marekani.Ndio maana umeona Roho ya mpinga Kristo imesimama kwa nguvu kubwa,wote wenye roho hii ndio hawa wanapiga kelele kwasababu shetani ameshuka akiwa na ghadhabu nyingi akiwa anajua wakati wake upo karibu

Tukishakuyaelewa hawa tuendelee mbele na ikiwa hukufuatilia masomo yaliyopita basi wasiliana nami kwa namba nilizoandika mwishoni chini,Nitakupatia kuanzia mwanzo mpaka tulipofika

*2⃣ VIASHIRIA VYA KUBOMOLEWA KWA MSIKITI WA AL-AQSA(DOME OF THE ROCK)*

Kutangazwa kwa Yerusalem kama Makao yao makuu ya Israel,Kumeanza Kuonyesha viashiria vikubwa vya kuanza Kubomolewa kwa ule *Msikiti wa Dom of the Rock* Maana ndipo kulipokuwepo lile hekalu la Suleiman lililobomolewa kabla ya Israel kutawanywa kwenda kila kona duniani

Kumbuka Shauku yao Kubwa Israel si tu ilikuwa Kuipata Yerusalem yao bali hasa walitamani Kurudisha hekalu lao lililobomolewa mahali pale pale ulipokuwepo huu msikiti wa Al-aqsa,Hivyo Hilo Hekalu la 3 Suleiman lazima lijengwe tena hapo hapo

Maandiko yanasema Chukizo la Uharibifu litakaposimama hapo patakatifu (Chukizo la uhatibifu ni Mpinga Kristo) yaani atasimama hapo kulipo na hekalu.

Kwanini nasema viashiria vya kubomolewa huu msikiti upo tayari kuonekana ni kwasababu hivi tunavyozungumza Kwa Miaka mingi Vifaa vyote vya Ujenzi wa Hekalu vimekwishaandaliwa na vimeandaliwa kila kitu kuhusiana na hekalu hilo ambalo lazima lijengwe ndipo chukizo la uharibifu linalotajwa ambalo alizungumza Yesu Kristo alipokuwa anazungumza juu ya kuja kwake katika *MATHAYO 24:15-21* Aliulizwa juu dalili ya kuja kwake na ya mwisho wa Dunia *MATHAYO 24:1-3* Aliwaeleza kuwa hekalu kuwa litabomolewa

Dhiki kubwa inakuja baada ya kunyakuliwa kwa kanisa na huyu mpinga Kristo ndipo anatajwa atasimama kwenye hekalu hilo ambalo litajengwa baada ya huo msikiti wao wa Al-aqsa kubomolewa

Vifaa vyote vilishaandaliwa kabisa na Israel wameandaa kila kitu kama ilivyokuwa nyakati za suleiman,Zaidi sana wameandaa mpaka Mavazi ya Makuhani yote yapo tayari.
Na Jengo lile ujenzi wake sio kama tunavyojenga hivi sas kwa ujenzi aa kawaida,hivyo ingechukua Miaka Mingi kukamilika bali wameandaa kwa kutumia Technologia za kisasa kabisa yaani ile filimbi itakapolia,Ni kuta zinainuka,zinainuka,zinaungwa na kuungwa Kama unaunganisha vyuma,Ni kitu kinasimama tu kufumba na kufumbua kila kitu kipo mahali pale

Yaani sasa inangojea tu filimbi(Tangazo) na hichi ni kishiria kikubwa kwasababu huwa wanapata nguvu kuwa hapo ni kwao,hivyo wanaona pakishakuwa ni makao yao makuu basi wana haki ya kujua mji huu wanaufanyeje?Ndio maana unaona hawa wengine wanapiga kelele,Ndio maaana Palestina ndio wanaosema hii Yerusalem Mashariki ndio makao makuu ya nchi yao,itakayokuja‼

3⃣ ONYO KWA KWA WAKRISTO KUSHABIKIA KUPINGA ISRAEL

Sasa unapoona Tangazo la Mji wa Yerusalemu kutambuliwa kama makao makuu na Ikiwa wewe ni Mkristo ambaye unajua Neno,Unajua kuhesabu Miaka,Unajua Kusoma vitabu na kuhesabu miaka hupaswi kuwa upande wa mashetani bali utakuwa upande wa Israel(Katika unabii kuwa upande wa Israel ni kuwa Upande wa Mungu).Ukiibariki Taifa la Israel na wewe utabarikiwa,Iombee Amani Yerusalemu

Hivyo na wewe ukikurupuka na kuchukuliwa na na micoment ya watanzania ambao hawajui kupambanua kipi cha Mungu na kipi cha Shetani ambao hao hao ndio waliweza Kuchukuliwa na Babu wa Loliondo na kudai ni Mungu basi nawe utakuwa upotevuni maana siku zote wanashabikia vitu vya upande wa pili vya kishetani

Lakini hapa ndio tujue Miaka 70 imefika tayari ya taifa la Israel(14/5/2018) Asomaye na afahamu kuhesabu miaka na kujua jinsi tulivyo karibu kiasi gani na hili Chukizo la Uharibifu(Mpinga Kristo) ambaye atasimama muda si mrefu kwenye hekalu hilo litakalojengwa baada ya Msikiti kubomolewa

Unaweza kuona mbele yetu ni muda gani upo❓ Ni Muda mfupi sana ndugu yangu

Hakuna ajuaye siku wala saa lakini ni muda mfupi hapa,Chukizo la uharibifu litasimama katika hekalu ambalo maandalizi ya ujenzi wake upo tayari ndipo dhiki kuu inakuwepo, Na Kumbuka dhiki kuu ikiwepo ujue kanisa limekwisha nyakuliwa

⚠ Kwa hivyo chochote cha kufanya yote haya kutimia, kitakuwa na Upinzani sana,kutakuwa na matukio mazito mazito ya kupinga Tangazo hilo na mengineyo mengi Kama haya Maandamano ya Palestina ambayo yaliyokuwa yanaendelea mpaka sasa

4⃣ NGUVU ZA MAPINGAMIZI KUONGEZEKA KUTOKANA NA MUDA MCHACHE WA SHETANI ALIOBAKIZA KUFANYA KAZI DUNIANI

Kuanzia sasa na kuendelea tutaanza kuona matukio mengi ya Mapingamizi na kelele nyingi kutoka kila kona dhidi ya maamuzi hayo Kwasababu Shetani anajua Muda wake si mwingi kwasababu dhiki kuu ni Miaka 7,Na dhiki kuu ikiisha kanisa lililonyakuliwa na Yesu linakuja duniani na Yesu anatua kwenye mlima mzeituni mahali pale pale alipopaa wakati anaenda mbinguni, akiwa na Jeshi la watakatifu walionyakuliwa ambapo kutatokea vita inayoitwa *VITA VYA HARMAGEDONI* na baadae Utawala wa miaka 1000 wa Yesu Kristo dunia *(Ikiwa haujapata mfululizo huu matukio haya ya siku za Mwisho pia unaweza kuwasiliana nami nitakupatia)*

Wakati huo wa miaka 1000,Shetani atakuwa amekamatwa na kufungwa kwa miaka hiyo hiyo 1000.Hivyo ile tu Kanisa linanyakuliwa kuna miaka 7 tu ya dhiki kuu,Na baada ya hapo shetani anakamatwa kufungwa miaka 1000

Hivyo Shetanj anajua haya,Anajua viashiria vyake kwa hiyo anapoona hatua hii inaanza na hii nyingine inaanza, kadiri inavyosogelea ni mapambano, ni vita vikali utaona dunia lote linakuja kwa nguvu zote,huwezi kutegeme kuona *Jumuiya ya nchi za ulaya* ikisapoti hili wakati hicho kinachofanyika ni cha kiMungu
Kumbuka hata hizo sarafu za Euro zina michoro ya 6⃣6⃣6⃣ zimewekwa pale,Na Jengo lao zima lina mavitu ya ajabu ajabu hivyo huwezi kutarajia sapoti ya jambo hili kuunga mkono kutambuliwa kwa Mji wa Yerusalem

Kinyume chake ndio utaona Mapambano na Maneno mengi ya kupinga uamuzi huo uliofanywa na Rais wa Marekani,Kwahiyo na wewe Ukiwa Upande huo wewe ni Mjinga,Hujui Neno wala hujui Wewe ni Nani❓Hujui hata kilichopo mbele yetu lakini unachukuliwa na siasa za wajinga katika nchi yetu na dunia kwa ujumla

5⃣ NINI WAJIBU WETU WA KUFANYA BAADA YA YOTE❓

Kwasababu hii tuukomboe wakati kwasababu tujue hatuna muda mwingi unaotusubiria,Kama hujafa basi siku ya mwisho kwa watu wote nayo haipo mbali *(Sisemi kuwa Yesu anarudi lini kwamba ni kesho au kesho kutwa bali ni bado kitambo kidogo Yeye hajae atakuja wala hatakawia)*

