Juhudi za Miguna Miguna kurejea Kenya zakwama, azuiwa Berlin

Juhudi za Miguna Miguna kurejea Kenya zakwama, azuiwa Berlin

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Mamlaka nchini Ujerumani zimemzuilia wakili wa kujitegemea Miguna Miguna kuabiri ndege kwenda Kenya, Afrika Mashariki au nchi yoyote ya Afrika.

Miguna aliyetenda kosa la kumwapisha kinara za upinzani Odinga kama Rais alifurushwa nchini Kenya na passport yake kushikikiwa na mamlaka za Kenya kwa uhaini huo.

Jana mamlaka za mahakama ya ngazi ya juu ya Kenya ilitoa ruksa kwa Miguna kuingia Kenya na kutoa hukumu ya passport yake arudishiwe akifika tu nchini Kenya.

BBC

USSR
-----------

1578389316232.png

Wakili wa Kenya Miguna Miguna, amedai kuwa mamlaka nchini Ujerumani imemzuia kuabiri ndege ya kuja Kenya.

Bw. Miguna amesema kuwa tahadhari imetolewa kwamba asiondoke uwanja wa ndege wa Berlin kuelekea uwanja wa kimataifa wa JKIA au nchi yoyote ya Afrika.

Ndege ya shirika la Lufthansa aliyokuwa aabiri kuja Kenya ilikuwa imepangiwa kuondoka nchini Ujerumani saa tano na dakika ishirini na kuwasili Nairobi saa tatu na dakika ishirini na tano za usiku, majira ya Afrika Mashariki.

Hatua hiyo inajiri saa kadhaa baada ya mahakama ya juu nchini Kenya kutoa agizo la kuitaka serikali ya Kenya kutomzuia wakili huyo aliyefurushwa kurejea nchini humo.

Serikali ya Kenya imesema kuwa itashughulikia suala hilo ili kumsaidia mwanasiasa huyo wa upinzani kurejea nchini siku ya Jumanne, karibu miaka miwili baada ya kumfurusha kwenda Canada.

Wizara ya Mambo ya Ndani katika taarifa yake imesema, itazingatia agizo la mahakama la mwaka 2018 ambalo liliagiza serikali impatie Bw. Miguna na stakabadhi za kumsaidia kurejea nchini humo.

Mahakama hiyo pia ili amuru maafisa wa kutetea haki za binadamu kuruhusiwa kuingia katika uwanja wa ndege kufuatilia mchakato huo.

Miguna Miguna ni nani?

Miguna alizaliwa katika kijiji cha Magina, katika jimbo la Kisumu, magharibi mwa Kenya.

Bw Miguna amekuwa kiongozi wa kundi linaloitwa National Resistance Movement (NRM, Vuguvugu la Taifa la Kupinga Serikali), ambalo liliundwa na muungano wa upinzani wa National Super Alliance siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio ambao Bw Odinga alisusia mnamo 26 Oktoba mwaka 2017.

Bw Miguna baadaye alijitangaza kuwa Jenerali wa NRM.

Mnamo 30 Januari, siku ya kuapishwa kwa Bw Odinga kuwa 'Rais wa Wananchi', muungano huo uliorodheshwa kuwa kundi haramu na waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i.

Hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa Bw Miguna kujipata akikabiliana na serikali na nguvu zake.

Mwaka 1988, alikamatwa na serikali ya wakati huo ya Rais Daniel arap Moi.

Bw Miguna baadaye alitorokea Kenya ambapo alipata hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa.

Pia soma:
 
Wakati yeye anafurushwa Raila anakula bata!
 
Vipi tena amri ya mahakama inapuuzwa kwa Mara ya pili mtawalia?, MAHAKAMA iliamuru asifurishwe lakini alifurushwa, sasa MAHAKAMA imesema asizuiliwe, lakini amezuiliwa, wapi hadhi na Uhuru wa MAHAKAMA?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi tena amri ya mahakama inapuuzwa kwa Mara ya pili mtawalia?, MAHAKAMA iliamuru asifurishwe lakini alifurushwa, sasa MAHAKAMA imesema asizuiliwe, lakini amezuiliwa, wapi hadhi na Uhuru wa MAHAKAMA?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha. Atapata stakabadhi na ataruhusiwa kurejea Kenya
 
Hahaha. Atapata stakabadhi na ataruhusiwa kurejea Kenya
Hapana Tony254, katika hili tupo nyuma sana Africa. Tabia ya serikali za nchi za Africa kupuuza amri za MAHAKAMA zetu tulizojiwekea sisi wenyewe ni kitendo kinachotudhalilisha sana sisi waafrika.

Kwa miaka miwili sasa tangu MAHAKAMA ilipitoa hukumu ya kwamba arudishiwe Passport yake ya Kenya, serikali haijafanya lolote na bado inazidi kumsumbua, hii ni aibu sana na kwakweli inatia hasira sana. Ndio sababu Mimi ninamuunga mkono 100% yule mkulima wa kizungu anayekamata ndege za Tanzania, hizi Serikali za Afrika ni hovyo sana "sometimes".


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari sana, ila jamaa kwenye ujuuzi wa maswala ya sheria hanaga mpinzani.
 
magu ingilia kati mazeee! jiwe of afrikaaa!
 
Very true! Ni aibu sana!, ama kuna kitu serikali inajua yenye hatufahamu. Lakini hata hivyo inasikitisha sana, serikali kuto tii mahakama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom