Judith Kapinga amesema Serikali imetenga takribani shilingi bilioni 4.6 kupeleka umeme kwenye maeneo ya migodi mkoani Ruvuma

Kadodo1

Member
Joined
Apr 18, 2024
Posts
25
Reaction score
24
SHILINGI BILIONI 4.6 KUPELEKA UMEME MAENEO YA MIGODI RUVUMA - KAPINGA

πŸ“Œ Asema Serikali itaendelea kupeleka umeme maeneo ya uwekezaji

πŸ“Œ Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji

Your browser is not able to display this video.

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali imetenga takribani shilingi bilioni 4.6 kupeleka umeme kwenye maeneo ya migodi mkoani Ruvuma.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Agosti 18, 2024 wakati akizindua Kituo cha Mauzo ya Makaa ya Mawe ya kampuni ya Market Insight Limited (MILCOAL), inayojihusisha na uchimbaji, uuzaji na usambazaji wa Makaa ya Mawe, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

"Hapa katika mgodi wa MILCOAL tutatumia takribani shilingi milioni 280 kuleta umeme, nguzo tayari zimeshawekwa na sasa hivi wataalam wameanza kazi ya kuvuta waya." Amesema Mhe. Kapinga

Ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati inatekeleza miradi ya kupeleka nishati ya umeme kwenye maeneo makubwa ya uwekezaji ikiwemo migodini.

Mhe. Kapinga amesisitiza kuwa makaa ya mawe ni chanzo cha nishati thabiti na ya kutegemewa katika maeneo ya uwekezaji mkubwa hususani viwandani.

Amewapongeza MILCOAL kwa uwekezaji huo ambao unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amewahakikishia wawekezaji kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu wezeshi na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inathamini wawekezaji.

Kuhusu Kampuni kuwajibika kwa jamii inayozunguka miradi kwa maana ya CSR, Mhe. Kapinga amesema Sera za Nishati na Madini zinatambua uwajibikaji wa Kampuni kwa jamii zinazozunguka miradi na hivyo ameitaka Kampuni ya MILCOAL kutekeleza suala hilo ipasavyo.
 
Tatizo la millcoal mkaa wao ni grad A mkali sana, inabidi wawe na marketing manager mzuri kwa ajili ya soko la china na ulaya.
 
Tatizo la millcoal mkaa wao ni grad A mkali sana, inabidi wawe na marketing manager mzuri kwa ajili ya soko la china na ulaya.
Hivi nilisikia kama haya mambo ya makaa ya mawe yanapingana na athari za tabia nchi kwenye mazingira sijaelewa limekaaje hili
 
Hivi nilisikia kama haya mambo ya makaa ya mawe yanapingana na athari za tabia nchi kwenye mazingira sijaelewa limekaaje hili
Mimi si mtaalam eneo hilo hivyo sina comment na hilo.

Ila huko Mbinga kuja Ludewa kuna mkaa mwingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…