Sasa itakukuta Umefanya kazi gani ya Mungu❓ Tangu umeokolewa hutaki kujihusisha na kuwaleta watu kwa Yesu unadhani kazi hiyo ni ya Mchungaji wako au wainjilisti fulani❓ Unategemea kwenda kufanya kazi ya Mungu kanisani bali unachukuliwa na shughuli za dunia hii‼ .Itakushangaza Yesu atarudi atakuacha Ukiwaza kufanya mambo mengi ya kidunia bila kuwaza na kufanya kazi ya Mungu

Au Je itakukuta upo Safi kwenye maisha ya Utakatifu au Unachanganya masomo tu(Vuguvugu)❓ Je itakukuta unaliishi Neno hili hili❓ Maana ni Kanisa Takatifu tu ndiolitakalonyakuliwa *WAEFESO 5:25-27*

Ndugu yangu wewe ndio unayafahamu Maisha yako ya sirini,Ni kweli inawezekana unasali kanisani na unafanya hata huduma lakini maisha unayoishi unayajua sio ya usafi‼ Maisha yako yamejaa unafki,Unafanya dhambi sirini kwa makusudi eti unasema unatubu kimya kimya‼ Ndio maana maisha yako yapo vile vile hauoni tena ile furaha ya wokovu,Amani imepotea kabisa wala hufurahii Neno kama Mwanzo,Unaenda kanisani kama desturi na mazoea‼ Na Kwambia ndugu yangu hivyo ulivyo unaenda Motoni kama hujashtuka Ukaamua Kugeuka Leo na kuanza Upya Yesu anakuja kutunyakua ila wewe utaachwa kama utaendelea na maisha haya uliyo nayo ambayo umeshayazoe

Ndugu yangu na wewe ambaye unasoma Ujumbe huu ambaye bado hujaokolewa au unajiita umeokolewa ila hauna badiliko la kweli la maisha,Kila siku unatubu ila upo vile vile,Unajikuta lile usilopenda kulufanya ndilo unalifanya na unalopenda kulifanya ndio hulifanyi‼Yaamkini unatamani Kumpendeza Mungu ila unashindwa unajikuta unaendelea katika dhambi‼ Unajifahamu wewe ni Mwenye dhambi wala unafki ndani yako,huu si wakati wa kujihesabia haki kwa dini zetu eti mimi dini Fulani,Yesu haji kunyakua dhehebu fulani au dini fulani bali anakuja kulinyakua kanisa takatifu❓ Je wewe ni Mtakatifu❓Huu ndio wakati wa Kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha nawe utapewa uwezo wa kushinda dhambi na kusamehewa dhambi zako zote na utakuwa sehemu ya watakaonyakuliwa

Je Wewe nawe ni Miongoni mwa wale waliokuwa wanampenda Mungu hapo mwanzo ila ilifika siku wakaanguka na kuacha wokovu na sasa upo mbali,unaishi maisha kama mtu asiyemjua Mungu❓ Sasa kwa somo hili Mungu amelileta kwako ili nawe usiachwe!Wewe ni mteule wa Mungu!Ni kweli shetani atataka kuwapoteza hata yamkini walio wateule ila hataweza kwakuwa watu kama ninyi ni wepesi kuisikia sauti ya Mchungaji wenu Yesu Kristo anapowaita.Kwa Ujumbe huu Mungu anakuita urudi kundini,Utubu nae atakupokea nawe utakuwa miongoni mwa watakaonyakuliwa muda mfupi Yesu akija‼ Ebu kumbuka ulipoanguka ukatubu,ukumbuke upendo wako wa mwanzo

▶Hivyo huu si wakati wa kuchanganya masomo,Lazima ujue viashiria hivi vinatupa kujua muda uliopo mbele yetu ni mfupi sana hatujui siku wala saa ila hatuna muda mrefu,Kinachowezekana kufanyika leo kisingoje kesho hivyo ikiwa unahitaji Msaada wowote Kati ya mambo niliyo yataja Ikiwa hujaokoka na unahitaji Uwezo huo wa kushinda dhambi na kukoka basi utawasiliana nami ,Vivyo hivyo ikiwa ulirudi nyuma na kuacha wokovu vile vile unaweza kuwasiliana nami kwa ushauri zaidi na maombezi ili tumalize safari kwa nguvu maana Mungu anaangalia umaliziaji si uanzaji

▶ Ikiwa Umeokolewa hakikisha unatafuta kanisa linalohubiri wokovu na kufundisha mafundisho ya utakatifu na wokovu kama hivi iki uzidi kuukulia wokovu na ujitambukishe hapo Kuwa umeokoka ila kama utahitaji Ushauri pia utawasiliana kwa namba zangu hapa chini

Mpaka kufikia hapa tumefikia Mwisho wa Mfululizo wetu wa masomo yanayohusiana na kutambukiwa kwa Yerusalem kama Makao makuu ya Israel,Natumai umejifunza Mengi mpaka kufikia hapa basi usiache kushare na kuwasaidia wengine ndani na nje ya kanisa ili nao wawe miongoni mwa watu watakaonyakuliwa siku ike Yesu akiwwa Mawinguni.Mungu akubariki kwa kufuatilia na ikiwa una swali au ushauri au lolote usisite kuwasiliana nami

*♨ Kwa mawasiliano zaidi,Ushauri au Maswali*
* Na: Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
www.facebook.com/charles.mwaisemba?__nodl
_stmwaisembac@gmail.com_
 
MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL

✳ SOMO 3⃣ : MAREKANI KUPITISHA SHERIA YA KUITAMBUA YERUSALEMU✳

Na: Shujaa Charles Mwaisemba

VITA YA ISRAEL KUTEKA YERUSALEMU MASHARIKI
BUNGE LA MAREKANI KUPITISHA SHERIA YA KUITAMBUA YERUSALEMU
UTOFAUTI WA TRUMP NA MARAIS WA MAREKANI WALIOMTANGULIA

1⃣ UTANGULIZI

Kama tulivyokwisha kuona katika somo lililotangulia jinsi Bunge la Israel lilivyopitisha sheria juu ya Jiji laYerusalemu kuwa ndio makao yao makuu na kudai Yerusalemu Yote isiyoweza kugawanyika yaani Yerusalem mashariki na Yerusalemu Magharibi.Leo tutaendelea kutokea hapo ikiwa hukuweza kufuatilia mfululizo uliopita ili kuweza kuelewa zaidi yaliyo mbele yetu basi utawasiliana nami kwa Namba hapo chini ili nikupatie mfululizo uliopita.

*2⃣ VITA YA ISRAEL KUTEKA YERUSALEMU MASHARIKI*

Mara baada ya ile sheria kupitishwa kwenye bunge la Israel kulianza kufanyika jitihada nyingi za kuanza kutaka kurudisha Baadhi ya maeneo yao ambayo tulieleza yalikuwa yanakaliwa na Waarabu wapalestina na wengineo hasa Yerusalemu Mashariki

Lakini ilipofika mwaka 1967 Kulitokea vita vikali ambavyo ni vya siku 6 tu ambapo Israel ilipambana na waarabu combine (Palestina,Syria,Urusi n.k) ambao wameizunguka pande zote ila kwa ajabu sana Kataifa hako Kadogo kamoja kaliwapiga vikali na kuwasambaratisha vikali na wakateka Yerusalemu Mashariki pia ikawa mikononi mwao

Hivyo sasa wao wakahesabu Yerusalemu yote sasa ni kwao yaani Yerusalemu Magharibi na Yerusalemu Mashariki,Lakini dunia karibu yote ikawa inawahesabu kama wavamizi na miaka yote hiyo kumekuwepo na ushindani mkubwa katika eneo hilo na ndio chanzo cha Mgogoro huu Mkubwa kati ya Palestina na Israel.

Wapalestina wakidai Eneo lao na waisrael wakidai ni Eneo lao(Nitaeleza kwa Kina kwenye Somo jingine *NANI NI MMILIKI HALALI WA ENEO HILO?KATI YA PALESTINA NA ISRAEL❓*).Ila kwa ufupi kama Wanafunzi wa Biblia hatuna budi kuele
wa *WAPALESTINA NI AKINA NANI❓*

WAPALESTINA ni Wafilisti Kibiblia(Philistine)!Maanake wale wakina Goriathi wale ndio wapalestina wenyewe.Wale hawajawai kuwa Israel.Ukiangalia Biblia yako huwaoni wakina Goliathi kama wamiliki halali wa Israel(Haikuwa nchi yao).Kwahiyo tangu wakati ule ilikuwa ni shida sana baina ya waisrali na wapalestina

3⃣ BUNGE LA MAREKANI KUPITISHA SHERIA YA KUITAMBUA YERUSALEMU

Baada ya Muda mrefu na Mgogoro huu wa Wapalestina na Israel kuzidi kuwa gumzo kwa ulimwengu wote juu ya umiliki wa Ardhi na hasa jijila Yerusalem.Taifa kama La marekani limemekuwa likikaa chini kujadili na kutafuta kwa kusoma vitabu historia juu ya jiji la Yerusalem na nchi hii kwa mipaka yake na Kugundua kuwa Yerusalemu ni Mji wa Israel tangu awali ulikuwa ukijulikana kama *MJI WA DAUDI 2 SAMWELI 5:4-9*

