X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,605
- 1,843
Juisi Ya Melon Na Embe
Vipimo Na Mahitaji
- Tikiti la asali (honey melon)..............1
- Unga wa embe au embe...................1
- Tangawizi........................................1 Kijiko
- Ndimu..............................................1
- Sukari..............................................¼ Kikombe cha chai
- Arki rose..........................................2 Matone
Namna Ya Kutayarisha
- Limenye melon na ulikate kate kisha tia kwenye blender
- Tia unga wa embe au embe iliyokatwa katwa
- Kisha tia ndimu iliyokatwa vipande kiasi pamoja na maganda yake
- Halafu weka sukari
- Saga vizuri hadi ilainike
Mimina kwenye jagi kisha tia matone mawili ya arki rose ukoroge na tayari kwa kunywewa
Kidokezo:
Ukiweka ndimu weka na maganda yake unapata ladha nzuri zaidi.