Juice ya maembe na karoti

Juice ya maembe na karoti

Lady niece

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
953
Reaction score
414
Mwadilla

Marafiki zangu leo tutajifunza namna ya kuandaa juice ya maembe na karoti

UTAYARISHAJI WAKE

Chukua maembe 5 au kiasi chako, chukua karoti 3, tangawizi kidogo,
kisha anza kuviosha kwa maji ya uvuguuvugu, weka kwenye sahani na
anza kumenya hayo matunda yako kwa usafi wa hali ya juu sana.
ukimaliza andaa blender, sukari kiasi kidogo sana

b) Anza kumenya vipande viodogo vidogo vya maembe weka kwenye
bakuri kisha menya karoti vipande vigodo vichanganye kwenye maembe
chukua tangawizi kidogo sana imenye na changanya na hayo matunda

c) Chukua blender yako weka hayo matunda mchanganyiko weka na maji
yaliyochemsha kiasi kidogo kisha anza kusaga matunda yako
hakikisha kuwa yanakuwa malaini sana kisha chuja pembeini kwenye
bakuli, weka sukari kidogo sana kama vijiko 5 vya chakula
koroga koroga mpaka ilainikie kwenye matunda hayo kisha weka kt
jagi lako na weka hiyo juice kwenye friji ili iwe baridi kiasi

Tayari umeshapata juice yenye mchanganyikko wa maembe na karoti
inafaa kunywa na mikate, keki, au chochote utatakachojisikia kunywa
nacho karibuni kwa mlo huo.
 
nitajaribu nami kuchanganya na apple nione inavyokuwa test yake

Izo carrots vizuri zichemshe kidoooogooo na sukari kabisa. Then.zikipoa ndo zisage hadi ziwe laini. Juice yake inakua nzito kdg. Na huna.haja ya kuchuja.
 
Izo carrots vizuri zichemshe kidoooogooo na sukari kabisa. Then.zikipoa ndo zisage hadi ziwe laini. Juice yake inakua nzito kdg. Na huna.haja ya kuchuja.

Mumie nakuaminia hapo afya tupu...!
 
Napenda fresh juice lakini hapo bongo juice fresh nyingi ukiletewa inatoa harufu ya uvundo.wenzetu mmezoea ila sio sawa
Kuna matunda na ujiuji wa matunda unanasa ndani kule kwa mashine na wauzaji wengi hawasafishi vizuri mashine zao.Then ule ujiuji wa matunda fikiria maembe au papai ukae wiki.then unanunua hiyo juice bakteria hao utahara mpk kigoma mwisho wa reli na kuendelea
 
aisee hili kwangu jipya kabisa acha nifanye hivyo nione ikoje na radha yake itakuwaje
asante mamito kwa kuniambia hili kwangu ni jipya kabisa sikulijua
Izo carrots vizuri zichemshe kidoooogooo na sukari kabisa. Then.zikipoa ndo zisage hadi ziwe laini. Juice yake inakua nzito kdg. Na huna.haja ya kuchuja.
 
Niibie siri Farkhina Zatar ninini ? Sitaki wengine wajue kwamba sijui

Zatar ni vimajani vikavu fulani vinaweka kwenye chai tamu sana vikikutana na hiliki mchaichai tangawizi na mdalasini wa vijiti basi hiyo chai utamu wake lazima unywe hadi uoge lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Thanx very much Farkhina ntamsuprise bebi wangu A.N
 
Back
Top Bottom