Juice za azam zina madhara yoyote?

Juice za azam zina madhara yoyote?

okon

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2008
Posts
305
Reaction score
92
Nimesikia habari za soda na madhara yake, sasa nimeamua kupunguza soda niwe nakunywa juice. Na juice rahisi kabisa kuipata ni ya Azam (napendelea zaidi ya box, mango). Sasa kuna mtu ananiambia eti juice hiyo haina tofauti na soda. Eti zote si nzuri kwa afya. Haya maneno ni ya kweli wadau? Sasa ntakunywa nini?
 
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya juice za Azam ni makemikali si matunda halisi kama wanavyotaka kudanganya watumiaji.Juice ya matunda halisi ni gharama sana kuitengeneza na wanachofanya Azamu ni kujaza makemikali ya kutosha kuharibu afya yako.

Nakushauri nenda sokoni nunua matunda tengeneza mwenyewe.Matunda katika masoko mengi ni rahisi sana ukilinganisha na haya makemikali ya Azam.
 
Una andika hivi huku ukiwa tayari umeshaingia maabara na kutest hiyo juice ikaonekana na hizo kemikali au unaongelea majungu tu hapa? Hebu jamani tujaribu au kama si kuacha majungu tafadhali.
 
Sasa kama ni makemikali tupu na hakuna matunda, yale matunda yote wanapeleka wapi? wanayatupa au? au hujui matunda ambayo azam hua inatumia kila mwaka? Afu si kila kitu kina madhara kiasi hicho kama mnavyokuza mambo, dunia siku hzi imejaa conspiracy theories sasa kila kitu kinaonekana hakipo sawa, ukianza hayo utabaki kuchukia hadi mafuta ya mboga unayotumia, chumvi, sukari kila kitu utabaki kula majani plain na hayo utasoma yako contaminated sasa utakula nini mwisho wa siku
 
Ndiyo maana nkakwambia asilimia kubwa ni kemikali.matunda halisi yaweza kuwa 10% tu.

Sasa kama ni makemikali tupu na hakuna matunda, yale matunda yote wanapeleka wapi? wanayatupa au? au hujui matunda ambayo azam hua inatumia kila mwaka? Afu si kila kitu kina madhara kiasi hicho kama mnavyokuza mambo, dunia siku hzi imejaa conspiracy theories sasa kila kitu kinaonekana hakipo sawa, ukianza hayo utabaki kuchukia hadi mafuta ya mboga unayotumia, chumvi, sukari kila kitu utabaki kula majani plain na hayo utasoma yako contaminated sasa utakula nini mwisho wa siku
 
Hapana ina madhara madogo madogo kama kuishiwa nguvu za kiume na kike katika mpango maalum,
 
Juisi za Azam ni marufuku kuingizwa soko la Kenya kwasababu hazikidhi viwango vya ubora kwa mujibu wa shirika la viwango la Kenya.

Sasa kama ni makemikali tupu na hakuna matunda, yale matunda yote wanapeleka wapi? wanayatupa au? au hujui matunda ambayo azam hua inatumia kila mwaka? Afu si kila kitu kina madhara kiasi hicho kama mnavyokuza mambo, dunia siku hzi imejaa conspiracy theories sasa kila kitu kinaonekana hakipo sawa, ukianza hayo utabaki kuchukia hadi mafuta ya mboga unayotumia, chumvi, sukari kila kitu utabaki kula majani plain na hayo utasoma yako contaminated sasa utakula nini mwisho wa siku
 
Juisi za Azam ni marufuku kuingizwa soko la Kenya kwasababu hazikidhi viwango vya ubora kwa mujibu wa shirika la viwango la Kenya.

Sio ushindani wa kibiashara na vile viwanda vya Thika Del monte?
 
