Nashindwa kuelewa kuhusu hizi tabiri za mwisho wa dunia, sifahamu kama hawa watabiri wana mawasiliano ya moja kwa moja na huyo atakayeimaliza dunia, yaani MUNGU kwa mana kwamba kila akibadilisha mawazo anawaeleza?. Pili, Kijiografia mataifa au sehemu mbali mbali duniani zinafautiana kwa masaa, tarehe na siku kwa maana kwamba kuna sehemu ambazo tarehe 21/05/21 au kama ilivyobadilishwa kuwa 22/05/2011 itafika mapema kabla ya sehemu nyingine, sasa swali langu ni kwamba hizo sehemu zitaangamia kabla ya nyingie? Na kwa maana hiyo kwa kuwa tuna marafiki zetu katika maeneo kama China, Austarlia na mengine mengi ambayo yako mbele kwa masaa au siku, yataangamia kabla yetu wakati sisi tukisubiri tarehe 21/22/05/2011 ifike?