Hivyo ilipofika Mwaka 1995,Bunge la Marekani likaleta hoja hii bungeni na kuijadili kisheria Ikiwa kama Yerusalemu ni makao makuu ya israel au la❓Lakini baada ya mjadala huo wote,Bunge lote la marekani lifikia kufanya azimio la pamoja kwa kupitisha sheria ya Kuitambua *YERUSALEMU KAMA MJI MKUU WA ISRAEL* kw sheria kwa kura nyingi sana za bunge

Lakini pamoja na Kupitishwakwa sheria hiyo tangu mwaka 1995,ila utelelezaji wakendio ulikuwa ni shida sana kwasababu ulikuwa na vitisho vya kila namna kutoka kila kona kila mahali kwamba Marekani wakitangaza tu rasmi kwamba wanaitambua Yerusalemu kama Makao makuu ya Israel basi itapelekea machafuko makubwa sana duniani .Kumbuka Marekani walipitisha Sheria kuwa Yerusalemu ni Mji usiogawanyika yaani Yerusalem Masharikona Yerusalemu Magharibi zote ni Yerusalem iliyo chini ya Israel)

Ukizingatia Ndani ya Yerusalemu Masshariki ndio kuna Msikiti mkubwa unaoitwa MSIKITI WA ALAQSA(DOME OF THE ROCK) mahali ambapo waislamu wote kote duniani wanapahesabu kama sehemu pa 2 pa utakatifu baada ya Macca

Kwahiyo ilikuwa ni mgogoro mkubwa kwa marekani kutangaza hiyo juu ya sheria waliyoipitisha.Bunge lote la Marekani wamekuwa wakitamani hivyo kwa miaka tangu wakati huo kuona utekelezaji wa Sheria hiyo ya kuitambua Yerusalemu kama Mji mkuu wa israel ukitimizwa na maraisa waliokuwa wakiingia madarakani

Marais wote waliokuwepo tangu wakati uke,Walikuwa wanapigia debe ahadi hiyo kuitekeleza lakini,Nani mwenye ubavu wa kutangaza hivyo❓ Kwa kuwaza chuki atakayoipata dunia yote,kwasababu kila kilichokuwa kinagusiwa ilionyesha ilikuwa ni hali tete

Kwahiyo Marais tangu nyakati zile za kina Bill Clinton, George W Bush, Barack Obama wote hawa utaona ukiingia Youtube,utaona hotuba zao za za kampeni zote walikuwa hasa wanasisitiza kuwa wataitambua Yerusalemu kama Makao Makuu ya Israel.Walitamka hivyo marais hao wote niliowataja ili kupata kura za wengi katika Maeneo yale ya waktisto wengi marekani ambapo wengi ni Wapentekoste ,lakini utekelezaji wake ndio ulikuwa mgumu

Kwahiyo walikuwa wanahairisha utekelezaji wake kila baada ya miezi 6,Na wamekuwa wakifanya hivyo tangu wakati ule

4⃣ UTOFAUTI WA DONALD TRUMP NA MARAIS WALIOMTANGULIA

AHADI YA TRUMP YA UTEKELZAJI WA SHERIA ILE KWA WAMAREKANI NA WAYAHUDI

Rais wa Marekani, Donald Trump tangu awali katika Kampeni zake zote vile vile akaahidi kwa uzito mkubwa na nguvu kubwa akasema Sasa hilo ambalo limewashinda wengine wote,Yeye atalifanya na hatajali Ushindani wowote utakalojitokeza,Akazidi kuwahakikishia Israel kwamba hilo atalifanya bila uoga wowote

HESHIMA YA WAYAHUDI NCHINI MAREKANI KWA AHADI HIYO

Kwa Muda mrefu wayahudi waliopo nchi marekani wamekuwa wakiheshimika sana sana hivyo ahadi ile ilikuwa pia inawalenga wayahudi wote waliopo Nchini marekani.Kwahiyo israel wote wakawa wanasubiri alivyoingia Trump madarakani mwanzoni mwa mwaka 2017 Kama sheria ilivyo ikifika miezi 6 inabidi tena kuhaitisha utekelezaji wake (mpaka wakati huo msimamo wa bunge ulikuwa nu ule ule)Kwasababu ukipinga tu msimamo wa Bunge itakuwa vigumu kupata kura kwa Wakristo wa wamarekani

Kumbuka Marekani kuna wayahudi wengi sana na wayahudi kwa watu wanaowafahamu kuwa kote duniani ni watu wenye akili kupindukia,Ni watu ambao wamebarikiwa kwa ajabu sana.

▶Wanasayansi wengi wakubwa unaowasikia wamefanya mambo ya uvumbuzi wa vitu vingi huko marekani ni Waisrael.

▶Madakrari bingwa wakubwa sana na maalumu hi waisrael

▶Watu wengi kwenye fani nyingi marekani ni wanaisrael

Kwahiyo ni watu wanaoheshimika sana sio tu Maraekani bali nchi nyingi sana kama sweden Kwa mfano wametengewa sehemu au eneo maalum kwa waisrael pekee na kupewa mazingifa mazuri kuliko hata raia wenyewe kwasababu ya uwezo wao na akili zao za ubunifu ambayo huwezi kuyaona kwa mtu mwingine wa kawaida kuweza kuyabuni kwa jinsi ambavyo wamebarikiwa na Mungu n.k.Wamepewa ulinzi kwa namna isiyo ya kawaida kwa mataifa mengi hata kule ulaya

Kwahiyo Bunge la marekani likikuwa haliwezi pia kusimama kinyume na Israel kwa gharama yoyote ila tatizo ndio ilikuwa ni nani atangaze?Kwasababu kutangaza hivyo ni kama Kutangaza vita duniani kote

Hivyo hata kwa Trump alivyoingia kukawa na uzito fulani ingawa alikjwa amedhamiria tangu mwanzo lakini hivyo hivyo kutoka kila kona,kila mahali wakamwambia tu ukithubutu kufanya hivyo utakuwa umetangaza machafuko katika dunia yote.Na ilivyopita miezi 6 nae vile vile akahairisha utekelezaji wake ile sheria ya mwaka 1995 mara ya kwanza

Lakini hatimaye ndiye alikuwa Rais wa Kwanza na wakipekee kuweza kutangaza jambo hilo ambalo lilisisimua duni.Usikose kufuatilia somo linalofuata Ambalo nitakueleza nini kilifanyika kabla ya kutangaza huku alikokufanya na kilichompa nguvu zaidi ya kutangaza tofauti na Marais wenzake wote waliopita❓ Usikose kufuatilia Sehemu ijayo ya mfululizo huu ambapo pia nitakueleza Maana ya70 Kibiblia inavyohusishwa na nyakati za Mwisho

Nashukuru kwa kufuatilia mpaka hapo,Unaweza kushare ujumbe huu kwa magroup mengine na watu wengine.ila Pia ikiwa unahitaji ushauri!una maswali Au unahitaji Kuokoka kutokana na Haya uliyoyafuatilia na unaamua Kutaka kuacha dhambi.Basi wasiliana nami kwa namba hizo hapo chini nami nitakuombe utaoewa uwezo wa kushinda Dhambi

MUNGU AKUBARIKI

♨Kwa mawasiliano zaidi
Na:Shujaa Charles Mwaisemba
0712054498/0759420202
_stmwaisembac@gmail.com_
 
*MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳ SOMO 2⃣: UMOJA WA MATAIFA KULITAMBUA TAIFA LA ISRAEL KWA KURA✳*

* Na: Shujaa Charles Mwaisemba*

*▶KUREJESHWA TENA KWA TAIFA LA ISRAEL

*▶KURA YA UMOJA WA MATAIFA JUU TAIFA LA ISRAEL
*▶KURA YA BUNGE LA ISRAEL JUU YA JIJI LA YERUSALEMU*

*1⃣ UTANGULIZI*

✍Kama tulivyokwisha kuona jinsi Taifa la Israel lilivyobomolewa kama Yesu alivyosema na Hekalu kubomolewa,Basi leo tena tunaendelea kuangalia mambo mengine kadhaa yaliyoendelea mpaka kupelekea Kurudi tena kwa Taifa la Israel kama Taifa kamili. Ikiwa hujapata somo la 1⃣ la mfululizo huu hakikisha unawasiliana nami ili kuweza kuendelea kuelewa mwendelezo wa matukio yaliyofuata.

2⃣ KUREJESHWA TENA KWA TAIFA LA ISRAEL

Kama tulivyotangulia kusema Mungu alikwisha sema kuwa Israel itatawanywa kona zote za dunia pale ilipomfanya Bwana Dhambi ndivyo hivyo hivyo Bwana ndiye aliyesema pia atalirudisha tena Taifa lake na kuwa Taifa kamili kwa wakati wake.