Madhara pia yanatokana na artificial flavour na colour wanazoongeza zinasababisha cancer na pia sukari ni nyingi sana zinaweza sababisha kisukari au obesity cha msingi tafuta matunda sokoni tengeneza juice mwenyewe au kunywa maji
 
Artifial flavour, colour, preservatives, stabulizers E ngapi ngapi sijui..wanachanganya humo humo...my littlte biology inaniambia Ivo vyote vinasababidha kansa Hapo sasa kazi ni kwako kusuka au kunyoa
 
Ili kujua kitu ni fake, ni lazima kwanza ujue original kikoje!. Juice za Azam ni fake!, ndio maana ziko cheap hivyo, hata maziwa kwenye ice cream zake pia ni fake!. Ili kujua juice za Azam ni fake, nunua Ceres onja hala angalia tofauti!. Kama ni jiuce za embe nunua Maaza!.

Anachofanya Azam ni kuweka fruit pulp kidogo tuu, kisha anajaza kemikali za food colors, artificial flavours na sweeterners, ukinywa utaisikia inakereketa!. Hii ni kwa some juices, zile zilizo bora ndizo zilizopelekwa TBC na kupata nembo ya ubora wa TBS, Kenye walipopokea mzigo wa Azam, wakaupima, wakagundua ni fake!, hazina viwango, wakapiga marufuku juices za Azam.

Kutengeza juice home nayo ni changamoto!, kwanza you have to love eating natural organic products, then you can do anything in the name of love.

Pasco
 
With EAC free movement of goods si rahisi ki hivyo tatizo hapa ni ubora kiwango cha juice ya Azam ni hovyo sana.
Mimi huwa nashangazwa na wingi wa juisi za embe kulinganisha na maembe yanapatikana Tz! naungana nayi msioamini juisi za huyu mwenzetu kuwa halisi
Kinachotisha zaid ni haya mengine maazam nini sijui kila ladha zipo mh1
 
Mbaya zaidi kinachonisikitisha ni kuwa matunda mengi yanaoza tu masokoni huku wakijiona fahari kujaza majuice ya kwenye maboksi majumbani mwao. Hii inakosesha ajira kwa wakulima wetu waTanzania. Tengenezeni wenyewe homemade juices.
 
Nashukuru siko popote kwenye hizo juice. tunda nalila tunda kama tunda as long as naweza fatuna sina haja ya kupondewa kwa kweli... na kuchanganya na maji tunda nalila kama tunda na maji km maji mengne mbwe mbwe tuu
 
Daaahhh.....twafaaaa.....nawaonea huruma madogo wanaoshindana kunywa hizo juice kwa siku....hakika adi 2040 robo ya watz watakuwa na madhara yatokanayo na hizo kemikali..... bora kipindi sisi tunakuwa uko mikoan....hatukuwa tunajua vitu kaa hivi.....
Zetu ilikuwa ni soda kwenye sikukuu au akija mgeni unamtolea mimachoo weee mpaka unawekewa kwenye kikombe kidogoo tuu ili mradi nafsi yako iseme leo nimekunywa soda na kwenda kutambia wenzako kuwa leo umekunywa soda......
 
Ili kujua kitu ni fake, ni lazima kwanza ujue original kikoje!. Juice za Azam ni fake!, ndio maana ziko cheap hivyo, hata maziwa kwenye ice cream zake pia ni fake!. Ili kujua juice za Azam ni fake, nunua Ceres onja hala angalia tofauti!. Kama ni jiuce za embe nunua Maaza!.

Anachofanya Azam ni kuweka fruit pulp kidogo tuu, kisha anajaza kemikali za food colors, artificial flavours na sweeterners, ukinywa utaisikia inakereketa!. Hii ni kwa some juices, zile zilizo bora ndizo zilizopelekwa TBC na kupata nembo ya ubora wa TBS, Kenye walipopokea mzigo wa Azam, wakaupima, wakagundua ni fake!, hazina viwango, wakapiga marufuku juices za Azam.

Kutengeza juice home nayo ni changamoto!, kwanza you have to love eating natural organic products, then you can do anything in the name of love.

Pasco
Pascooo, shkamoo!
 
Back
Top Bottom