Juice inaitwaje kwa kiswahili?

Kumbe,niliwahi kumsikia gwiji wa maigizo maruhumu Mzee Upara akisema nataka maji ya sharubati kwenye duka la juisi nikadhani anatania kwa kuita juisi maji ya sharubati,loo usichokijua kweli usiku wa kiza ,watanzania wengi hatujui neno sharubati
 
Sharubati
Hili neno la sharubati linatokana na juisi ya sharbati (itengenezwayo na matikiti). Nadhani haitakuwa vibaya kama "juice" itatafsiriwa kama maji ya matunda; kama kwamtoro alivyoandika.
 
Last edited by a moderator:
juice n 1 maji ya matunda/nyama n.k.; juisi (of grated coconut) kasimile, tui. 2 digestive/gastric ~ maji- tumbo. 3 (colloq) mafuta; umeme; gesi. juicy adj 1 -enye maji mengi. 2 (colloq) nayovutia (kwa sababu inaongelea tabia/kashfa za mwingine) give me all the juicy details leta umbeya wote. juiciness n.
 
Namaanisha juice za matunda yote kwa ujumla yanayokamuliwa.

Hii imeletwa tena humu? tulishaijadili sana ikaishia Juice kwa Kiswahili ni Maji ya Matunda so katika tafsiri halisi la neno Juice = Juisi
 
Kwa yale maneno tusiyokuwa nayo katika lugha yetu ya kiswahili kama Juisi tunaweza kukopa maneno(misamiati) toka katika makabila yetu na kutumia katika kiswahili. Lugha zote duniani zinakopa maneno toka katika lugha nyingine.
 

Mkuu naona una kamusi karibu. Mie nilisikia ikijadiliwa na akina Mzee Akida miaka ile na walikubaliana juice ni sharubati.
 
Mkuu naona una kamusi karibu. Mie nilisikia ikijadiliwa na akina Mzee Akida miaka ile na walikubaliana juice ni sharubati.

ni kweli mkuu hata mimi nilisikia wakihitimisha kuwa ni sharubati, lakini nashangaa hii dictionary ya TUKI inasema ni maji ya matunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…