Juice na unga wa ngano kutoka viwanda vya Kenya vitaingia Tanzania bila vikwazo na sementi kutoka viwanda vya Tanzania vitaingia Kenya bila vikwazo

What about influx of TZ goods in Kenya? Why sie tunajiwekaga kinyonge kinyonge tu? Sasa tunazungumzia soko la Africa. Unadhani tutaendelea kujifungia milele?
 
Makubaliano ni ngano ya Kenya kuuzwa Tanzania and not vice versa. Sisi tunaruhusiwa kuuza Kenya sementi na gesi tu, siyo ngano.
Hapa umechapia kabisa! Hakuna kitu kama hicho.

Vikwazo vimeondolewa potepote kama itifaki inavyotaka.

Kwa nini unapotosha? Yaekekea una ajenda yako.
 
Viwanda vinatakiwa vishindane kwenye free market,ukiritimba wa soko umepitwa na wakati, ambaye hawezi akae pembeni huo ndio mwelekeo wa uchumi wa dunia(survival of the fittest) na hapo ndipo mraji atapata manufaa,,kwani wewe hutaki manufaa? Swala muhimu ni Kodi za serikali zilipwe kwa ukamilifu wake.
 
Umesemaje paragraph ya mwisho?
Kenya wanajitahidi kwenye quality aisee , lakini sisi bongo ndio huwa tunapenda ujanja ujanja kwenye quality za goods zetu kwa kupenda kumlazimisha mtu anunue local manufactured substandards goods(Kwa kutumia protectionism) ,na kwa bei ambazo hata hazina unafuu,as compared to imported quality products! Tujaribu kutengeneza products zenye quality, ili ziweze kushindana na kupata masoko mazuri nje. Ubabaishaji kwa uchumi wa dunia ya leo' ni vigumu kutoboa..... That's a bitter truth ......na kazi iendelee.
 
Konyagi inavuka sana tu kwenda kenya , utaratibu ni kuwa Quality iwe ya juu
Konyagi ina alcohol level ya 35%abv , kebs wakipima wakaikuta ina 34.4% imekula kwako inarudi hata kama ulishalipa entry na fees zote.
Vipi kwa wale wanaopitisha kwa njia za panya mkuu ?
 
Hapa umechapia kabisa! Hakuna kitu kama hicho.

Vikwazo vimeondolewa potepote kama itifaki inavyotaka.

Kwa nini unapotosha? Yaekekea una ajenda yako.
Soma hayo makubaliano niliyoya attach ya gazeti la Buissines Times yaliyoandikwa kwa lugha ya malikia. Natumaini lugha hiyo unaijua vizuri.
 
Mkuu inauma sana aisee..vita vya uchumi sio lele mama aisee...ndio maana nasema washauri wa Raisi kwenye uchumi wawe wazawa wanao own viwanda ambavyo raw materials zao ni za wakulima na wafugaji sio wachumi waliopata PHD za kwenye kiyoyozi ambao hawajawahi hata kuuza bazoka...
 
Huyo huwa hana akili, kifupi huwa ni mduni wa hoja na kudharau akili za wengine kujifanya anajua sana.
Sidhani kama unachosema ni sahihi,pitia vizuri michango yake,yuko objective sana sijawahi kuona mchango wa kijinga kutoka kwake.
 
Itakuwaje feadher weight akashindanishwa na heavy weight kwenye mchezo wa boxing? Matokeo yake si ni kifo cha wazi?
 
Sijakuelewa ili viwanda vyetu visimame vinanzia Advanced teknoloji to local au Local to Advanced tecn?
Au visiwepo kabisa , au Waje wawekezaji na Advance tech? au vyote
 
Nafasi ya viwanda vyenu kuanzia huko chini imekuwepo kwa miaka karibu 60 sasa baada ya uhuru, lakini mie nafikiri imekuwa ni ubabaishaji mwingi tu, hivyo kwa uzoefu huu wa kushindwa kuibuka, mie naona mnahitaji 'kusaidiwa'!.... kazi iendelee.
Sijakuelewa ili viwanda vyetu visimame vinanzia Advanced teknoloji to local au Local to Advanced tecn?
Au visiwepo kabisa , au Waje wawekezaji na Advance tech? au vyote
 
Bams Uko sawa sawa hakuna watu majihil na wajinga kama Watanganyika yaani huyu mama anavowafanyia munaona sivyo mmezoea yule mm Raisi wa wanyonge akichanga shilingi mbili tatu kuwachangia ama kweli wajinga ndio waliwao .Mzoe Punda hapandi Farasi .Mama SSH nakupenda sana move on achana na wajinga anza kutoka ukaone mambo duniani mimi nitakupa vitu vitatu muhimu vya kuweza kuwa na maendeleo kwa haraka sana .UMEMEE (ENERGY) Bila ya kuwa na umeme wa uhakika huwezi kuwa na maendeleo tena uwe standard .
MAJI ya uhakika 24 hours yanatoka tena standard.Bara bara za uhakika tena ziwe standard . Health uwe na spitali za kisasa zinazo kidhi mahitaji ya wananchi wakati umefika kila wilaya kuwa spitali yake kubwa pamoja na clinic zake la mwisho na si la mwanzo Fungua nchi Kibiashara weka kodi za chini Dunia nzima itakuja Tanganyika kununua vitu wakiingia wageni kila kitu kinakwenda mbele kuanzia tax hoteli and restaurant.
 
Mkuu hakuna kitu expensive kama counterfeit au low quality products ,
Low quality tiles zitakufanya kila siku ukimbizane na mafundi ku replace hizo zilizopoteza ubora

Ni bora ununue ghali lakini mara moja kuliko kurudia rudia
Je watanzania wengi wana huo uwezo wa kununua izo ghali????


Usiangalie nafsi yako angalia tz nzima
 
Je watanzania wengi wana huo uwezo wa kununua izo ghali????


Usiangalie nafsi yako angalia tz nzima
Unaponunua kitu cha low quality , maana yake ni kuwa utatumia pesa nyingi kuliko yule aliyeamua kununua cha kitu bora kwa bei ghali
 
Waeleze Vijana hao..[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…