Hivyo tuliona jinsi Israel walivyofukuzwa na Kwenda kila kona na wakazaliana sana vizazi kwa vizazi vilipita lakini Mungu aliposema atawatawanya alitoa ahadi kuwa Siku za mwisho zitakuja ambayo atawakusanya tena na kurudisha katika nchi yao

*♨{EZEKIELI 36:24}*
_"Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami *nitawakusanya* na kuwatoa katika nchi zote, na *kuwarudisha* katika nchi yenu wenyewe."_

Na moja kati ya kiashiria kimoja kikubwa cha siku za mwisho ni Kurudi kwa Taifa la Israel kwa Muujiza Mkubwa,Jambo lililoshangaza dunia.

Mwishoni mwa karne ya 19 kulitokea jambo la ajabu miongoni wa Wayahudi walikuwa wametawanyika duniani kote, ingawa hawakuwa na na mawasiliano kati yao lakini roho fulani ikamwagwa juu yao
Ingawa walikuwa duniani kote lakini utamaduni wao haukubadilika.Wazazi walikuwa wanawahadithia watoto wao na watoto wao wanawahadithia watoto wao toka kizazi kimoja mpaka kingine juu ya ahadi ya Mungu ya kuwarejesha na kuwapa Kaanani kuimiliki

*♨{ ZABURI 78:1-11}*
_"............................Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia.Hayo hatutawaficha wana wao, Huku *tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za BWANA, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya*.Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao,............................Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao.............................Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.................."_

Hivyo kwa muda wote waliokaa pande zote watoto walikuwa wamewafundishwa na kukumbushwa juu ya ahadi za Bwana.
Walikuwa wakiteswa na kuuliwa sana wakiwa nchi za jirani pande zote za dunia lakini bado walijua watarudi kwenye nchi yao.
Mwishoni mwa karne ya 19,baada ya miaka karibu 1800 Yerusalemu ilipobomolewa,Ndipo ilipomwagwa roho juu ya wana Israel(Wayahudi) wote kutoka pande zote walipo kila mmoja wakaaanza kupata mawazo ya kubuni na namna ya kurudi bila mawasiliano na wale wa upande mwingine

Kulitokea kitu kinachoitwa *ZIONIST MOVEMENT* juu ya wayahudi ambacho ndicho kilianza kuhamasisha wayahudi kurudi tena kwenye nchi yao na kuyachukia makazi waliyokuwa waishi katika pande zote za dunia bali wakaanza kurudi kwa Kasi kubwa sana

*3⃣ KURA YA UMOJA WA MATAIFA JUU YA TAIFA LA ISRAEL*

✍ Vuguvugu la hilo la wanaisrael lilipoendelea kwa nguvu kurudi kwenye Nchi yao ambayo wakati huo ilikuwa chini ya utawala wa waingeleza,Mwaka 1947 ndipo Umoja wa mataifa ilipigwa kura ambayo ndiyo ilikuwa mwanzo wa Taifa la Israel kutambulika mwakani baadae

✍Tarehe 29 Nov 1947 ndipo kulifanyika kura katika UMOJA WA MATAIFA ambao ulijadili juu ya makazi hayo ya Eneo hilo la Israel ambalo yalikuja na kufanya Mwaka uliofuata Taifa la Israel kuja kuwa Taifa Kamili

✍ Tarehe 14 May 1948 ndipo Israel wakatangaza kuwa ni Taifa na Kuitwa tena *TAIFA LA ISRAEL* kama lilivyokuwa mwanzo baada ya miaka 1800 toka mwaka 135 B.K

✍Jambo hili la Taifa la Israel kutangazwa kuwa kama Taifa halikukubalika na mataifa mengi ya wakati huokama ilivyolewa wanavyopinga haya Lakini siku ile ile 14/5/194 walivyotangazwa kama Taifa,Rais wa Taifa la Marekani wakati huo, *RAIS HARRY TRUMAN* ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza nae kusimama kusema analitambua Taifa la Israel

✍Ingawa nchi nyingi hazikukubaliana na kuafikiana na Rais huyo wa Marekani kwa Uamuzi alioufanya wa kuitambua Israel kama Taifa Lakini Israel wakapata Nguvu sana,Na baadae mataifa mengi nayo yakaanza kuwatambua kama Taifa Kamili.

*4⃣ KURA YA BUNGE LA ISRAEL JUU YA JIJI LA YERUSALEM*

Lakini Mwaka 1950,Kumbuka wamekwend katika nchi mbalimbali duniani na hivyo wamerudi wakiwa na Mfumo wa Kidemocrasia wameuleta sasa katika nchi yao ya Israel.Hivyo mara baada ya Taifa lao kutambuliwa ndipo walipoweka mfumo wa kiserikali ambao ulikuwa na Bunge ambalo linaitwa *KNESSET*

Kwa mara ya kwanza Bunge la Israel 23 January 1950 likatangaza tena bungeni baada ya kuwa wamepiga kura katika bunge lao na kura 62 kwa 2 (Matokeo ya kura za bunge la Israel)Wakakubaliana katika Bunge hilo kwa kura hizo kuanzia Tarehe hiyo Kwamba *YERUSALEM NDIO UTAKUWA MJI WAO MKUU WA ISRAEL*

Katika maazimio hayo wakasema itakuwa ni Yerusalemu isiyoweza Kugawanyika yaani Yerusalem nzima katika eneo lake lote ambayo inatajwa katika mipaka ya Yerusalemu kama ilivyo katika Maandiko
Swala hili pia lilipingwa vikali sana na mataifa mengi kwamba Yerusalem kuwa mji mkuu wa Israel tangu wakati ule.Wakati huo Israel walikuwa sehemu kubwa wapo katika Yerusalemu Magharibu na huku Yerusalemu Mashariki walikuwa wanakaa waarabu wa Aina mbalimbali

Usikose kufuatilia Somo la 3⃣ la mfululizo huu ambapo utajifunza mambo mengine mengi kuhusu vita vilivyofuata baadae vya israel na mataif yote ya waarabu na jinsi Marekani walivyopiga kura ya kuitambua Yerusalem.Kwa leo tuishie hapa

Ila Kuna mambo nataka tujifunze na tutafakari tunapohitimisha somo hili,Kwanza tumeona kumbe tangu Mwanzo kama ilivyo leo maamuzi yote yaliyokuwa Yanafanywa yalikuwa yanaonekana yanapigwa kwa nguvu na mataifa mengi lakini kwakuwa ni wakati wa Bwana hivyo kupinga kwao hakukuzuia Taifa la Israel kuanzishwa na kurudishwa kama Neno la Bwana linavyosema

Pia kwako wewe unayesoma Ujumbe huu,Mungu anataka akuambie kuwa Kama aliweza kuwatawanya Israel na sasa akawarudisha Na kuwa kama taifa na kuwapenda kama mwanzo,Basi hata wewe Mungu anakupenda anataka kukurudisha katika Imani majira haya ya mwisho mwisho wa dunia.

Yamkini ulikuwa unampenda san Mungu hapo mwanzo ila sasa Umerudi Nyuma,Umechoka,Unafanya mambo ya kidunia na kuishi maisha ya Uchafu kama mataifa,Huu ni wakati wa Bwana wa kuwarudisha tena walio wake Kabla Kristo Yesu hajarudi!Unaposoma Ujumbe huu Ikiwa ulirudi Nyuma na Kuacha wokovu au unaishi maisha ya Uvuguvugu,Nasema Na wewe kuwa *RUDI KWA BWANA,RUDI KWA BWANA,RUDI KWA BWANA*.Mungu bado anarehema na anakupenda ndio maaana kalileta somo hili kwako

Na Ikiwa Wewe unajifahamu hujaokoka,Huna uwezo wa kushinda dhambi,Unajitahidi kuacha dhambi fulani lakini unajikuta unarudi pale pale!Ni wakati wa kumaliza vizuri,Mungu anaangalia sana Umaliziaji wa mtu si uaanzaji!Ni kweli ulianza vibaya,ni kweli umefanya dhambi nyingi wewe unazijua lakini ikiwa utakubali Kutubu dhambi zako ,Mungu hatakumbuka dhambi zako zote ulizotenda,.Hata kama uliua au umefanya uasherati ana uzinzi sana,Hata kama ulitoa mimba n.k,Mungu atakupokea kama alivyowapokea Taifa la Israel

Hivyo ikiwa unahitaji msaada wowote wa kirohi kama Kukuombea upewe uwezo wa kushinda dhambi basi wasiliana na mimi kwa namba hiyo hapo chini,Nami nitakuombea na ikiwa umerudi nyuma au unatamani kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ila unajikuta unaanguka anguka basi pia wasiliana na mimi nitakushauri na kukuombea pia ili tumalize Safari hii pamoja!!

