Hakuna binadamu anayevumilia kukaa katika mazingira yasiyomweka huru. Tukubaliane tu kwamba uwepo wa vyama mbadala ulimaanisha harakati mpya za kubadilisha mawazo wa mfumo uliozoeleka na kutengeneza mtizamo mpya ulioimara kufanikisha kile kinachoitwa "ukombozi wa wanyonge". Wanaoitwa wanyonge, hawapo nje ya familia za hawa wanasiasa, ni wazazi wao, ndugu zao, jamaa zao, rafiki zao, wake ama waume zao na jirani zao. Tujiulize kwa pamoja, hawa wakombozi, wametawaliwa na ubinafsi kwa kiasi gani? Juhudi yao kama ina lengo moja, kukomboa, mbona wanabishana wenyewe? Ninadhani kuna haja kwa wakombozi hawa kufanya tathimini za kina kabla ya kwenda mbele ya umma, maana huku kwenye mashina yao hawana maisha tofauti na haya ya kubishana na pengine wapo wanaotamani hata kubadili koo zao. Tunapaswa kuwa wanamapinduzi, changamoto zipo, tusizikimbie wala kuziogopa, maana kama Zuma angeondoka kwenye Umakamo na kujiondoa ANC, basi Mbeki angeonekana mkweli mbele ya Dunia. Wakati ndio huu tuutumie vizuri!!