SoC01 Jukumu la kutengeneza ajira lianzie kwenye ngazi ya familia

SoC01 Jukumu la kutengeneza ajira lianzie kwenye ngazi ya familia

Stories of Change - 2021 Competition

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Asiye kujua hakuthamini, lakini vile vile uchungu wa mwana aujuaye mzazi, hakuna mzazi anayependa kuona mtoto wake anateseka au anaishia kuwa na maisha duni,

kila mzazi anashughuli inayomuingizia kipato cha kulisha familia na kuendesha familia, kwa kuajiliwa au kujiajiri,

Hapa nchini kwetu Tanzania watoto wanazaliwa kila siku (ukitaka kuamini tembelea wodi ya wazazi yeyote iliyopo eneo lako) hivyyo basi kuna ongezeko la watu kila siku, serikali inahitaji bajeti kubwa zaidi ili kuendesha nchi, haina pesa za kutosha ndio maana inaongeza wigo wa kodi kila kukicha, na kutokana na ongezeko hili la idadi ya watu ajira zinazotolewa zinakuwa ni chache.

kila familia ikiwa na ndoto kubwa ya kufikia malengo iliyojiwekea inaweza ikawa ndio njia bora ya kukuza uchumi nchimi kwetu na kutatua changamoto ya ajira.


Mfano kama baba ni mjasilia mali anajihusisha na kilimo cha mboga mboga na akawa na malengo ya familia kuwa siku moja atakuwa mzalishaji mkubwa wa mboga mboga na atapata mafanikio makubwa, sio vibaya akimuandaa mtoto wake kwa kumhamasisha na kumpereka akasomee Horticulture SUA ili alete maarifa yatakayo fanikisha kuifikia ndoto ya familia ya kupata msfanikio makubwa zaidi kupitia ķilimo cha mboga mboga,

MFANO WA PILI
Kama baba au mama ni mkurugenzi wa JAMII FORUMS, awe na ndoto ya familia ya kupata mafanikio makubwa zaidi, sio vibaya watoto wake akawasomesha na kuwahamasisha ktk mambo ya computer sxience, Information Technology n.k yaani wabobee huko ili waje walete mageuzi ktk kampuni ya mzazi,

MFANO NAMBA TATU,
Kama baba ni Fundi wa boda boda, sio vibaya akimpereka mtoto wake VETA au chuo kikuu akasomea Mechanical engineering ili aje kuleta maarifa yatakayosaidia kufanikisha ndoto ya familia,
Kama mzazi anamiliki PHARMACY basi mtoto alasomee mambo ya ufamasia abobee huko aje kuleta ujuzi utakao fanikisha ndoto ya familia,
Mifano ipo mingi sana.

Kila familia ikiwa na dira, ikiwa na jukumu la kumtengenezea mtoto ajira tangu akiwa mdogo na sio kumsomesha tu na kisha kumwaga ktk jamii akajitafutie maisha kama mamba anavyofanya kwa kuwaweka watoto wake mdomoni na kisha kuwatosa mtoni wakajitegenee. Mzazi awena jukumu la kuwajibika kwa mtoto kama baba ni daktari kaajiliwa serikalini basi ahakikishe anaanzisha chochote kama ni zahanati au ni biashara yeyote kisha awaandae watoto wake kwa kuwapa elimu inayoendana na kile alichowaandalia ili wafikie malengo ya familia na sio kumuachia mtoto au watoto urithi wa nyumba au kiwanja peke yake ambapo wanaweza kukiuza wakaishia kuwa na maisha duni.

Kila familia ikiwa na dira, ikiwa na malengo ikiwa na ilani, tutakuwa tumetatua tatizo la ajira na kukuza uchumi nchini kwetu, pia tutakuwa tumeongeza morali ya watoto ktk kusoma na kupenda kile wanachokisomea na sio kusoma ilimradi wapate vyeti, pia watakuwa wanasomea kile wanachoenda kukifanyia kazi .