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

Kwa mawasiliano Zaidi
* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
* MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳SOMO LA 4⃣ : MAANA YA 70 KIBIBLIA KWA ISRAEL NA KANISA✳*

*Na: Shujaa Charles Mwaisemba*

* VIKAO VYA VIONGOZI WA DINI MAREKANI PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI NA BUNGE JUU WAKATI WA BWANA*
*MAANA YA 70 KIBIBLIA JUU YA ISRAEL NA KANISA*
*DONALD TRUMP KUTANGAZA RASMI KUUTAMBUA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*1⃣ UTANGULIZI*

Tuliona kwenye Sehemu iliyopita Kuwa hata Rais Donald Trump kwa mara ya kwanza nae alivyoingia madarakani jinsi kulivyokuwa na uzito mkubwa fulani kutoka kila kona duniani kuwa endapo angetangaza kungeweza kuleta machafuko hivyo kumpelekea nae baada ya mezi 6 kupita alihairisha utekelezaji wa ile sheria ya mwaka 1995 ya marekani kuutambua Yerusalem kama makao makuu ya Israel.Sasa leo tunaendelea kutokea hapo na ikiwa hujaanza na mimi tangu Somo la 1⃣ la mfululizo huu basi wasiliana nani nikupatie

*2⃣ VIKAO VYA VIONGOZI WA DINI MAREKANI PAMOJA NA VIONGOZI WA KISERIKALI NA BUNGE JUU YA WAKATI WA BWANA*

Baada ya Trump kushindwa kutangaza kwa mara ya Kwanza,Walijikusanya Viongozi wengi wa dini wanaoyaelewa maandiko Kuanzia mwezi 10,11 na 12 mwaka 2017 na kufanya vikao mbalimbali vya watu waliokuwa wanatafakari juu ya Neno la Mungu na wakati wa Mungu

Hivyo kuliendelea kuwepo na watu mbalimbali ambao walisukumwa kwa msukumo usiokuwa wa kawaida wa Roho mtakatifu, wakawa wanafanya vikao mbalimbali na kila mmoja kutoka huku na kule akawa anaingiziwa msukumo tofauti kabisa wa KiMungu ndani yake kwamba ni kweli hapa katikati tangu mwaka 1995 jambo hili halijawezekana kwasababu wakati wake ulikuwa bado lakini sasa mwaka 2017 huu ndio Wakati wa Bwana umefika kwasababu ni *MIAKA 70* imetimia baada ya mwaka 1947 kwenye ile kura ya Mwanzo ya Umoja wa Mataifa ambayo ndiyo iliyosababisha Kuwako kwa Taifa la Israel mwaka uliofuata

Hivyo wakawepo wanazuoni,wakawepo watu ambao wanachambua maandiko,Wakawepo wale watu wanaotoka huku na huku wakamkarisha chini Rais wa sasa wa Marekani, *Donald Trump* na viongozi kadhaa wa serikali na Viongozi wa Bunge na kuanza kuchambua kuhusu 70

⚠Hata Kanisa la Mungu tunatakiwa tuifahau 70 katika mpango wa Mungu......

*3⃣ MAANA YA 70 KIBIBLIA JUU YA ISRAEL NA KANISA*

Sasa Sabini(70) katika Israel ina kitu kikubwa sana katika mpango wa Mungu..Na Vile Vile *Sabini(70)* Inazungumzia juu ya *NYAKATI ZA MWISHO ZA KUMALIZIA*

Ndio maana ni vyema Kulifahamu hili nyakati zote,Maana Mungu amekuwa akisema na Kanisa lake kwanza kabla ya kutokea kwa wengine

Hivyo lile kusanyiko lililowaita Viongozi wa kiserikali na Viongozi wa Bunge la Marekani pamoja na Rais wakitafakari wakati wa Bwana ndio ikaja Kwamba Mwaka 2017 ni Mwaka wa 70 baada ya ile Kura ya Mwaka 1947 na ikaja habari ya Mwaka wa 70 kuhusiana na Israel(Jubilee ya miaka 70),kuhusiana na Wakati wa Bwana

*♨{ YEREMIA 25 :11-12}*
_"Na nchi hii yote pia *itakuwa ukiwa*, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli *miaka sabini(70)*.Na itakuwa miaka hiyo *sabini(70) itakapotimia*, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, nayo nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele."_

*♨{YEREMIA 29:10-11}*
_"Maana BWANA asema hivi, Babeli *utakapotimiziwa miaka sabini*, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa *kuwarudisha mahali hapa*.Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini *siku zenu za mwisho*."_

Mwaka wa 70 katika mpango wa Mungu na hususani kwa Israel na hususani kwa Kanisa lake ambalo tunasimama kama Israel ina maana kubwa sana ikizungumziwa na kuhusishwa na siku za Mwisho kama tulivyoona na siku za Mwisho
*Maana ya 70 inatupa tafsiri tatu za kibilia*

*1) Ni mwaka wa Kutimiza Neno lake la kuwajiria Watu wake au Kurudi kwake kuwaokoa na kuwasaidia Watu wake*.Utaona Sehemu Nyingi ambapo biblia inataja 70 juu ahadi ya Mungu kutimizwa kwa watu wake.Na Kwa kanisa Ahadi kuu tunayoisubilia ambayo Mungu alituahidi watakatifu ni kuja kwa Yesu kulinyakua Kanisa lake.Hivyo Neno hilo nalo litatimizwa Kama alivyosema

*2) Ni Mwaka wa Kurudisha Walio wake*.
Kipindi hichi kutakuwepo na wimbi la watu wengie Kumrudia Mungu kwa toba,Waliokuwa wamerudi Nyuma wataanza tena kusikia Sauti fulani ya Roho mtakatifu ikiwakumbusha juu ya Toba(Usiipuuze sauti hiyo).Ni mwaka Ambao Hata wengi ambao hawajaokoka wataokolewa kwa wingi wake .Hata wale wateule Shetani aliotaka kuwapoteza zaidi watarudi tena kwenye njia na wataisikia sauti ya Bwana wao

*3) Ni mwaka wa Mawazo mema ya Mungu kwa Watu wake Na kanisa lake YEREMIA 29:10-11*.

Utaona Mwaka huu wa 70 unazungumziwa pamoja na Siku za Mwisho

*♨{DANIELI 9:1-2}*
_" .................katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danieli, *kwa kuvisoma vitabu,* nalifahamu *hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii*, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, *miaka sabini.*

Utaona Daniel hapa,hìi yote mpaka mwisho anazungumzia juu ya siku za Mwisho,Mfano *(DANIELI 12:9)*

Kwahiyo Sabini,Sabini ,sabini,Sabini kwa habari ya Israel inazungumzia vilevile juu ya Nyakati za Mwisho juu ya Kanisa wa majira haya tuliyo nayo

*4⃣ RAIS WA MAREKANI,DONALD TRUMP KUTANGAZA RASMI KUUTAMBUA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

Ndipo Katika kikao kile baada ya Trump Kukaa nao,Roho alishuka kwa namna ya ajabu sana ikajulikana ilikuwa Mwaka 1947 kura ile ya Umoja wa mataifa ilipigwa na Mwaka 2017,Miaka sabini(70) ilitimia wakati umefika wa kutangaza Kulitambua mji wa Yerusalem kama makao makuu

Na ni tangazo linalotolewa mwaka wa 70 lakini kumbuka linatolewa katika mwaka 70 katika nchi ile ile ambayo Umoja wa mataifa una Makao makuu (Marekani)
Lakini zaidi sana Tangazo la Kuutambua Yerusalemu kuwa Makao makuu ya Israel liliyolewa vilevile Muda mfupi kabla ya Jubilee ya Miaka 70 ya Israel ya Israel ambayo imefanyika 14/5/2018 mwaka huu.

Sabato ya Miaka 70,mwaka huu 2018 tarehe 14/5/2018 taifa hili la Israel linakuwa limetimiza Miaka 70 ya kuwapo kwake tangu lilipotangazwa kuwepo 14/5/1948(Sabato ya Miaka 70) ambayo inaashiria kitu kingine Kikubwa na ni Mwanzo wa kuyaona Mengi ya KiMungu na kinabii juu ya dalili za kuja kwake Kristo yakitimia kwa haraka sana

Kabla ya wakati ule mwaka wa 70 katika nchi ile Tangazo linatolewa *TUNAITAMBUA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL* (Imekuwa ni Sheria yao israel kwamba ni Makao makuu tangu mwaka 1950)

Lakini Hapa anasimama Huyu *Rais wa Marekani (Donald Trump)* Kulitangaza hili kwa mara ya Kwanza kwamba anaitambua Yerusalemu Kama makao Makuu ya israel mwaka 2017, na Kuamua Kuhamisha Rasmi ubalozi wake Kutoka Telhaviv(Makao makuu ya awali ya israel) na Kupeleka Rasmi Yerusalemu Siku ile ile ambayo ndiyo Kulikuwa na Jubilee ya Miaka 70 ya Israel

✍Usikose kufuatilia sehemu ya 5⃣ ya Mfululizo huu ambapo utajifunza mambo mengi yajayo tunayotarajia kuyaona yakitokea kabla Kanisa halinyakuliwa.Ila Mpaka hapa Jiulize wewe umejifunza Nini?

Mungu anakupenda sana ndugu yangu ndio maana amekupa hamasa Kuyafuatilia na kulisoma Somo hili,anataka likupe kujiweka tayari na Unyakuo ambao upo karibi sana kutujilia!Je utaendelea na maisha haya ya dhambi uliyo nayo❓ Inawezekana ni kweli umekoka lakini unayaona maisha yako kama huyaelewi elewi hivi,unajikuta unaanguka anguka kwenye dhambi,Unajikuta hauna uwezo wa kushinda dhambi❓Inawezekana ni kweli ulishawai kuokoka ila umerudi nyuma,Je utaendelea na maisha hayo?

