Judgment Day: May 21, 2011 (Really?)

Judgment Day: May 21, 2011 (Really?)

Si kazi ya mwanadamu kusema lini ni kiama bali Mungu mwenyeme ataamua iwe lini
 
hiyo cku ya mpunga! Ngoja nimwambie mwajir wangu aniwekee mpunga mapema ile niiage dunia!
 
Wala msihangaike ndugu zanguni kuhusu siku ya kiama,hakuna ajuae lia MwenyeziMungu tu.
Siku hiyo ni siku ya kifo chako. kwani hakuna ajuae atakufa lini bali ni Mungu peke yake.
 
kwa maana hiyo zimebaki siku 8 tuuuu haya ngoja niponde mali kufa kwaja

Mmhhhhhhhh
mali yako isiguse
waambie hao wanaotangaza kihama
wakupe zao maana hawata zihiitaji
kama kifo chao kimefika.. ni wazo tu mmhhh
 
kiama naomba kije hata kesho nikapumzike kwa amani na I can't wait to reunite with all friends and relatives that passed away!!
 
Mi naamini kuwa kiama ni kufa kwako!Hawa jamaa sijui wana nia gani hasa,ngoja tuone hiyo cku!Mungu tusaidie.
 
Una mpango wa kwenda kokote katikati ya mwaka huu? Mie nilikuwa na mpango, na bado ninao, wa kwenda kushangaa wanyama huko mbuga ya Mikumi. Pia nina mpango wa kufanya marekebisho madogomadogo katika nyumba ninayoishi kwa sababu mwenye nyumba wangu kagoma kunikarabatia. Pia nina mpango wa kukutana na watu hapa kijijini na kujuzana hili na lile kama ilivyo ada kila siku.

Lakini ati pamoja na kuwa na mipango yote hii ambayo inasubiri utekelezaji jamaa wananambia ati tarehe 21 /05 /2011 dunia yetu inafika tamati, au kwa kiswahili rahisi ni kwamba tarehe hiyo ndio 'mwisho wa dunia', namaanisha ' Kiama'.

Waliokuja na habari hizi ni jamaa fulani huko Carlifornia, Marekani, ambao wanasemekana kutumia fursa hiyo kujiongezea umaarufu kwa kutafuta air time kwenye vyombo vya habari.

Jamaa hawa waliokuja na habari hizi za 'mwisho wa dunia' ni wafuasi wa dini ya Kikristo wenye msimamo mkali wanaoongozwa na mtangazaji wa radio, Harold Camping, anayetangaza katika radio ya Family Radio Network.
Akitumia mistari ya Biblia, jamaa huyu amesema kwamba dunia itafika tamati miaka 7 ,000 kutokea mafuriko makubwa katika uso wa dunia, na kwa mujibu wa kalenda yake ni kwamba mwisho wa dunia yetu ni Mei 21.

Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa Harold kufanya utabiri kama huu kwani mwaka 1994 kutabiri kuwa mwaka huo dunia ilikuwa ikifikia tamati lakini cha kustaajabisha hadi leo bado yupo pamoja na wafuasi wake. Siku zote amekuwa na namna ya kujitetea utabiri wake unapokwenda kombo, " Kuna wakati Mungu anakuonesha mambo lakini hakuoneshi kwa ukamilifu wote.

Ni miaka mitatu iliyopita ndipo Mungu amenionesha ukweli wote." Lakini mara hii, Harold amekuwa akisisitiza kwamba yuko sahihi kabisa tofauti na mwaka 1994 , na mara hii emungwa mkono na watu wasiopungua 50 , akiwemo Gary Vollmer, mwajiriwa katika wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ambaye amechukua likizo ya bila malipo, likizo inayokwisha tarehe 23 Mei.

Gary amesema hategemei kurejea kwa mwajiri wake kwani tarehe 21 Mei atakuwa ' amekwishanyakuliwa'.

Enewei, nimefurahi kufahamiana na kila mmoja tuliyekutana na kubadilishana hili na lile hapa kijijini. Iwapo kweli tarehe 21 litatokea la kutokea tukutane upande wa pili. Chiazzzzz.
Sijui libi watu watakua na akili njema za kuukubali ukweli?
Majitu yanadanganywa weeeee...lkin yanakubali tuuuu:
Ndio tatizo la kuwakubali manabii wa uongo uongo. Bible said: Yeremia 14:14.
 
Sijui libi watu watakua na akili njema za kuukubali ukweli?
Majitu yanadanganywa weeeee...lkin yanakubali tuuuu:
Ndio tatizo la kuwakubali manabii wa uongo uongo. Bible said: Yeremia 14:14.

Nabii wa ukweli nani? Manabii wote asili yao ni uongo tu! Yesu mwenyewe aliwaongopea watu kuwa atarudi si kitambo, tena wengine aliwadanganya kurudi kabla hawajafa!!!!! leo ni miaka zaidi ya elf mbili bado watu wanaamini kuwa huju jamaa atarudi!!
 
Mwisho wa Dunia utafika tu, haraka za nini?....Carry on with your life. Just beware of Manabii feki.......:A S-coffee:

..........................................................................Washindwe kwa Jina la Aliye Mbinguni,,,!!!:A S-omg:
 
Pole sana mwisho wa dunia ni siku ambayo wewe na nafsi yako mtakapo ondoka wengine watakao baki wanaendeleza libeneke
 
Please! please! transfer all your property and possessions to me before hiyo siku. Mungu atakulipa mema huko uendako.:yo:
 
Kama wahusika wanatumia Biblia, basi siyo lazima itakuwa siyo biblia hii tunayoijua wote. Kwa sababu biblia ninayoijua hata mimi inasema "Walakini, habari za siku ile na saa ile hakuna ajuaye, HATA MALAIKAWALIO MBINGUNI wala Mwana ila BABA PEKE YAKE"! [Mathayo 24:36]

Sasa hawa jama zangu habari za mwisho wa dunia wa tarehe 21 mei 2011 wanazipata wapi? Yesu anayeuwakilisha uKristo ndiyo aliyeyasema haya, sasa hawa jamaa zangu habari za Mungu wanawakilishwa na nani? Au wanadhani Mungu anaweza kufanyiwa utafiti kama mambo ya kisayansi tu?

Ninaamini kuwa tarehe 21 itapita na hakuna lolote litakalotokea, kitakachotekea ni aibu tu kwa hao walioleta unabii huo na pia watajulikana kuwa ni manabii wa uwongo kama biblia yenyewe inenavyo katika Mathayo 24:4-5; Yesu akajibu akawaambia, [yale waliyotaka kuyajua wanafunzi wake kuhusiana na mwisho wa dunia]Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi. Unaona!

Kwa ujumla hizi ni nyakati za mwisho, na hizo habari za akina 21 mei ni dalili mojawapo. Msingi wa uhakika wa habari hizi ni Mathayo 24:36 zaidi ya hapo ni uwongo!

Asante, nimeingia bila hodi; naomba mnikubali nyumbani mwenu, huko nje kuna watu wanakera wanasema habari za kuwatisha watu, nimekasirika nimejikuta nimeingia mpaka ndani bila hodi ili niwajuvya uwongo huo wa mchana kweupe.
 
Back
Top Bottom