HOJA Juhudi za kukwamua barabara ya Tatedo Goba zimeishia wapi? Tangu uchaguzi Hatumuoni Mbunge wala Diwani

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252


Your browser is not able to display this video.
Barabara ya Tatedo iliyopo katika mtaa wa Kunguru Kata ya Goba jijini Dar es Salaam ni kama imesahaulika, kwani licha ya juhudi zilizofanywa na wakazi wa eneo hilo, tangu mwaka 2020, mpaka leo hakuna mwitikio wa Serikali.

Barabara hiyo inayoingilia karibu na nguzo za umeme unaokwenda Zanzibar, ina matawi mwili, moja upande wa kushoto inaelekea hadi Kinzudi Salasala, na tawi kuu linaelekea hadi Mbezi Africana.

Maria Shinge anayeishi mtaa huo, anasema barabara hiyo awali ilikuwa nyembamba kutokana na ujenzi holela, lakini uongozi wa mtaa ulianza mikakati ya kuipanua ili ifae kwa ujenzi.

“Tuliwaambia watu waliosogelea barabara wavunje sehemu za nyumba zao ili barabara ipanuke na kweli, wengi walifanya hivyo,” anasema.

Anasema mwamko wa ukarabati wa barabara hiyo uliongezeka baada ya kufahamika kuwa aliyekuwa mlinzi wa Rais marehemu John Magufuli alikuwa akiishi huko.

“Kuna wakati Rais Magufuli alimtembelea msaidizi wake huku (mwaka 2020) na alishangazwa na ubovu wa hiyo barabara, akasema haiwezekani msaidizi wake aishi kwenye barabara mbovu kiasi hicho.

“Ndipo tukaanza kuona juhudi za ukarabati zikianza. Lakini baada ya kifo cha Magufuli, juhudi zote zikafa,” amesema.

“Kinachofanyika sasa ni kila mwenye uwezo kuweka kifusi pale anapoweza.

“Kuna wakati Kanisa la Kiinjili la Kilutheri walikuwa na sherehe ndio wakaleta malori ya kifusi kwenye eneo korofi lenye bonde, lakini mpaka sasa hali bado ni ngumu,” ameongeza.

Mzee Ludovick Boniface anayeishi Mtaa wa Kunguru anasema walielezwa kuwa mkakati uliokuwepo ni ujenzi wa kiwango cha lami urefu wa kilometa mbili.
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
“Tangu mwaka 2020 tumekuwa na juhudi mbalimbali za kujenga hii barabara, lakini kwa nguvu zetu wananchi hatuwezi peke yetu.

“Tulichokifanya ni kusogeza nyumba zilizokaribia barabara na kuziba maeneo yenye hali mbaya, lakini tunajua Serikali nayo ina mipango yake,” amesema.

Maelezo ya Diwani wa Goba

Diwani wa Goba, Meya wa Manispaa ya Ubungo​

Akizungumzia kero hiyo, Diwani wa Goba ambaye pia ni Meya wa Ubungo, Lawrence Mlaki amesema barabara hiyo imeshawekwa kwenye bajeti ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mwaka 2026/27 na ujenzi wake utakwenda hadi Mwaka 2030.

“Hii barabara tumeshaiweka kwenye mpango wa TATRURA wa mwaka 2026/27, ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni ujenzi wa maeneo korofi ikitengewa Sh35 milioni.

“Awamu ya pili itakuwa ni ujenzi wa makalavati na uwekaji wa zege, maana hiyo barabara itakuwa ni ya zege sio lami. Ujenzi utakwenda hadi mwaka 2030, kwani fedha zitakuwa zikitolewa kwa awamu,” amesema.
 
Hiyo barabara wakazi wa hapo wengi wanauwezo wa kuipambania kuanzia msaidizi huyo wa JPM,DC Gondwe,wakubwa kibao wanaitumia kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…