Nisikilize Ndugu yangu neema bado ipo,Usijihukumu kwa dhambi unazotenda au ulizotenda,Mungu anaangalia umaliziaji sio Uanzaji.ikiwa unahitaji uwezo wa Kushinda dhambi au unahitaji maombi ili upate Nguvu za Kumalizia basi wasiliana nami nitakuombea utapokea nguvu hiyo mpya

*♨Kwa mawasiliano zaidi au Ushauri*

*Na: Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
*MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳SOMO LA 5⃣ : VIASHIRIA VYA KUBOMOLEWA VYA MSIKITI WA AL-AQSA(DOME OF THE ROCK)✳*

* Na :Shujaa Charles Mwaisemba*

*KUBOMOLEWA KWA MSIKITI WA AL-AQSA(DOME OF THE ROCK)*

*ONYO KWA KWA WAKRISTO KUSHABIKIA KUPINGA ISRAEL*

* NGUVU ZA MAPINGAMIZI KUONGEZEKA KUTOKANA NA MUDA MCHACHE WA SHETANI ALIOBAKIZA KUFANYA KAZI DUNIANI*

* NINI WAJIBU WETU WA KUFANYA BAADA YA YOTE❓*

*1⃣ UTANGULIZI*

✍ Tukumbuke kuwa Mara baada ya Rais Donald Trump Kutangaza Kuutambua Mji wa Yerusalemu kama Makao Makuu ya Israel,Lakini hata Israel walikuwa na Sababu ya Kuhamisha makao yao Makuu Kutoka Telhaviv Kwenda Yerusalemu kwasabbu mambo mengi ya Muhimu Yapo Yerusalem Kama
i) Bunge la Israel lipo Yerusalem
ii)Makao ya Viongozi wa juu wa nchi yapo Yerusalemu
iii)Ofisi nyingi aa kiserikali zipo Yerusalem

Kwahiyo imekuwa ni makao yao makuu tangu mwaka 1950 kisheria yao,Lakini kusimama kutangaza ndio ilikuwa ni shughuli kubwa na ngumu ambayo ndiyo imetekelezwa na Taifa la Marekani.Ndio maana umeona Roho ya mpinga Kristo imesimama kwa nguvu kubwa,wote wenye roho hii ndio hawa wanapiga kelele kwasababu shetani ameshuka akiwa na ghadhabu nyingi akiwa anajua wakati wake upo karibu

Tukishakuyaelewa hawa tuendelee mbele na ikiwa hukufuatilia masomo yaliyopita basi wasiliana nami kwa namba nilizoandika mwishoni chini,Nitakupatia kuanzia mwanzo mpaka tulipofika

*2⃣ VIASHIRIA VYA KUBOMOLEWA KWA MSIKITI WA AL-AQSA(DOME OF THE ROCK)*

Kutangazwa kwa Yerusalem kama Makao yao makuu ya Israel,Kumeanza Kuonyesha viashiria vikubwa vya kuanza Kubomolewa kwa ule *Msikiti wa Dom of the Rock* Maana ndipo kulipokuwepo lile hekalu la Suleiman lililobomolewa kabla ya Israel kutawanywa kwenda kila kona duniani

Kumbuka Shauku yao Kubwa Israel si tu ilikuwa Kuipata Yerusalem yao bali hasa walitamani Kurudisha hekalu lao lililobomolewa mahali pale pale ulipokuwepo huu msikiti wa Al-aqsa,Hivyo Hilo Hekalu la 3 Suleiman lazima lijengwe tena hapo hapo

Maandiko yanasema Chukizo la Uharibifu litakaposimama hapo patakatifu (Chukizo la uhatibifu ni Mpinga Kristo) yaani atasimama hapo kulipo na hekalu.

Kwanini nasema viashiria vya kubomolewa huu msikiti upo tayari kuonekana ni kwasababu hivi tunavyozungumza Kwa Miaka mingi Vifaa vyote vya Ujenzi wa Hekalu vimekwishaandaliwa na vimeandaliwa kila kitu kuhusiana na hekalu hilo ambalo lazima lijengwe ndipo chukizo la uharibifu linalotajwa ambalo alizungumza Yesu Kristo alipokuwa anazungumza juu ya kuja kwake katika *MATHAYO 24:15-21* Aliulizwa juu dalili ya kuja kwake na ya mwisho wa Dunia *MATHAYO 24:1-3* Aliwaeleza kuwa hekalu kuwa litabomolewa

Dhiki kubwa inakuja baada ya kunyakuliwa kwa kanisa na huyu mpinga Kristo ndipo anatajwa atasimama kwenye hekalu hilo ambalo litajengwa baada ya huo msikiti wao wa Al-aqsa kubomolewa

Vifaa vyote vilishaandaliwa kabisa na Israel wameandaa kila kitu kama ilivyokuwa nyakati za suleiman,Zaidi sana wameandaa mpaka Mavazi ya Makuhani yote yapo tayari.
Na Jengo lile ujenzi wake sio kama tunavyojenga hivi sas kwa ujenzi aa kawaida,hivyo ingechukua Miaka Mingi kukamilika bali wameandaa kwa kutumia Technologia za kisasa kabisa yaani ile filimbi itakapolia,Ni kuta zinainuka,zinainuka,zinaungwa na kuungwa Kama unaunganisha vyuma,Ni kitu kinasimama tu kufumba na kufumbua kila kitu kipo mahali pale

Yaani sasa inangojea tu filimbi(Tangazo) na hichi ni kishiria kikubwa kwasababu huwa wanapata nguvu kuwa hapo ni kwao,hivyo wanaona pakishakuwa ni makao yao makuu basi wana haki ya kujua mji huu wanaufanyeje?Ndio maana unaona hawa wengine wanapiga kelele,Ndio maaana Palestina ndio wanaosema hii Yerusalem Mashariki ndio makao makuu ya nchi yao,itakayokuja‼

*3⃣ ONYO KWA KWA WAKRISTO KUSHABIKIA KUPINGA ISRAEL*

Sasa unapoona Tangazo la Mji wa Yerusalemu kutambuliwa kama makao makuu na Ikiwa wewe ni Mkristo ambaye unajua Neno,Unajua kuhesabu Miaka,Unajua Kusoma vitabu na kuhesabu miaka hupaswi kuwa upande wa mashetani bali utakuwa upande wa Israel(Katika unabii kuwa upande wa Israel ni kuwa Upande wa Mungu).Ukiibariki Taifa la Israel na wewe utabarikiwa,Iombee Amani Yerusalemu

Hivyo na wewe ukikurupuka na kuchukuliwa na na micoment ya watanzania ambao hawajui kupambanua kipi cha Mungu na kipi cha Shetani ambao hao hao ndio waliweza Kuchukuliwa na Babu wa Loliondo na kudai ni Mungu basi nawe utakuwa upotevuni maana siku zote wanashabikia vitu vya upande wa pili vya kishetani

Lakini hapa ndio tujue Miaka 70 imefika tayari ya taifa la Israel(14/5/2018) Asomaye na afahamu kuhesabu miaka na kujua jinsi tulivyo karibu kiasi gani na hili Chukizo la Uharibifu(Mpinga Kristo) ambaye atasimama muda si mrefu kwenye hekalu hilo litakalojengwa baada ya Msikiti kubomolewa

Unaweza kuona mbele yetu ni muda gani upo❓ Ni Muda mfupi sana ndugu yangu

Hakuna ajuaye siku wala saa lakini ni muda mfupi hapa,Chukizo la uharibifu litasimama katika hekalu ambalo maandalizi ya ujenzi wake upo tayari ndipo dhiki kuu inakuwepo, Na Kumbuka dhiki kuu ikiwepo ujue kanisa limekwisha nyakuliwa

⚠ Kwa hivyo chochote cha kufanya yote haya kutimia, kitakuwa na Upinzani sana,kutakuwa na matukio mazito mazito ya kupinga Tangazo hilo na mengineyo mengi Kama haya Maandamano ya Palestina ambayo yaliyokuwa yanaendelea mpaka sasa

*4⃣ NGUVU ZA MAPINGAMIZI KUONGEZEKA KUTOKANA NA MUDA MCHACHE WA SHETANI ALIOBAKIZA KUFANYA KAZI DUNIANI*

Kuanzia sasa na kuendelea tutaanza kuona matukio mengi ya Mapingamizi na kelele nyingi kutoka kila kona dhidi ya maamuzi hayo Kwasababu Shetani anajua Muda wake si mwingi kwasababu dhiki kuu ni Miaka 7,Na dhiki kuu ikiisha kanisa lililonyakuliwa na Yesu linakuja duniani na Yesu anatua kwenye mlima mzeituni mahali pale pale alipopaa wakati anaenda mbinguni, akiwa na Jeshi la watakatifu walionyakuliwa ambapo kutatokea vita inayoitwa *VITA VYA HARMAGEDONI* na baadae Utawala wa miaka 1000 wa Yesu Kristo dunia *(Ikiwa haujapata mfululizo huu matukio haya ya siku za Mwisho pia unaweza kuwasiliana nami nitakupatia)*

