Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Viwanda vyetu hususani kama vya Azam vijiandae kwa maumivu kwani itakuwa ngumu kushindana na maviwanda ya Kenya. Pia na sisi tunaotaka kujenga tujumba twetu tujiandae maumivu kwani cementi ya kutoka viwanda vyetu ambayo ina ubora wa hali ya juu hususani ile ya Dangote, kiasi kikubwa kitakuwa kinaenda Kenya kwani huko itauzwa bei kubwa. Hii ndiyo win win situation? Tunapata juice kwa bei nafuu na kupata sementi kwa bei ya juu zaidi.

Pia majadiliano ya EPA yameanza ili bidhaa kutoka nchi za Europa nazo ziingie Tanzania bila vikwazo kushindana na bidhaa za viwanda vyetu. Hili ni jambo jema ili kuvifundisha adabu viwanda vyetu ambavyo kila kukicha vinatupandishia bei ya bidhaa zao. Mafuta ya kupikia, sukari na kadhalika bei zake hazikamatiki.

Ndio wanapaswa watanuwe akili zao ili waweze kuleta vitu bora kwa bei nzuri kuwashinda wakenya
Wataweza? Viwanda vya Kenya na vya European Union vina uzoefu wa miaka mingi. Nishati ya umeme kwao ni senti 0.004 ya dola kwa unit wakati sisi ni senti 20 ya dola kwa unit (= TZS 500). Sasa tunatarajia kujenga bomba la kupeleka gesi yetu kutoka Mtwara hadi Kenya kwa bei nafuu ili viwanda vyao vipate nishati ya bei nafuu zaidi ili juices zao watuuzie kwa bei nafuu zaidi.
 
Ukiachana na nishati, vipi kuhusu mikopo ya riba nafuu huko EU, kupata mkopo wa riba ya 1-3 % huko ni kitu cha kawaida, bongo ni kiwanda gani kinaweza pata huo mkopo, SSH anatengeneza bomu la kujitakia, upuuzi mtupu.
 
Tutakuja kujua baadae kuwa hatuna rais, ila wacha tupige miruzi na vigelegele kwa Sasa!

What's going to happen is an influx of Kenyan made goods in Tz, our export will be totally reduced hence decline of our currency due to higher importation of goods than exportation.

Rais huyu anajaribu kuivua chupi nchi ili kila taifa lijipigie litakavyo, soon ujanja ujanja wa Kenya dhidi ya Tz utarudi kwa Kasi.
 
1622581635644.png

Tunaisubiri kwa hamu.
 
Back
Top Bottom