Hatuwezi kutatua matatizo yale yale ya siku zote kwa njia zile zile, mabadiriko yanaanzia ktk fikra, mabadiriko ya Taifa yanaanzia ktk ngazi ya familia, familia yako yangu na yule zote kwa pamoja ndio zitaleta mabadiriko ya Taifa.

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA IKIWA YATAANZIA KTK NGAZI YA FAMILIA.

Ahsanteni na muwe na tafakari njema.
 
Upvote 3
Vijana wengi siku hizi tunaona kwenda chuo ni kupoteza muda wakati elimu ni mkombozi wa Taifa letu,

Wewe kijana mwenzangu kama ni wakala wa benki (CRDB, NMB n.k) wakala wa huduma za kifedha (TIGO PESA, MPESA n.k) mtoto wako unaweza kumshauri akasomee mambo ya fedha na usimamizi, Masoko, Tehama n.k ili akitoka huko chuo alete maarifa yake mtimize ndoto ya familia kuifanya biashara iwe kubwa zaidi na yenye manufaa zaidi, kuliko kumsomesha mtoto mambo ya kilimo, ualimu au kemia ambayo akimaliza huko hajui ataajiliwa wapi.

Mtoto akisoma kitu ambacho anajua akitoka hapo chuoni anaenda kukifanyia kazi kwanza atakipenda na kujiamini zaidi na atakuwa kafuata maarifa na sio vyeti huko chuomi,

Hii ndio njia itakayoweza kufanya vijana wawe na maisha bora na wabunifu waliobobea zaidi,

Leo hii kijana aliyesomea udaktari wa binadamu unamuambia akajiajiri kwa kuanzisha kilimo cha kisasa hapo mzazi unategemea nini?
Tunatengeneza Taifa la watu wanaoichukia elimu
Maradhi, ujinga na umasikini havitakwisha
 
Umesemaje
Familia zahapa bongo unazijua wewe hizi hizi za tasaf
Kuna faida gani baba Fundi magari kumsomesha mtoto shahada ya ualimu wa masomo ya sanaa ambapo akimaliza chuo hajui ataajiliwa wapi. Wakati kama angempereka VETA au chuo akasomea mitambo ya magari angerudi nyumbani na kumsaidia baba kukuza garage na baadae nayeye akafungua yakwake au kurithi hiyo ya baba yake. Kuna ubaya gani mkuu? Au mmekarili urithi ni nyumba na mashamba tu.

Mwaka huu baraza la wafamasia limesajili wafamasia wapya zaidi ya 1500, Baraza la wauguzi limesajili wauguzi wapya zaidi ya 1900
Na kila mwaka mabaraza yanazalisha maelfu ya vijana unategemea ifikapo 2035 ajira au nafasi za kujitolea zitakuwepo? Tutaanza kuona daktari wa binadamu akipiga debe stand,

Lama unabisha wait time will tell
 
  • Thanks
Reactions: pha
Kuna faida gani baba Fundi magari kumsomesha mtoto shahada ya ualimu wa masomo ya sanaa ambapo akimaliza chuo hajui ataajiliwa wapi. Wakati kama angempereka VETA au chuo akasomea mitambo ya magari angerudi nyumbani na kumsaidia baba kukuza garage na baadae nayeye akafungua yakwake au kurithi hiyo ya baba yake. Kuna ubaya gani mkuu? Au mmekarili urithi ni nyumba na mashamba tu.

Mwaka huu baraza la wafamasia limesajili wafamasia wapya zaidi ya 1500, Baraza la wauguzi limesajili wauguzi wapya zaidi ya 1900
Na kila mwaka mabaraza yanazalisha maelfu ya vijana unategemea ifikapo 2035 ajira au nafasi za kujitolea zitakuwepo? Tutaanza kuona daktari wa binadamu akipiga debe stand,

Lama unabisha wait time will tell
Luckdube!
 
Back
Top Bottom