Wakati huo wa miaka 1000,Shetani atakuwa amekamatwa na kufungwa kwa miaka hiyo hiyo 1000.Hivyo ile tu Kanisa linanyakuliwa kuna miaka 7 tu ya dhiki kuu,Na baada ya hapo shetani anakamatwa kufungwa miaka 1000

Hivyo Shetanj anajua haya,Anajua viashiria vyake kwa hiyo anapoona hatua hii inaanza na hii nyingine inaanza, kadiri inavyosogelea ni mapambano, ni vita vikali utaona dunia lote linakuja kwa nguvu zote,huwezi kutegeme kuona *Jumuiya ya nchi za ulaya* ikisapoti hili wakati hicho kinachofanyika ni cha kiMungu
Kumbuka hata hizo sarafu za Euro zina michoro ya 6⃣6⃣6⃣ zimewekwa pale,Na Jengo lao zima lina mavitu ya ajabu ajabu hivyo huwezi kutarajia sapoti ya jambo hili kuunga mkono kutambuliwa kwa Mji wa Yerusalem

Kinyume chake ndio utaona Mapambano na Maneno mengi ya kupinga uamuzi huo uliofanywa na Rais wa Marekani,Kwahiyo na wewe Ukiwa Upande huo wewe ni Mjinga,Hujui Neno wala hujui Wewe ni Nani❓Hujui hata kilichopo mbele yetu lakini unachukuliwa na siasa za wajinga katika nchi yetu na dunia kwa ujumla

*5⃣ NINI WAJIBU WETU WA KUFANYA BAADA YA YOTE❓*

Kwasababu hii tuukomboe wakati kwasababu tujue hatuna muda mwingi unaotusubiria,Kama hujafa basi siku ya mwisho kwa watu wote nayo haipo mbali *(Sisemi kuwa Yesu anarudi lini kwamba ni kesho au kesho kutwa bali ni bado kitambo kidogo Yeye hajae atakuja wala hatakawia)*

Sasa itakukuta Umefanya kazi gani ya Mungu❓ Tangu umeokolewa hutaki kujihusisha na kuwaleta watu kwa Yesu unadhani kazi hiyo ni ya Mchungaji wako au wainjilisti fulani❓ Unategemea kwenda kufanya kazi ya Mungu kanisani bali unachukuliwa na shughuli za dunia hii‼ .Itakushangaza Yesu atarudi atakuacha Ukiwaza kufanya mambo mengi ya kidunia bila kuwaza na kufanya kazi ya Mungu

Au Je itakukuta upo Safi kwenye maisha ya Utakatifu au Unachanganya masomo tu(Vuguvugu)❓ Je itakukuta unaliishi Neno hili hili❓ Maana ni Kanisa Takatifu tu ndiolitakalonyakuliwa *WAEFESO 5:25-27*

Ndugu yangu wewe ndio unayafahamu Maisha yako ya sirini,Ni kweli inawezekana unasali kanisani na unafanya hata huduma lakini maisha unayoishi unayajua sio ya usafi‼ Maisha yako yamejaa unafki,Unafanya dhambi sirini kwa makusudi eti unasema unatubu kimya kimya‼ Ndio maana maisha yako yapo vile vile hauoni tena ile furaha ya wokovu,Amani imepotea kabisa wala hufurahii Neno kama Mwanzo,Unaenda kanisani kama desturi na mazoea‼ Na Kwambia ndugu yangu hivyo ulivyo unaenda Motoni kama hujashtuka Ukaamua Kugeuka Leo na kuanza Upya Yesu anakuja kutunyakua ila wewe utaachwa kama utaendelea na maisha haya uliyo nayo ambayo umeshayazoe

Ndugu yangu na wewe ambaye unasoma Ujumbe huu ambaye bado hujaokolewa au unajiita umeokolewa ila hauna badiliko la kweli la maisha,Kila siku unatubu ila upo vile vile,Unajikuta lile usilopenda kulufanya ndilo unalifanya na unalopenda kulifanya ndio hulifanyi‼Yaamkini unatamani Kumpendeza Mungu ila unashindwa unajikuta unaendelea katika dhambi‼ Unajifahamu wewe ni Mwenye dhambi wala unafki ndani yako,huu si wakati wa kujihesabia haki kwa dini zetu eti mimi dini Fulani,Yesu haji kunyakua dhehebu fulani au dini fulani bali anakuja kulinyakua kanisa takatifu❓ Je wewe ni Mtakatifu❓Huu ndio wakati wa Kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha nawe utapewa uwezo wa kushinda dhambi na kusamehewa dhambi zako zote na utakuwa sehemu ya watakaonyakuliwa

Je Wewe nawe ni Miongoni mwa wale waliokuwa wanampenda Mungu hapo mwanzo ila ilifika siku wakaanguka na kuacha wokovu na sasa upo mbali,unaishi maisha kama mtu asiyemjua Mungu❓ Sasa kwa somo hili Mungu amelileta kwako ili nawe usiachwe!Wewe ni mteule wa Mungu!Ni kweli shetani atataka kuwapoteza hata yamkini walio wateule ila hataweza kwakuwa watu kama ninyi ni wepesi kuisikia sauti ya Mchungaji wenu Yesu Kristo anapowaita.Kwa Ujumbe huu Mungu anakuita urudi kundini,Utubu nae atakupokea nawe utakuwa miongoni mwa watakaonyakuliwa muda mfupi Yesu akija‼ Ebu kumbuka ulipoanguka ukatubu,ukumbuke upendo wako wa mwanzo

▶Hivyo huu si wakati wa kuchanganya masomo,Lazima ujue viashiria hivi vinatupa kujua muda uliopo mbele yetu ni mfupi sana hatujui siku wala saa ila hatuna muda mrefu,Kinachowezekana kufanyika leo kisingoje kesho hivyo ikiwa unahitaji Msaada wowote Kati ya mambo niliyo yataja Ikiwa hujaokoka na unahitaji Uwezo huo wa kushinda dhambi na kukoka basi utawasiliana nami ,Vivyo hivyo ikiwa ulirudi nyuma na kuacha wokovu vile vile unaweza kuwasiliana nami kwa ushauri zaidi na maombezi ili tumalize safari kwa nguvu maana Mungu anaangalia umaliziaji si uanzaji

▶ Ikiwa Umeokolewa hakikisha unatafuta kanisa linalohubiri wokovu na kufundisha mafundisho ya utakatifu na wokovu kama hivi iki uzidi kuukulia wokovu na ujitambukishe hapo Kuwa umeokoka ila kama utahitaji Ushauri pia utawasiliana kwa namba zangu hapa chini

Mpaka kufikia hapa tumefikia Mwisho wa Mfululizo wetu wa masomo yanayohusiana na kutambukiwa kwa Yerusalem kama Makao makuu ya Israel,Natumai umejifunza Mengi mpaka kufikia hapa basi usiache kushare na kuwasaidia wengine ndani na nje ya kanisa ili nao wawe miongoni mwa watu watakaonyakuliwa siku ike Yesu akiwwa Mawinguni.Mungu akubariki kwa kufuatilia na ikiwa una swali au ushauri au lolote usisite kuwasiliana nami
 
*MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEM KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳SOMO 1: KUFUTWA KWA TAIFA LA ISRAEL✳*

* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*

* TANGAZO RASMI LA RAIS WA MAREKANI DHIDI YERUSALEM*

*UTABIRI WA YESU KUBOMOLEWA KWA HEKALU*

* KUFUKUZWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA KUBOMOLEWA KWA HEKALU*

*1⃣UTANGULIZI*

Kwa muda mfupi sasa umepita kumekuwepo na mijadala mingi sana katika mitandao ya kijamii,Magroup ya whatsap na Forum mbalimbali kote duniani kujadili juu ya hili swala la Israel na Palestina hasa Kuhusu Marekani kuutambua Mji wa Yerusalem kama makao makuu ya Taifa la Israel na juu ya Marekani kuhamisha ubalozi wake kuupeleka Yerusalem

✍Jambo hili limechukua sura mpya sana katika vyombo vya habari na Magazeti na mijadala ya wiki nzima ambapo wengi wasio na maarifa ya Neno la Mungu wamechuliwa na Upepo na wimbi la roho ya Mpinga Kristo Kupinga vikali juu ya Uamuzi uliofanywa na Rais Marekani dhidi ya jiji Yerusalem.

✍Ni makusudi ya Mfululizo huu kwamba kila mmoja si tu awe na maarifa sahihi bali awe upande wa Mungu kuzipinga roho zote za Mpinga Kristo zinazoletwa kupinga Unabii wa Mungu usitimie au Mapenzi ya Mungu kwa Kanisa na Israel kwa Ujumla Usitimie.Hivyo ikiwa umeanza nami kwa somo hili hakikisha unafuatilia mpaka Mwisho wa Mfululizo huu ambao utakuwa na masomo kadhaa ambapo tutajifunza mambo mengi ya kibiblia na Unabii wa Miaka 70 juu ya Israel na kanisa na mengine Mengi ambayo Masikio yako yatawasha yakiyasikia kwamba Kumbe yaliandikaa kwenye biblia⁉

*2⃣ TANGAZO LA RAIS WA MAREKANI JUU YA YERUSALEMU*

Mwishoni kabisa wa mwaka 2017,Dec ,6 Rais wa Marekani, *DONALD TRUMP* Alitoa Tangazo kubwa la kutangaza Rasmi kuutambua Mji wa Yerusalem kuwa ni Makao makuu ya Israel, na kudai kuwa Yerusalem tangu Mwanzo Kabisa ulikuwa ni Israel na ulitambulika kama *MJI WA DAUDI {2SAMWELI 5:4-9 }* Jambo ambalo lilisisimua dunia kwa ujumla wake kwa Tamko hilo

Lakini baada ya Tamko na Tangazo hili kwa Ulimwengu,Yameinuka mataifa mengi ambayo yamesimama na kupinga vikali Marekani Kufanya hivyo kuwa eti wanahatarisha Amani ya dunia.Lakini ni Muhimu kuelewa Mataifa mengi hayo yanayopinga ni kwasababu ya Roho za Mpinga Kristo zinafanya kazi ndani yao wasijue undani wa maswala ya kiroho kwa jambo hilo

Ni muhimu kuelewa kuwa Kutangazwa kwa Yerusalem kama Makao makuu ya Israel,kuna viashiria vikubwa sana katika siku za Mwisho

*3⃣ UTABIRI WA YESU,KUBOMOLEWA KWA YERUSALEMU*

✍Mwisho Kabisa kabla ya Mateso yake Bwana Yesu akiwa anauingia Mji wa Yerusalemu katika huduma yake duniani *ALIULILIA MJI WA YERUSALEMU* akatamka maneno haya katika
*♨{ LUKA 19:41-44}*
_"Alipofika karibu aliuona mji, *akaulilia*,akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.Kwa kuwa siku zitakuja, *adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini* wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, *kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa* kwako. Yesu Atakasa Hekalu"_

Yesu aliwaeleza kuwa Yerusalem Mzima itabomolewa Kwakuwa Wayahudi walikuaa wakiringia sana hilo Hekalu la Suleiman ,Hawakuwa Tayari hata kumpokea Yesu kristo kama Masihi wao wala hawakumsikia kwa lolote lile ndio maana walikuwa waifanya hadi machukizo ndani ya Nyumba ya Mungu *(LUKA 19:45-46)*

Yesu alikuwa akitabiri na kusema kuwa Mji mzima wa Yerusalem utabomolewa na hekalu nalo litabomolewa wala halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa na ndivyo ilivyotokea

*4⃣ KUFUKUZWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA KUBOMOLEWA KWA HEKALU*

Kufukuzwa kwa Taifa la Israel kulikuwa kwa Awamu 2 tofauti
Miaka karibu 30 baadae baada ya kauli ile ya Yesu Kama tulivyoisoma,Basi ilipofika Mwaka 66 -70 B.K wayahudi walifanya uasi dhidi ya Mfalme na Himya ya Kirumi iliyokuwa inatawala,Hivyo kulitokea mapambano makali yapata miaka 4 ya vita hiyo dhidi ya israel Mpaka kupelekea Hekalu Kubomolewa

Tamko likatolewa kuwa Wayahudi hawatakiwi Yerusalem na waliteswa sana wakati huo na kuonekana kama wahaini,Hivyo kupelekea wayahudi wengi wakaanza kukimbia kwenhe miji yao na nchi yao ingawa kulikuwepo na Wachache walioendelea kubaki kwenye maeneo na miji yao ambayo haikubomolewa yote ingawa hekalu lilikuwa limeshabomolewa

Baada ya Tukio la kwanza la kubomolewa kwa Hekalu lile la Suleimani,Mwaka 118 B.K , *Mfalme Hadrian* alitokea na kuwaambia wale waliobaki kuwa wanaweza kuwepo tena Yetusalemu na kuwaahidi kuwa wataweza tena kujenga lile hekalu

Lakini muda si mrefu baada ya Wayahudi kuanza kujenga jenga makazi yaliyokuwa yameharibiwa ndipo wakaanza kumdai Mfalme huyo atimize ahadi yake ili waanze kujenga hekalu ,Lakini mfalme akawa tayari amebadilisha mawazo
▶ Aliwaruhusu Kujenga hilo hekalu lakini sio Pale pa mwanzo bali ni mbali kabisa na Eneo lile,Jambo ambalo wayahudi walilipinga kabisa
▶ Akawabadilikia zaidi na ile ahadi kwamba angekuwa Rafiki yao hakuitimiza bali alikuwa kinyume nao kabisa

Mwaka 132 B.K Ndipo israel wakafanya Uasi Mkubwa mwingine dhidi ya Mfalme huyo wa kirumi ambao uliitwa *Bar-Kokhba Revolt*( uasi dhidi ya Serikali) ambao ulikuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo.Ndipo kulipofanyika vita nyingine kubwa kuliko ile ya mara ya kwanza mwaka 132-135B.K na na ule mji wote ukavunjwa vunjwa kabisa na watu wengi waliuwawa wala hakukusalia nyumba iliyobaki,

Walipigwa Marufuku kwa Myahudi kuwepo kwenye Nchi ile,hivyo kupelekea hao waliobakia,wakakimbia na kutawanyika sehemu mbalimbali duniani ili litimie Neno lililotabiriwa katika unabiii kuwa *_" Israel watakapokuwa wameasi,watatawanywa na kwenda kila mahali kwenye kona zote za dunia"_*
*♨{EZEKIELI 36:16-19}*
_Tena, neno la BWANA likanijia, kusema,Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, *waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao*. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake.Kwa hiyo *nalimwaga hasira yangu juu yao,* kwa ajili ya damu waliyoimwaga juu ya nchi, na kwa sababu wameitia uchafu kwa vinyago vyao. *Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao*, naliwahukumu."_

*♨ {KUMBUKUMBU 28:64}*
_" *BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia*; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe."_

Hivyo ndivyo Israel walivyotawanywa na kufukuzwa katika Taifa lao na ndivyo hekalu hilo la suleiman na makao yao yote yalivyobomolewa bila kubakia jiwe juu ya jiwe lilisalia kule kama Yesu alivyosema ndivyo ilivyopelekea Tangu wakati huo Wayahudi walitawanyika na kwenda Pande zote nne za dunia kwani wengine walienda Afrika,Wengine Urusi,wengine Ulaya na mwisho wengine wakaenda Marekani baadae sana

Hapo ndipo hilo Taifa likafutwa na kutokuwepo tena kama Taifa la Israel,Bali Mfalme aliyekuwepo aliita jina jipya mji huo *AILIA-CAPITOLINA*

⚠ Ndugu yangu hapa ninapohitimisha kuhusu hili hatuna budi kujifunza kitu Kimoja ambacho nasi kitupe taadhari Kuwa Neno lolote alilolisema Yesu lazima litimie.ikiwa alisema Yerusalem itabomolewa wala lisisalie jiwe juu ya jiwe na kweli kihistoria na kimaandiko yakatimia

Oooh ndugu yangu unayefuatilia somo hili tusiyapuuze maneno ya Yesu aliyosema na kutabiri juu kuja kwake kulinyakuwa kanisa safi lisilo na doa wala waa *WAEFESO 5:25-27*,Tusipuuze tukawa kama hawa wana israel bali ndio uwe wakati wa kujiandaa kwa utakatifu ambao pasipo huo hakuna mgu atayemuona Mungu.Huu si wakati wa kuendelea kung'ang'ania dini zetu badala ya kutafuta wokovu Kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha.Si wakati wa kuendelea na wokovu vuguvugu,unafanya dhambi sirini ila kanisani unajionyesha ni mtakatifu

⚠Kama yalivyowajiria mabaya wayahudi kwa kutawanywa kutoka katika nchi yao ndivyo ambapo Mungu nae atakapokufukuza utoke mbele zake uende kwenye moto wa milele pamoja na shetani kwa maana uliyapuuza maneno kama haya yanayokutaka utubu ,uliyapuuza maneno kama haya yanayo yanayokuonya kuwa usiishi maisha ya unafiki na maisha ya Uvuguvugu,Ya kufanya dhambi sirini! *ACHA NAKWAMBIA ACHA‼* Mungu amekupenda ndio maana amekula nafasi usome ujumbe huu ili utubu, *USIPUUZE‼*.Ikiwa utahitaji kuanza upya na Bwana Yesu basi wasiliana nami kwa namba hizo hapo chini nami nitakuombea utapewa uwezo wa kushinda dhambi‼

*USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU ZINAZOFUATA ZA MFULULIZO HUU*

♨Kwa mawasiliano Zaidi
* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
What a shame, we spend so much time reading and understanding other people's history while our own is full of blank pages
 
Back
Top Bottom